NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, February 18, 2010

J.K.T HALIKUWA MCHEZO ATI!!!

 • Hapa ni Makutupora J.K.T Dodoma Operesheni Miaka 30 ya Uhuru. Naikumbuka siku hii kwa sababu ng'ombe wote hao walipotea kwa zaidi ya masaa sita. Kumbe walikuwa wametupiga chenga mimi na hao wachungaji wenzangu na kwenda kuparamia shamba la mizabibu tena ile myeupe. Ni stori ndefu hii, we acha tu. Maisha!

5 comments:

 1. Zamani ilikuwa safi, je hiyo stori ndefu hutaki kutusimulia yote nasi tufaidi? ...LOL

  ReplyDelete
 2. Hahahahaaaaaaaaaaa.
  Sitaki kuhisi ambacho kingewatokea kama msingewapata mpaka wakati wanaostahili kuwa zizini.
  Si unajua J.K.T ilikuwa kama chemba ya kusubishana???
  Kweli taswira muhimu

  ReplyDelete
 3. Hapo mpaka ng'ombe wanapotea prof utakuwa ulienda kuchukua chai na mabinti wakaenda kuiba nyanya na vitunguu au wakarudi serengeti!!Umenikumbusha tukiwa zamu ya kwa Mbuzi tuliwapeleka Mzakwe halafu mmoja akajichanganya na vijiji vya Nzasa mbele ya Mzakwe!!Hadithi ilikuwa ndefu baada ya buti kutobolewa na mtunduru!!

  ReplyDelete
 4. Yasinta na anony - stori ndefu ni ndefu kweli. Huyo binti mwenye kofia, suruali na fimbo ilikuwa ndiyo mara yake ya kwanza kuchunga ng'ombe na walipopotea alishtuka sana. Babake ni daktari bingwa na tayari alipiga simu kufanya mipango atumiwe pesa ili tuweze kulipa gharama ya ng'ombe hao. Mimi sikuwa na wasiwasi kwani nilijua kwamba watapatikana tu. Nilishapoteza ng'ombe mara nyingi na ukubwa wa pori lile la Makutupora nilijua kwamba watakuwa wameenda sehemu. Yaani stori zilinoga na bila kujitambua ng'ombe haooo wakatokomea. Aliyetuokoa ni mshikaji mmoja ambaye alikuwa mwangalizi wa hilo shamba la mizabibu myeupe na alikuwa anajua kwamba sisi ndiyo tulikuwa wachungaji. Aliwaangalia ng'ombe hao vizuri na baadaye akatuma mtu kuja kututafuta jioni jioni...Isingekuwa yeye sijui ingekuwaje.

  Mzee wa Changamoto - ilikuwa ukipelekwa getini basi umekwisha. Huko unapigishwa kadebra kudadeki hata ukifleti maafande wanakumwagia maji ufufuke ili uendelee na mzigo. Na pia kulikuwa na kufungwa kabisa + kazi ngumu. Niliwahi kwenda getini mara moja kwa kosa la kuiba matikiti maji. Nilipiga push ups nyingi siku hiyo mpaka mwenyewe nikajishangaa. Yote kwa yote - nilipenda JKT ingawa sikupenda mambo waliyokuwa wakitendewa wasichana. Kama ningekuwa huko na JKT likaweko, basi mtoto wa kiume lazima angeenda lakini mabinti zangu kamwe wasingetia guu huko unless kama mambo yamebadilika! Kweli taswira ni muhimu!

  ReplyDelete
 5. Duh! mie nilijongo JKT nkaenda kwenye upadre....lol

  Kama ingekuwepo tena kwa mujibu wa sheria ningekwenda...lol

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU