NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, February 27, 2010

MATETEMEKO YA ARDHI JAPAN NA CHILE - HALAFU HAITI

 • Jana Japan ilikumbwa na tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa 7.0 katika kipimo cha Richter. Tetemeko hili lilikuwa na ukubwa sawa na lile lililoikumba Haiti na kusababisha vifo vya watu zaidi ya laki mbili na elfu hamsini pamoja na kuharibu kabisa mji mkuu wa nchi hiyo masikini. Kule Japan, tetemeko hili halikusababisha uharibifu mkubwa wa mali na maisha.
 • Leo, Chile imekumbwa na tetemeko kubwa kabisa lenye ukubwa wa 8.8 katika kipimo cha Richter. Wanasayansi wanasema kwamba tetemeko hili lilikuwa na nguvu mara 500 kuliko lile la Haiti. Habari zinazoendelea kupatikana kutoka Chile zinasema kwamba japo kuna uharibifu wa majengo na maisha, uharibifu huo hautafikia wala kukaribia ule wa Haiti.
 • Kinyume na Haiti, Japan na Chile zina uzoefu wa muda mrefu na matetemeko makubwa ya ardhi na teknolojia okozi na zuizi zinatumika katika ujenzi wa miundo mbinu yote.
 • Hii inaonyesha ni kwa jinsi gani umakinifu na maandalizi ya muda mrefu vinavyoweza kuokoa mali na maisha ya watu. Haiti na nchi zingine zinayo mengi ya kujifunza kutoka Chile.

2 comments:

 1. Profesa Masangu, nakubaliana na wewe kabisa. Katika kila jambo uzoefu unayo nafasi kubwa. Mbali na tetemeko la ardhi, mfano hapa Ulaya winter imesababisha maafa na kero katika maisha ya kawaida, hili limesibu hasa nchi zile ambazo hazina uzoefu na winter.

  ReplyDelete
 2. Wakati wa Hurricane Katrina kule USA Cuba ilijitolea kutoa technical assistance kabla hurrican haijahit inland lakini Americans kutokana na hate yao kwa Castro wakagoma. Results tunazijua. Dharau yao kwa Cuba iliwaponza. What they didn't know is that Cuba is in the hurricane corridor na ina uzoefu sana na majanga ya aina hii.

  Fikiria earthquake ya 8.8 Chile. This is one of the biggest earthquakes - 500 times that of Haiti. And yet no major destruction and loss of life. Very impressive!!!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU