NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, February 26, 2010

FIKRA YA IJUMAA: ATI, KUNA NINI KATIKA OMBWE LA KUTOKUWAKO?

Hebu tuwaze: Kama kusingekuwa na cho chote, kungekuwa na nini?

**************************
 • Tuweko!

4 comments:

 1. kuna kutokuwepo! au kuna usichoweza kukijua kuwa kipo.

  ReplyDelete
 2. kungekuwa na hicho ambacho hakipo...lol

  you think so you are, i presume...lol

  ReplyDelete
 3. Kama kusingekuwa na cho chote, kungekuwa na nini?

  I have no idea. I never thought about this. Fikiria there is no earth, no planets, no the vastness of space, nothing...Kungekuwa na nini. Can't even think about it and I think it is a privilege that things (including me) were created. Sometimes I also think that it would have been better if I was never created...and this brings another question... where were things before they came to be? Before creation or before the big bang?

  This is turning out to be a mental exercise for me. Thanks for provoking my mind. Spend a lot of time thinking about girls...It is important sometimes to think about these philosophical questions..

  ReplyDelete
 4. Swali hili laja akilini mwangu kwa makundi mawili.
  Kwanza ni kutokuwepo kwa chochote kwa kuwa hakikuwahi kuwepo na pili ni kutokuwepo kwa chochote kwa kuwa kilichokuwepo kimechukuliwa.
  Tofauti ya haya ni kubwa lakini ntazungumzia kwa ufupi.
  Kama tusingekuwa na chochote kwa kuwa hatujawahi kuwa nacho wala tusingewaza lolote kwa kuwa tusingekuwa na la kuwaza. Lakini kutokuwa na chochote kwa kuwa kilichokuwepo kimeondolewa hiyo ingeleta ulinganifu wa hali ya sasa na zamani. Nakumbuka nilivyokuwa hodari wa kuendesha baiskeli lakini nilipoanza kuendesha pikipiki sikuweza kuvumilia "kusimamia" baiskeli tena kwani kila nilipofika mlimani na kuanza kutoka jasho nikakumbuka kuwa "ningekuwa na pikipiki ningebadili gia tu"
  Kuna msemo usemao "not doing anything on purpose is not the same as having nothing to do". Ndilo ninalozungumzia hapa
  Kwa ujumla maisha yetu yangekuwa mazuri saaana bila kuwa na chochote tunachoamini kinatufanya tuwe na urahisi wa maisha sasa.
  Si waona kuwa "zamani" watu hawakuwa wakisahau sherehe za kuzaliwa na kumbukumbu mbalimbali za ndugu na marafiki zao, lakini sasa hivi wanaweza kusahau na ukiwauliza.... watasema "alarm yangu ama simu yangu ama reminder yangu haikunikumbusha"
  NAAMINI TUNGEKUWA VEMA TUUU BILA CHOCHOTE NA PENGINE KUTOKUWA NA CHOCHOTE NDIO CHOCHOTE AMBACHO TUNGEKUWA NACHO

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU