NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, February 18, 2010

AFRIKA INAWEZA KUULISHA ULIMWENGU - RAIS JAKAYA KIKWETE

  • Hebu msikilize Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete katika "clip" hii ya dakika 1:42. Hapa ilikuwa tarehe 29/1/2010 alipokuwa akizungumza katika kongamano la Uchumi wa Dunia kule Davos nchini Switzerland.
  • Ni hotuba inayoonyesha welewa mzuri wa masuala ya msingi ambayo Afrika inahitaji katika harakati zake za kujikomboa katika sekta ya kilimo (ambayo ndiyo sekta ya msingi japo imetelekezwa) na hatimaye kuweza kujilisha yenyewe pamoja na ulimwengu mzima.
  • Kitu pekee ambacho Mheshimiwa Rais hakukitaja, na ambacho nadhani ni cha msingi kabisa, ni uongozi bora. Hata Afrika ikiwezeshwa kiteknolojia na kifedha kama anavyobainisha hapa, bila kuwa na viongozi makini na wenye moyo wa kweli wa kutaka kuwakomboa watu wao, itakuwa ni kazi bure. Ukosefu wa uongozi bora, kwa maoni yangu, ndiyo sababu mama inayoifanya Afrika iendelee kuwa katika paradoksi iliyomo - bara tajiri sana lakini lenye watu masikini sana!

1 comment:

  1. maneno kama hayo yanaweza kuwa ni ya kuashiria kuwa twahitaji wawekezaji kuja na hizo teke-nolojia.
    Je kuna haja ya KUBINAFSISHA uongozi bora kwa 'development partners'? (nakumbuka post moja hapa kijiweni wako ambako kuna mdada mmoja ambaye alisema hataki kuolewa na m-black kwa kuwa wamelaaniwa....lol)

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU