NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, February 24, 2010

CHANGAMOTO ZA WATU WEUSI HAPA NINAPOISHI (NA POPOTE KWINGINEKO)

Ninaishi katika mji wa Gainesville, kata/tarafa/wilaya? (county) ya Alachua. Kidemografia, asilimia 22 ya wakazi wa Alachua ni weusi. Ripoti inayoainisha masuala ya kiafya ya wakazi weusi wa Alachua iliyotolewa wiki jana inashangaza na hata kusikitisha. Mbali na mambo mengine, ripoti hiyo inaonyesha kwamba:
 1. Vifo vinavyotokana na kansa viko juu kwa asilimia 24 kwa watu weusi ikilinganishwa na wazungu.

 2. Katika mwaka 2008, vifo vilivyotokana na kisukari (diabetes) vilikuwa juu kwa asilimia 211 kwa weusi ikilinganishwa na wazungu.

 3. Katika mwaka 2008, ni asilimia 60.7 tu ya akina mama weusi waliweza kupata huduma za ujauzito (prenatal care) ikilinganishwa na asilimia 78.7 kwa akinamama wa kizungu na asilimia 76.6 kwa akinamama wa kilatino.
Nilipoziona data hizi nilisikitika halafu nikamkumbuka AIKA. Popote pale tulipo, watu weusi tunaandamwa na changamoto ya kujikomboa na kuna sababu nyingi zinazosababisha hali hii - nyingine za kihistoria na kijamii - na nyingine za kujitakia. Msome na kumsikiliza Bill Cosby hapa kuhusu changamoto zinazowakabili Wamarekani weusi na mchango wao wenyewe katika kuziendeleza changamoto hizi.

Kwa sisi Afrika, mbali na mambo mengine, ukosefu wa viongozi bora na wenye uchungu na watu wao ni sababu mojawapo kuu inayolifanya bara letu tajiri liendelee kusikinika. Wamarekani weusi bado wanalaumu utumwa. Na sisi tutaendelea kulaumu ukoloni mpaka lini?

7 comments:

 1. Duh! 'wanalaumu utumwa na siye twalaumu ukoloni'

  kazi kweli kweli. Ni lini tutajilaumu wenyewe na kuchukua hatua?

  Matonndo: hatua itachukuliwa na mimi na wewe individually. Be the change you want to see!

  ReplyDelete
 2. Bill Cosby has a point. The blacks in the USA don't want to speak standard English, don't pay attention to school and more importantly - there is no parenting and the kids are not raised with the proper foundations. You cannot compare a black and a white kid even in the class even if both are athletes. weusi simply don't have the basics. Ni kweli, they can no lnger keep on blaming wazungu. Part of ze problem ni wenyewe - drugs, violence, umalaya, uvivu etc. Niaje? Haya si makosa eti ya wazungu. Fist time to hear this speech by Cosby. What was the reaction from the blacks? Did theu listen?

  ReplyDelete
 3. Ni kweli tunachangamoto nyingi za kupambana nazo, kama huko ughaibuni hali iko hivyo huku kwetu basi ni balaa maana yake huku hata hizo huduma kuzipata ni tabu sana hasa vijijini ambako malaria inapimwa kwa macho, na muuguzi anaitwa dokta

  ReplyDelete
 4. Viongozi wa Kiafrica Wapo madarakani kwa ajili ya manufaa yao Binafsi, na si kwa manufaa ya Taifa...Tutaishia kuomba misaada kila kukicha tukisingizia kuwa they have to clear up the Mess they did,Jamani hivi nchi kama Tanzania ni nchi ya kuomba misaada? Tanzania ni nchi ambayo imebarikiwa kuwa na kila kitu ambacho taifa lolote ulimwenguni lingetamani kuwa nacho,tumebarikiwa mito,milima,maziwa,mabonde,ardhi yenye rutuba,mbuga za wanyama,madini na nk.What a shame! ni miaka 45 sasa toka tumekuwa huru,nini kimefanyika zaidi ya rushwa na ufisadi kila leo...Alafu bado tunasingizia ukoloni.
  Anyway Asante kwa shule ya bure unayotupa kaka.

  ReplyDelete
 5. Hii habari ina changamoto nyingi kwa sisi weusi popote pale duniani,nimefuatilia pia umasikini wa kule Haiti hadi sasa sijapata jibu sahihi,ila nionavyo mimi tatizo ni uongozi na zaidi hawajali maslahi ya umma sana sana ni ubinafsi umezidi.Ila nadhani kuna mengi ya kujiuliza sisi weusi ili siku moja tupate jibu la pamoja la kuleta mabadiliko popote alipo mtu mweusi.

  ReplyDelete
 6. dk matondo ni vema umelileta hili la viongozi wasio bora katika afrika. nakumbuka niliwahi kukuuliza kwa changamoto huko kwenye post zako za zamani kuwa inakuwa vipi mtu kama bob mugabe naye tumuite kiongozi bora katika afrika. wakina mugabe na museveni ndio wanairudisha afrika nyuma. wengine wapo ingawaje hapa sitawasema kwa kuwa naogopa mkong'oto.

  ReplyDelete
 7. mimi sioni tatizo, sote ni binadamu sema tu ile ripot imeamua kubagua wakazi wake kwa kuangalia rangi za ngozi zao. ni sawa na wanaoua albino kwa sababu tu ya tofauti ya ngozi.

  je, pamoja na changamoto zoote hizo, unadhani weusi kwa kuwaangalia kwa ngozi hawana zuri hata moja au jema?? mbona Matondo ni mwalimu kule?? ikiwa na maana kuwa lazima mweusi (matondo) akafundishe yale ayafundishavyo wengineo ni vilaza, kwa hiyo tukiamua kufanya utafiti kwa mtizamo chanya, kuna mazuri ya weusi pia labda kuliko hata wadhungu japo Aika anatamani uume wa kudhungu kumbe nao unatoa manii yale yale

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU