NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, February 19, 2010

FIKRA YA IJUMAA: VALENTINE DAY, MASHINDANO YA UREMBO, NOECLEXIS NA DHANA YA UZURI.


 • Jumapili iliyopita ilikuwa ni "Valentine Day". Kwetu sisi Afrika nadhani siku hii bado ina ugeni fulani. Kwa mfano, wakati nikisoma pale mlimani miaka michache tu iliyopita,, sikumbuki kuona watu wakihangaika kusherehekea hii Valentine Day. Mambo yamebadilika kwa kasi mno na siku hii sasa ni muhimu kwa wapendanao kusherehekea kwa kwenda pwani, kwenye kumbi za starehe na kwingineko. Blogu kadhaa ziliwaonya na kuwakumbusha washerehekeaji wa sikukuu hii juu ya hatari ya kuambukizana gonjwa la UKIMWI.
 • Siku hii ya wapendanao na mashindano ya urembo tunayoyashuhudia kila leo (vyote ni matokeo ya utandawazi) vimenikumbusha swali gumu ambalo limewasumbua wanafalsafa tangu enzi na enzi: Uzuri ni nini? Hili ni swali linalohusu kila kitu hapa duniani lakini leo nitatumia mifano ya washiriki wa mashindano ya urembo yaani mabinti.
 • Ni kweli kuna wazuri/warembo au pengine uzuri/urembo umo katika fikra za mtazamaji tu? Inakuwaje leo tunalazimishana kuwa na mrembo mmoja tu tena mwenye sifa zile zile za Kimagharibi- tineja, mkondefu, mrefu, mwenye miguu mchongoko na tumbo tambarare, mwenye madaha, nyanya msumari kifuani na ikiwezekana "aliyepigwa pasi"? Hebu chunguza picha hizi kwa makini halafu ufikiri tena dhana hii ya uzuri/urembo:
(1) Tunalazimishana kuamini kwamba eti mrembo ni lazima awe hivi:

(2) Huu ni uwongo kwa sababu katika jamii zingine za Kiafrika mrembo alitakiwa/anatakiwa awe hivi:

free image hostfree image host free image host

(3) Na katika jamii zingine mrembo alitakiwa/anatakiwa apambike hivi:

free image hostfree image hostfree image hostfree image host

(4) Kwa wengine, mrembo ni lazima awe amenona kama hivi:

free image hostimagebam.com

(5) Au awe na umbo namba 8 kama hili:

free image host

(6) Au mwili na sura hii ya Kihabeshi

free image host

(7) Wengine huwa hawajali umbo ali mradi kuwe na "kitu" wakipendacho!

free image hostfree image hostfree image host

(8) NOECLEXIS - Mwanamke tabia ati! Msikilize Dudubaya hapa chini.(9) Swali: mbona tunalazimishana kwamba eti mrembo ni lazima awe hivi?

 • Na kama kila mtu ana dhana yake ya uzuri kama tulivyoona hapo juu, inawezekanaje tuwe na mzuri mmoja tu anayewakilisha dhana zote hizi? Ati, uzuri hasa ni nini? Wikiendi njema mnaposhuhudia "uzuri" uliotamalaki katika kila kitu hapa duniani!

4 comments:

 1. Nafikiri LUGHA zina mapungufu.

  Na nafikiri vilevile kuna udhaifu mwingine uletwao na NENO UZURI kutokuwa na uhusiano na KITU kwa kuwa ni neno tu.

  Na kiitwacho uzuri kilihitaji maneno mengi mengine katika kukinyambulisha.

  Pia nafikiri, Neno UZURI lina mapungufu na haliwezi kuongelea swala ndio maana KILA mtu anauwezo wa kuwa na MZURI wake.


  Lakini PIA BINADAMU anafundishika, na anafundishika mpaka ni kitu gani ni KIZURI.:-(  Ngojea nijaribu kuelezea kwa mfano tofauti;


  Nilishangaa siku moja rafiki yangu Msauzi alivyokuwa ananitajia majina tofauti kibao ya neno moja ambalo kwa kiswahili lingeitwa tu ``KIJANI´´ . Jamaa kwao wana jina tofauti mpaka wa ukijani huohuo kama unapigwa na jua au uko kivulini na alivyofananisha na Kiingereza akakuta wakiitacho GREEN kikwao kina majina kama ishirini tofauti.


  Ndipo nilipostukia hata kwa KISWAHILI tuzungumziapo rangi KIJANI sanasana tutaongezea Kijani kibichi n.k lakini ukifikiria utakuta KIJANI uionayo unaweza kukosa jinsi ya kuielezea kama huna kielelezo cha picha.
  Nachojaribu kusema ni kwamba.

  Labda mashindano haya sio ya uzuri kwa kuwa neno lenyewe UZURI linautata kutokana na mhusika.

  Pia mimi naamini ni kwa sababu tu BINADAMU anafundishika na kwa hiyo sishangai kuona BINADAMU waliokuwa wanaoa wake wengi muda sio mrefu wanamshangaa Rais ZUMA sasa hivi kwa kuongeza jiko. Wapenda matako makubwa niwajuao haikawii kuwakuta ladha imebadilika ghafla kwa kila siku kuelezewa tako zuri ni dogo lenye msaada hasa katika baadhi ya staili za uzinzi kama ie ya chuma mboga.  Pia, kwa sababu hiyo hiyo sitashangaa HALOWINI ikiwa bonge la sherehe muda si mrefu VIJIJINI Tanzania.:-(

  Binadamu tunafundishika na NI HILO tu .

  Na labda ndio maana chai ya sukari ni tamu pia kwa adaiye BIA tamu.

  Kwa kuwa twaweza kujiuliza UTAMU ni ni kama NGONO , Pilipili, na Asali vyote vyadaiwa vitamu.


  Samahani kwa kuandika kwa haraka haraka kitu ambacho kinaweza kukwaruza mtiririko wa hoja.:-(

  ReplyDelete
 2. Niungane na Kaka Kitururu katika "Point of view" (maana najua wapo watakaosoma "tone" ya maandishi yake). Lakini KIZURI NI KIPI? KITAMU JE?
  Nianze na mfano wa kitamu. Wapo wanaosema wanakula na kupenda ugali kwa kuwa ni mtamu. Hivi ni kweli? Na zaidi pale wanapoonekana wakila UGALI kwa PARACHICHI. Na bado wanasema ni vitamu. Lakini kwangu mimi si ugali wala parachichi vyenye ladha.
  Na UZURI nao ni yale yale. HAUTAFSIRI "KWA NIABA YA YEYOTE"
  Uzuri unakuwa miongoni mwa mtu na kwa manufaa ya mtu.
  Hakuna mwanamke mzuri duniani kama MKE WANGU. ESTHER a.k.a Mama Paulina ni mwanamke mzuri kuliko yeyote ulimwenguni (kwa mujibu wa Mubelwa Bandio). Lakini sababu ni kuwa hakuna anayewezwa katika mawazo yangu kwa namna alivyo yeye. Ni kwa kuwa uzuri kwangu unatafsiriwa na uwepo wake na nawaza mazuri kwa kuwa ananisaidia kuyawaza.

  Tatizo kubwa linalojitokeza Tanzania yetu ni kuwa TUNATAFSIRIWA NASI TUNAPOKEA. HATUCHUJI. TUNAONA KILA KIJACHO CHAFAA.
  Kama alivyosema Kaka Mkodo, nami sitashangaa nikiona HALOWEEN ni sherehe kubwa vijijini. Ni kwa kuwa TUNAZIDI KUJIPOTEZA KATIKA HARAKATI ZA KUJITAFUTA.
  Leo hii dada mwenye "big skin" anajikondesha ili "awe mzuri". Matokeo yake wanaishia kuugua maradhi ya ajabu wakisaka "uzuri"
  Labda picha namba 4 na 7 ndio "warembo" waliobarikiwa miili.
  Hivi tunapowazungumzia WAREMBO tunahusisha TABIA zao? Ama ndio mambo ya miss Tanzania kuelekezwa kunyea debe kwa makosa ya "asiyefunzwa na mamaye ...."?

  ReplyDelete
 3. Duuhh Kaka yangu Matondo umenijibu swali langu kwa kupita hapa, yaani nimepata shule sana,Ubarikiwe sana kaka wa mimi kwa njia yako hii,Kweli jibu ni tata na Penye wengi Pana mengi.Pamoja kaka.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU