NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, February 12, 2010

FIKRA YA IJUMAA: ATI, MSOMI NI NANI???

 • Hivi karibuni maoni mafupi ya Profesa Mbele kuhusu uzembe wa Watanzania, na uraia wa nchi mbili yalitundikwa katika blogu ya Issa Michuzi. Maoni hayo yalichangamsha watu sana na kama ilivyo kawaida, hoja za msingi ziliachwa na Profesa Mbele akaanza kuandamwa binafsi tena kwa matusi, kejeli na dhihaka (Nilishaligusia jambo hili hapa). Baada ya kuyasoma maoni hayo ya wachangiaji 76, nilianza kujiuliza maana hasa ya msomi. Ati jamani msomi ni nani? Ni lazima kuwa na shahada kuwa msomi? Vipi kuhusu babu jirani yetu kule kijijini (mganga wa kienyeji) anayefahamu karibu kila mti na matumizi yake tena bila kutumia daftari kuwekea kumbukumbu? Je, yeye ni msomi? Wewe ni msomi? Kuna faida ya kuwa msomi?
 • Hapa chini ni maoni wakilishi ya mitazamo tofauti ya wadau mbalimbali kutoka kwa Michuzi kuhusu dhana hii ya "usomi"
**************************
(1). Tarehe Tue Feb 09, 07:14:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous
 • Prof, Kuhn-Tucker conditions unazijua wewe?? super and submodularity je?? Je, vipi kuhusu maximum principle na calculas of variations (CV). Niambie unawezaje kujua iwapo a twice differentaible function ni concave au ni convex!! Baada ya hapo naomba u-state transversality condition ya Infinite Horizons model!! Ukimaliza hapo nieleze matumizi na umuhimu wa ARCH and GARCH models especially as applied to high frequency financial data, kabla ya kumalizia na maelezo kuhusu procedures zilivyo katika ku-conduct augument dickey fuller test (ADF) na short comings zake. Ahsante
 • Kidokezo changu: Kwa huyu mdau, huwezi kuwa "msomi" na kuweza kuanzisha wala kushiriki mjadala kama hukusoma kozi za juu za Uchumi na hatimaye kuweza kujibu maswali anayoyauliza hapa. Sina uhakika ni watu wangapi wanaweza kuyajibu maswali haya na hivyo kuonekana "wasomi". Je, tuupime usomi wa mtu kwa kuangalia uwezo wake wa kujibu maswali tata katika taaluma yake aliyosomea? Huyu mdau akiulizwa maswali kutoka katika taaluma zingine ataweza kuyajibu? Au pengine "Economics" ni taaluma bora kuliko zingine zote?
(2). Tarehe Tue Feb 09, 12:12:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous Fundi_mangungo
 • Huyu ni Professor wa kiswahili, I wonder anajifanya anaijuwa siasa na uchumi! Ni miongoni mwa wale wanaodhani kujipendekeza sana kwa Kikwete basi huenda wakapata hata ubunge wa kuteuliwa!!! Nna mashaka na u professor wake! Na daima ntaendelea kuwa hivyo! Uwezo wake wa kufikiri na kujenga hoja hauna tofauti na Baba yangu aliyeshia darasa la nne la mkoloni! Of coz sikutegemea kusikia mchango wa maana kuhusu uchumi kutoka kwa Professor wa Mofimu, virai, viima na viarifu (kiswahili), lakini nilitegemea angalau anyamaze au afunguwe blog afundishe watanzania Kiswahili! Unapopiga kelele watanzania wanapiga soga wakati huna statistical data na wewe kama Professor si aibu hiyo, una tofauti gani na hao unaowalaumu (wapiga soga)...uliozungumza ni mazungumzo ya maandazi tu! Tanzania ina hasara sana kama ina Professors wa aina hii! Na kama huu ndo u professor, mungu mie usinijaalie kamwe kuwa professor!
 • Kidokezo changu: Fundi Mangungo haamini kama mtu aliyesoma lugha anaweza kuanzisha mjadala wala kutoa mchango wa kitaalamu na wa kina katika mada zingine nje ya mofimu, virai, viima na viarifu! Vipi kuhusu mtu aliyesoma Jiografia, Udaktari, Fizikia, Historia, Sayansi ya Siasa au Kemia? Anaweza kutoa mchango wowote wa maana katika mijadala nje ya uwanja wake wa kitaaluma au pengine upungufu huu ni kwa "vilaza", "ngwini" na "mbumbumbu" waliosoma lugha tu? Tazama pia maoni kama haya ya Fundi Mangungo hapa.
(3). Tarehe Tue Feb 09, 12:43:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous MADELA WA-MADILU
 • Professor Mbele, Heshima mbele mkuu mwenzangu. Kama una nia ya kutumwagia matusi sisi akina MADELA WA- MADILU njoo pale kwenye jamvi. Wote tuko hapa Marekani tunaganga njaa, shule tumepiga kisawasawa lakini si wote shule zetu zinafanana na kufundisha kiswahili. Hesabu za majoka (Calculus) na Ngeli wapi na wapi???

 • Kidokezo changu: Pengine kusoma hesabu za majoka (calculus) ni bora kuliko kusoma ngeli; na kufundisha hisabati ni bora kuliko Kiswahili. Pengine pia ni kweli kwamba mtu aliyesoma hesabu za majoka ni msomi kuliko aliyesoma ngeli. Na hesabu ni bora kuliko lugha!!!
*********************
Kulikuwa pia na maoni makini ambayo yalizingatia hoja. Mfano ni maoni ya Mdau Mkweli (Tue Feb 09, 01:49:00 AM) na ya mdau wa Tue Feb 09, 12:15:00 AM.
 • Turudi tena kwenye fikra yetu ya leo: Kwako wewe msomi ni nani? Unaweza pia kusoma hadithi hii fupi kuhusu dhana hii ya usomi.

7 comments:

 1. Matondo,
  Swali lako ni gumu.Nani msomi?Hata baada ya kusoma maoni ya "wananchi" na mtizamo wako,bado nimebakia na maswali kichwani.Hivi kweli nani ni msomi?Ngoja niendelee kutafakari.

  ReplyDelete
 2. Hili swali limenikumbusha kisa kimoja kati yangu na mwalimu wangu wa Public Speaking (Speech). Ulikuwa ni mgongano wa mawazo (debate) ambayo almanusra inisababishe kufeli darasa.
  Nilienda kufanya Informative Speech kuhusu Tanzania. Na katika sehemu yake nikamnukuu Baba yangu (lakini si katika kitabu). Mwalimu wangu akasema niliyemnukuu si "muelimika" kwa kuwa sijanukuu kitabu ama maandishi yake yoyo ama speech aliyotoa mahala. Kwa hiyo hafai kunukuliwa kama mtaalamu wa jambo ninalozungumzia.
  Hilo lilinikera kwani niliona ni MTAZAMO M'BAYA JUU YA MSOMI.
  Nilipomuuliza kama ni sahihi kwa mimi kumnukuu Commando ama Navy Seals kuhusu maisha yao porini wanapokuwa wakisaka huo u-Commando akasema wale ni experts na ni sahihi kuwanukuu. Na akasema ile ni kazi wanayosomea namna ya kukabili wanyama na wana-graduate katika hilo. Kwa hiyo hao ni WASOMI. Nikamuuliza "Vipi kuhusu wamasai ambao maisha yao miaka nenda rudi ni sawa na hao "wasomi" wako ambao wanafanya hivyo kwa miezi kadhaa na kisha mnarejea kuwapokea kwa shangwe, maua na ongezeko la mshahara?" AKAKAA KIMYA.
  Nikamuuliza kama ni sahihi kumnukuu NAHODHA wa meli nitakapotaka kuzungumzia suala la kutumia pepo za baharini katika kusafiri, akasema ni sahihi kwani hao ni WASOMI. Kisha nikamuuliza kuhusu wazee wetu waliokuwa wakisafirisha karafuu bila kujua ramani, pande za dunia wala kutumia injini na bado wanatumia hizo pepo na kufika watakako kwa muda watakao, JE NI WASOMI NA NI SAHIHI KUWANUKUU?
  Tukaendelea kuhusu Babu zetu wanaoweza kutabiri mwaka kimavuno japo hawana Rada kama hawa ma-weather experts. Nikasema ni nani msomi? Ni yupi aliye expert? Huyu anayejua kuwa anakwenda kuishi porini kwa miezi sita ili apande cheo ama mmasai anayeishi maisha yote huko? Yupo MTAALAMU kati ya huyu anayetumia kompyuta na kompasi kujua aendako na yule anayetumia pepo za kusi na kaskazi kwenda waendako? Ama Bibi yangu anayeangalia mateso ya mama mjamzito na mabadiliko yake na kilichopo tumboni akatabiri jinsia ya mtoto ama hawa walio na sonogram ambao wameandika vitabu kadhaa?
  Mwisho nikamwambia anitafsirie MSOMI NA MTAALAMU na kwa hakika alishindwa kisha akanirejeshea pointi zoote alizokuwa amenipunguza.
  Mpaka leo sijajua MSOMI NI NANI
  Na nakumbuka Da Mdogo Koero aliwahi kuuliza hili likaleta mchanyato mreeeefu na Kaka Evarist Chahali akaeleza kwa kina juu ya mtazamo wake katika hili. Pia Kaka Bwaya alijimwayamwaya vya kutosha. Wengine mlikuwa hamjaanza kutembelea tuvijiwe twetu, hebu jikumbushe hapa http://koeromkundi.blogspot.com/2009/01/hivi-msomi-hasa-ni-nani.html

  ReplyDelete
 3. Dr. Shukrani sana za dhati kwa kuleta swala hili tata na ambalo binafsi liMEkekuwa likinitatiza sana. Kwani katika miaka yangu 33 ya kuishi hapa Duniani, nemeona mambo mengi ambayo yananifanya nishindwe kukupa jibu rahisi la hili swali lako.
  Kama alivyosema mzee wa changamoto hapo juu, ni vigumu sana kuamua kwamba ni yupi msomi; je msomi ni yule tu ambaye amefikia ngazi ya juu za FORMAL education, hali ya kwamba hiyo elimu yake haina manufaa kwake na kwa jamii kwa ujumla, au wasomi ni wale mababu zetu mbao japo hawakupitia kwenye hiyo Formal education, lakini INFORMAL education walioyokuwa nayo iliwawezesha kuyamudu mazingira yao?
  Kwa mfano, kule nyumbani Tanzania, miaka ya hivi karibuni nimeeshuhudia the "so called WASOMI", tena waliosomeshwa na pesa za WAKULIMA,
  wakapelekwa kwenye ELITE school huko marekani, lakini cha ajabu, maamuzi waliyoochukua kama viongozi wa nchi, yameleta maafa badala ya neema. Viongozi hao ambao nadiriki kuwataja (Bejamin Mkapa- Columbia University na Andrew Chenge- Havard University) ambao kwa mtazamo wa kawaida, wanaitwa wasomi, lakini ki ukweli, maamuzi waliyofanya, sidhani kama hata BABU yangu ambae aliishia darasa la nne la mkoloni, angeweza kuyafanya katika kuisulubu nchi yetu.
  Hapa ndipo utata wa hili swali lako unapokuja, je ni nani haswa anayepaswa kuitwa msomi? Dr. Matondo, kwangu mimi nadhani msomi ni yule ambae ameelimika kiakili, kiroho na kivitendo.
  Kwa maana nyingine, Elimu lazima ikukumboe, au ikutoe gizani kuelekea kwenye NURU, hata kama ni Elimu ya msingi.
  Sidhani kama kubobea kwenye mambo ya Uchumi, kompyuta, engineering, au science ndio kigezo kikubwa cha usomi. Sula nui kwamba, ni jinsi gani unatumia elimu yako ili kurahisisha maisha ya wanaadamu. Wabunifu wa HULOCAUST kule Ujerumani walikuwa ni wasomi, lakini matokeo yake tunayasoma mpaka leo.
  Hivyo basi, kumaliza tu madarasa bila ya kukombolewa na hiyo ELIMU ni kazi bure; hayo tumeyaona kwa MA- ALUMNI wetu wa HAVARD NA COLUMBIA UNIVERSITY.

  ReplyDelete
 4. Namhalah Matondo! Sina hakika na uwezo wa kujibu mada hii lakini natumai kuwa Msee ya Changa-moto na Anony hapo juu wamegusia jambo muhimu ktk maisha ya binadamu!

  Ninavojua ni kuwa MSOMI si mtu alobukua kama tunavodhani bali mtu mwenye KUPAMBANUA kati ya JEMA na BAYA! Na kwa bahati mbaya WASOMI wengi hawawezi kupambanua jema na baya :-(

  Kama Anony alivogusia hapo juu hao jamaa wasomi wametusaliti na ndo utashangaa kusikia hayo maoni ya ovyo ovyo ya wasomi katika hizo posti ulizozirejea hapo juu :-(

  Si ajabu kumsikia waziri mkuu mstaafu akisema kuwa 'kwa muda wote wa miaka 10 alokuwa waziri mkuu alikuwa hajui kwa nini Tanzania ni maskini' mpaka alipokwenda kufundwa huko Havard.

  Na si ajabu kumsikia rais akihojiwa na waandishi wa habari wa nje kwa nini tanzania ni maskini ilihali ina rasilimali lukuki na jibu linalotoka kwa mkuu wa nchi MSOMI ni kuwa HAJUI kwa nini tuko maskini :-(

  Kwa hiyo utaona wasomi wetu wameshindwa kupambanua baya na jema. Ama kwa hakika unaweza kuwa na mashahada 10 lakini ukawa bado hujaelimika. Naweza kulifananisha hilo na 'kutotumia common sense' :-(

  wazee wetu kijijini wanatumia common sense japo hawajawahi kuwa katika darasa la chuo kikuu. Wana uwezo wa kuhimili mikiki ya maisha magumu ambayo MSOMI hawezi kuyahimili.

  Je kuwa na digrii ndo kigezo cha usomi? na kama ni kigezo basi twafwa :-(

  ReplyDelete
 5. Nanukuu "...Prof, Kuhn-Tucker conditions unazijua wewe?? super and submodularity je?? Je, vipi kuhusu maximum principle na calculas of variations (CV). Niambie unawezaje kujua iwapo a twice differentaible function ni concave au ni convex!! Baada ya hapo naomba u-state transversality condition ya Infinite Horizons model!! Ukimaliza hapo nieleze matumizi na umuhimu wa ARCH and GARCH models especially as applied to high frequency financial data, kabla ya kumalizia na maelezo kuhusu procedures zilivyo katika ku-conduct augument dickey fuller test (ADF) na short comings zake"

  Kama wachumi wetu ndio hawa basi hatutakaa tuendelee. Wanachowaza ni concave na convex graphs bila kuangalia hasa maisha ya mwananchi wa kawaida. Hawa ndio wanaotamba kwamba GDP yetu mwaka huu imekua kwa asilimia 6 wakati maisha ya wananchi yanazidi kudidimia. Who cares if your stupid graph is concave or convex if the conditions of the people are deteriorating? Show me improvements katika maisha ya watu dammit. And then we can talk about concave and convex graphs. Please, Mungu Ibariki Tanzania!!!

  ReplyDelete
 6. Hiyo ndio kasheshe ya elimu yetu suku hizi, ni kukreumua formula ili upasi mitihani tu, lakini elimu yenyewe inakuwa haina manufaa yoyote kwa jamii. Dr. MATONDO, ELIMU kwa jinsi ninavyoelewa mimi, inatakiwa iwe kama TOCHI, na ambalo linalomuwezesha mwenyenalo (the possessor) kutoka GIZANI na kwenda kenye MWANGA au (to control his/ her enviroments); ni hapo tu ndipo unapoweza kusema kwamba ELIMU imefanya kazi yake. Lakini hayo mambo ya kukariri furmula za Uchumi au Physics ili kuonyesha watu kwamba umesoma, au ili kupasi tu mitihani, kamwe hazitatusaidia kuendeleza nchi yetu.
  Ni mfumo huohuo wa sasa wa elimu wa Tanzania, ambao lengo lake kubwa ni kupasi mitihani, na sio kutaayarisha UBONGO wa wanafunzi kuwa wabunifu, ndio maana sikushangazwa na comment ya watu kama Fundi_Mangungu, ambao hawawezi kutokubaliana na makala za watanzania wengine bila kudhalilisha taaluma zao.
  Leo hii wasomi wote wanaomaliza masomo yao kwenye vyuo vyetu, wanakimbilia D’salaam kwenda kutafuta ajira za maofisini na kuvutiwa na tamaa ya RUSHWA iliyopo mjini. Ni wachache sana ambao wanafikiria kwenda vijijini au nje ya miji mikuu, na mbako ndipo asilimia 80 ya watanzania wanapoishi ili kwenda kuleta madabiliko ya maana. May be I am wrong, lakini najaribu kufikiria kama wapo wanafunzi wa CIVIL ENGINEERING kutoka pale MLIMANI au chuo chochote kikubwa Tanzania, ambao wanamoyo wa kujituma wa kwenda kwenye zile sehemu ambazo zimekumbwa na mafuriko hivi karibuni (mfano kule Morogoro), na kujaribu kuwatengenezea au kubuni japo Madaraja ya DHARURA ya miti na ambayo yatawawezesha waathirika kuendelea na maisha yao ya kawaida, badala ya kuwa wafungwa wa Mother Nature. Lakini haya yote hayawezi kuja kiurahisi, yatakuja tu iwapo tutabadilisha mfumo wa elimu yetu, kuteka kwenye kupasi mitihani tuu, na kuelekea kwenye maaarifa na Uvumbuzi. Hakuna mwalimu mzuri Kwa binadamu kama MOTHER NATURE; unapoweza kukabiliana na dharuba zake, bila kujali kama unadegree au la, huo ndio usomi. Imagine maengineer wote walio graduate pale mlimani tangu 196? wakati hiyo faculty ilipofunguliwa, wengi wao wanachofanya sasa hivi ni kukarabati mitambo ya either WACHINA, WAINGEREZA, NA WAJERUMANI popote pale walipoajiriwa, hawakutayarishwa kuvumbua hata filimbi ya MGAMBO.
  Fikiria tena wale wasomi wetu ambao walitumwa na nchi kwenda kujadili na kusign deals kama ile ya UMEME ya mechmar Corp. ya Malyasia, Radar, Dowans, Kiwira, na RICHMOND, pamoja na elimu walizonazo, je wanastahili kuitwa wasomi? Na kama jibu ni ndio, kwa vigezo gani?
  David Orr wrote in his article “What Education Is For”
  “We cannot say that we know something until we understand the effects of this knowledge on real people and their communities” David Orr 1991.
  NB: Labda mfano mzuri ni reli ya TAZARA; hii reli ilikabidhiwa kwa serikali za Tanzania na Zambia in 1975, laini cha ajabu ni kwamba, mpaka leo hii matatizo yoyote ya kiufundi yanafanywa na wataalam kutoka CHINA. Nchi hizi mbili zimeshindwa kuchukua hatua zozote kuhakikisha kwamba WAZALENDO ndio wanachukua jukumu la kukarabati kitega uchumi hicho muhimu kwa nchi hizi mbili ZAO. Miaka 35 tangu reli ikabidhiwe, na bado mafundi wanatoka CHINA. Just think about it!!!

  ReplyDelete
 7. Inavyoonekana Fundi Mangungo ana chuki binafsi na waalimu wa lugha. Nadhani alipata F katika Kiswahili na Kiingereza form IV na bado anaamini kuwa alionewa. Mtu ye yote mwenye akili timamu hawezi kamwe kuoanisha taaluma ya mtu na kufanya generalizations ambazo haziko founded. Pengine angetoa data pia. Historia inaonyesha kwamba lugha hasa ndiyo ilikuwa kichocheo cha kila kitu na karibu wanafalsafa wote na wanasayansi wote wa mwanzo walishughulika pia na lugha. Lugha ndiyo mlango wa yote na watu wa lugha ndiyo hasa mabingwa wa kujenga hoja na kuzitetea. Kuchora graph ya concave au convex hakumpi mtu uwezo wa kujenga hoja na wanasayansi wanajulikana kwa ubutu wa mawazo nje ya uwanja wao wa sayansi. Tunapodharauliana na kutukanana namna hii INASHANGAZA. I AM KIND OF PUZZLED lakini pia we are human beings na kimsingi we don't like each other. Sasa actually chuki inazidi sana among Tanzanians and personally I don't know where we are going. God help us!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU