NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, January 7, 2010

UDSM YATOA MILIONI NANE KUSAIDIA SHULE ILIYOHARIBIWA NA MABOMU MBAGALA

  • Katika makala yangu ya jana, niliyalalamikia makampuni kujikita katika sekta ya urembo na kuacha kusaidia sekta za msingi za kijamii kama elimu na miundo mbinu (hasa vijijini). Nimefurahi leo nilipotembelea blogu ya jamii, na kukutana na habari hii nzuri ambapo Chuo Kikuu cha Dar es salaam kimetoa msaada wa milioni nane kusaidia shule moja ya sekondari kule Mbagala ambayo iliharibiwa na miripuko ya mabomu. Huu ni mfano wa kuigwa kwa makampuni mengine, taasisi mbalimbali na hata watu binafsi. Picha na maelezo yote hapa chini ni kutoka blogu ya jamii.
*******************************************************************************

Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala (Mwenye suti) akikabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Milioni nane kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Mbagala Dar es Salaam Mwl. Marcelina Kimario ikiwa ni michango ya wafanyakazi na wanafunzi wa UDSM kwa shule hiyo ili zisaidie kukarabati sehemu ya madarasa iliyoharibika kufuatia ajali ya milipuko ya mabomu iliyotokea mwezi Februari mwaka jana.

Makabidhiano hayo yamefanyika shuleni hapo mbele ya viongozi akiwamo diwani Mh. Charles wa kata ya Mbagala Kuu, waalimu na wanafunzi wa shule hiyo. Wengine waliofuatana na Prof. Mukandala ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Jamii Prof. Amandina Lihamba (wa Kwanza kushoto), Mkuu wa Shule ya Elimu Prof. E. Bhalalusesa(wa kwanza kulia) na Mkurugenzi wa Rasilimali watu na utawala Bw. Edward Jambo (hayuko pichani).

1 comment:

  1. Inapendeza na kutia changamoto na hamasa kubwa pale wasomi wanapokuwa mstari wa mbele katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali yanayoikumba jamii. nami nimefurahishwa na mchango ambao chuo kikuu kimeutoa.

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU