NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, February 11, 2010

HATIMAYE IMEKUWA: NG'WANAMBITI AFUNGUA KIJIWE!!!

 • Ni huyo pichani. Jina lake ni Chacha o'Wambura lakini wengi wetu tunamfahamu kama Ng'wanambiti! Anapenda sana michembe na Matobolwa na ni mfuasi makini wa michezo ya "manyalali" kule Usukumani ambako inasemekana ndiko alikojipatia hilo jina lake mashuhuri la kazi yaani "Ng'wanambiti - mtoto wa fisi!"
 • Yeye ni mchangiaji na mtoa maoni makini sana katika blogu zetu. Maoni yake mengi, hata yale yaliyotolewa kwa mzahamzaha tu na utani, ni makini pevu na yenye kufikirisha, maoni yanayoonyesha ukomavu wake wa kifikra, kifalsafa na kimtazamo.
 • Karibu sana Ng'wanambiti katika ulimwengu huu mzuri wa kublogu. Karibu katika uelimishaji, uhabarishaji, uburudishaji na upiganiaji wa jamii.

 • Kijiwe chake kipya kabisa kinapatikana HAPA. Hebu na tumkaribishe huyu mpiganaji wa Kikurya!

3 comments:

 1. Na kweli hatimaye afungua kijiwe chake. Karibu sana Kaka Chacha!!!

  ReplyDelete
 2. Habari nzuri hii, tumezoea kumsoma kupitia vibaraza vya watu.
  Karibu sana Chacha, lakini usisahau vijiwe ulivyovizoea pia

  ReplyDelete
 3. Aksanti sana Dkt. Masangu kwa kunikaribisha rasmi. Sina cha kuahidi saana ila natarajia kupata ushirikiano toka kwenyu nyote.

  Chib, unakumbuka ile methali ya 'USIACHE MBACHAOOOOO....'

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU