NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, February 9, 2010

MUHULA HUU NAFUNDISHA KISUKUMA!!!

 • Mwaka jana niliombwa na Mkuu wa Idara ya Isimu hapa chuoni kwetu kufundisha darasa linaloitwa Structure of an African Language. Nilikubali, na baada ya kukaa chini na kufikiri sana niliamua kuwahangaisha Wamarekani kwa kuwafundisha Kisukuma.
 • Darasa hili lina wanafunzi saba na wote ni wanafunzi wa shahada za uzamifu (Ph.D). Wote walikuwa hawajapambana na lugha za Kibantu na Kisukuma kinawashangaza na kuwahangaisha kweli kwani kina miundo ambayo haielezeki kirahisi kwa kutumia nadharia za kisasa hasa kwa upande wa Fonolojia. Mofolojia na Sintaksia yake pia inavutia sana!
 • Kwa upande wangu najivunia sana kuifundisha lugha hii niipendayo katika kiwango hiki cha juu kabisa cha elimu. Wakati sisi tunazidharau na kuzibeza lugha hizi na kuziona kuwa hazina mbele wala nyuma, kwa wanaisimu zinaonekana kuwa ni migodi ya thamani sana na nadharia nyingi muhimu za Kiisimu zilizaliwa ili kuweza kuzichambua kwa kina lugha hizi ambazo sisi tunazipiga teke. Inasikitisha na kuumiza moyo kufikiri kuwa pengine baada ya karne kadhaa zijazo lugha hizi na hasa zile ndogo ndogo zitaangamia kabisa na pamoja nazo utajiri mkubwa wa kiisimu na kitamaduni. Inavyoonekana hakuna Mwafrika anayejali!
 • Hapa chini ni sehemu ya "silabasi" ya darasa hili na kama unavyoweza kuona, mambo si lelemama!
*****************************
Brief Course Description
This course provides an introduction to the linguistic analysis of Kisukuma – a Bantu language spoken in Tanzania We will look at the characteristic linguistic features of Kisukuma, including its phonetics, phonology, morphology and syntax. We will also look at the social aspects of language, including language variation, language change and borrowing in Kisukuma. Since there are no good sources on Kisukuma language, we will examine its linguistic characteristics through a comparative approach.

Course Objectives
At the end of the semester, students are expected to (1) have a working understanding of the basic linguistic features and peculiar linguistic phenomena in Bantu languages and Kisukuma in particular and (2) have a clear understanding of the contribution of Bantu languages to Linguistic Theory. Graduate students, in particular, will be encouraged to pursue theoretical approaches to the linguistic phenomena that we will encounter in Kisukuma.

Evaluation
Each student will be required to write a high quality graduate-level final paper based on class discussion and readings. The topic selection will be made after discussion with the instructor. Feel free to seek the instructor’s assistance as you think about and proceed to write your papers. The paper must deal with linguistic phenomena in Kisukuma. The final version of the paper will be presented in class starting week 15, and it is due in class on the last day of class i.e. April 21st, 2010.
********************************
 • Hebu tuwasikilize watoto wa Kwaya ya Bethany wakiimba wimbo mashuhuri wa Kisukuma wa Gubyala Ng'wana.... Ni wimbo wa kwanza katika nyimbo za Kisukuma kwenye player hapo kulia.

9 comments:

 1. Nukuu ``Inavyoonekana hakuna Mwafrika anayejali!´´ mwisho wa nukuu.

  Nawasiwasi na hili baada ya kukusoma Prof.

  ReplyDelete
 2. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!February 9, 2010 at 8:45 AM

  Hi nimeipenda na semister ijayo tufundishe Kikurya ama hata kihaya :-)

  @Mt. Simon: nashea nawe wasiwasi wako kwa kuwa hata katika tenga la 'matobholwa' kuna kipande kimoja ambacho utamu wake umepotea ama ni zaidi ya vingine :-(

  ReplyDelete
 3. Nimemwona Mwafrika mmoja anayejali, naye ni Profesa Masangu Matondo Nzuzullima.
  Kazi nzuri Prof.

  ReplyDelete
 4. Mtakatifu Kitururu - nimekubali. Nilizidisha kauli. Kuna Waafrika wengi sana ambao suala hili linawanyima usingizi. Na sidhani kama wewe utakaa tu na kushuhudia Kipare chako kikifa hivi hivi bila kufanya cho chote.

  Ng'wanambiti - Nilipokuwa mwanafunzi kule UCLA nilijifunza Kimasai katika darasa la Field Methods in Linguistics - jinsi ambavyo unaweza kwenda na kufanya utafiti katika lugha ngeni usiyoifahamu. Safari nyingine nikiambiwa kufundisha darasa hili na nikapata mtu anayekifahamu Kikurya sawasawa, idara inaweza kumlipa na wanafunzi wakaanza kukichambua Kikurya chako...

  Halafu inaonekana unapenda sana michembe na Matobolwa. Nina miaka bila kuonja vyakula hivi. Nakumbuka tu michembe na maziwa mgando...haichukui muda mtu ushakuwa mnono!

  Da Subi - wapo wengi wanaoguswa na swala hili. Naamini na wewe ni mmoja wao!

  ReplyDelete
 5. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!February 9, 2010 at 5:38 PM

  Matondo, we ulidhani mwili huu ni wa kitimoto na nyamachoma? ni michembe na matobholwa hayo....lol

  ReplyDelete
 6. Hii sasa kali....najaribu kupata picha mmarekani kuongea kisukuma? na wakimaliza hiyo course wapeleke usukumani ili wakafanye majaribio.

  ReplyDelete
 7. Edna - siwafundishi kuongea. Darasa ni juu ya uchambuzi wa kina wa Kiisimu wa Kisukuma kwa kutumia nadharia za kisasa za Isimu (Linguistics). Ni darasa la kweli kweli ambalo hata Mzungumzaji wa kawaida wa Kisukuma hataelewa kinachoendelea.

  Hata hivyo tayari wanajua kusema mhola na Ng'wanawane! Pengine itabidi niwafundishe kuhusu matobolwa, chagulaga na michembe. We acha tu!

  ReplyDelete
  Replies
  1. Naomba email address yako, nina shida binafsi nawe

   Delete
 8. Naomba mawasiliano yako mkuu. (email)

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU