NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, February 8, 2010

NDEGE MBOVU ZA ABIRIA ZINAPORUHUSIWA KURUKA

 • Mwaka 2006 nilipanda ndege moja ya Air Tanzania kutoka Dar kwenda Mwanza ambayo ilikuwa choka mbaya vibaya sana. Karibu na mlango wa kuingilia katika bawa la kushoto nyaya nyekundu zilikuwa zinaonekana na baadhi ya nati zilionekana kuwa zimelegea. Wakati wa kuruka ndege hiyo (nadhani ni Boeing zile za mwanzo mwanzo kabisa) ilikuwa inatikisika na kupiga makelele kweli. Kwa mtu ninayeogopa kusafiri kwa ndege, hali hii ilinitisha sana na tangu siku hiyo niliapa kwamba sitasafiri na Air Tanzania tena!
 • Nilijipa moyo kwamba hii ni Afrika na mambo kama haya ni ya kawaida. Nilijifariji kwamba ndege kama hii kamwe isingeruhusiwa kuruka katika nchi za wenzetu. Kumbe nilikuwa najidanganya tu. Mambo haya yapo kila mahali.
 • Gazeti la USA Today la tarehe 2/2/2010 lilitoa ripoti ndefu na ya kina inayoonyesha kwamba ndege mbovu na zenye matatizo makubwa ya kiufundi zimekuwa zikiruhusiwa kuruka nchini Marekani.
 • Ripoti iliyotolewa na gazeti hilo inabainisha kwamba kuanzia mwaka 2002 ndege mbovu zimeruhusiwa kufanya safari zipatazo 65,000 - zikiwemo safari ndefu za kimataifa. Ubovu wa ndege hizi unasababishwa na uzembe wa mafundi, kutumia spea pamoja na dhana mbovu wakati wa matengenezo; na kutozingatia masharti ya uendeshaji ndege hizo.
 • Ripoti hiyo inatoa mifano mingine ya kushangaza sana. Mfano mwaka jana injini ya ndege moja ilipata matatizo wakati ndege hiyo ikijaribu kuruka kule Denver Colorado. Marubani waliizima injini ile wakarudi uwanjani na kutua salama. Baadaye iligundulika kwamba mafundi walikuwa wametumia taulo mbili kuziba matundu fulani badala ya kutumia vizibo vinavyotakiwa. Isome ripoti hii hapa.
 • Hitimisho: Usijidanganye kwamba eti kwa vile umepanda ndege inayoendeshwa na shirika la ndege la Ulaya au Marekani kwamba ndege hiyo ni salama. Pengine ndege choka mbaya ya Air Tanzania inaweza kuwa salama zaidi kuliko ndege ya shirika la ndege la Marekani yenye taulo mbili kwenye injini zake.

5 comments:

 1. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!February 8, 2010 at 4:44 PM

  Pole sana Dkt. siye wengine tushazoea kusafiri ktk ndege mbovu manake unaweza ukaondoka Dar mnafika singida mnaona ndege inageuza kurudi Dar na baada ya dk 20 rubani anawambia kuwa amelazimika kurejea Dar kwa sababu ya hitilafu ktk ndege. Hapo ndo utaisikia watu wakikemea MAPEPO :-( Huo ni uzoefu wangu na PW

  ReplyDelete
 2. Hii kali hata mimi nilidhani nege za nje zina usalama zaidi kumbe ni yale yale, poleni sana kwa wale mliosafiri na vyombo hivi vibovu

  ReplyDelete
 3. Binafsi si mpenzi wa kusafiri na ndege. Na ni kwa sababu tunawapa imani waongoza na watengeneza ndege kuliko wanavyostahili.
  Yaani uzembe wa fundi ama ruani unaweza kusababisha madhara makuubwa sana.
  Kwa hapa tunapotngeneza vipuri vyao, wana masharti maguu saana. Tolerance yao kwenye hizo parts ni ndogo na kabla hamjawapelekea kiwandani, mnafanya ukaguzi wa aina nne ama tano. Na hiyo yajumuisha ukaguzi binafsi, wa mtaalamu aliyepitishwa na mamlaka ya anga, ukaguzi wa kwenye fixture ambayo inakuwa na umbo la mahala inapokwenda kuwea, ukaguzi wa mshindilio wa upepo ndai ya maji (kuhakikisha kila sehemu iliochomelewa haipitishi hewa), ukaguzi wa kikemkali (wanaita Fluoresent Peetrant Inspection) na nyingine zaenda kwenye X-Ray kisha wafanye final inspection kuhakikisha kuwa size ya muungu, na specifications zooote ziko sahihi.
  Laki baada ya kupitia msoto huo, unasoma mtu kasahau kufunga nut na hivyo pressure inashuka na kuleta madhara. Ama kama ulivyosema kuahau taulo.
  Ni kweli kuwa yawezekana ule waya ulikuwa ni kwa "easy access" (Hahahahaaaaaaaa)
  Hata nikipandishwa ndege iliyotoka kiwandani leo, sjawahi kufurahia kusafiri kwa ndege (labda pale niwezapo kupiga picha)
  Hakuna kilicho salama

  ReplyDelete
 4. unajua kitendo cha kuruhusu vindege kama hivyo kuruka vikiwa na abiria,ni utovu wa nidhani na ni kutojari maisha ya abiria.vindege vya precision air mimi huwa sivielewi,nje vinaonekana vyenye rangi nzuri ya kuvutia,lakini ngoma nzito ukisha vipanda utaicheza ukiwa angani,utajiona kama umeisha kufa maana vinapiga kelele utadhani labda gari linapita kwenye barabara yenye mashimo!!!

  hivi serikali wanataka ndege zao zilete ajali kwa kuua makumi ya rai ndipo waje kuwa na mawazo ya kununua ndege mpya?au kukarabati ndege hizo kiufundi zaidi? mi nashindwa kujizuia kuwashangaa wahusika,!!! huu si uungwana,ndege ya rais aka!! haina matatizo yoyote,imeka njema kama ya EMERATES! lakini zile za wanyonge kama precision air utakuta hawana fikra ya kuzifanyia ukarabati ile ziwe kwenye standard! mimi hii inanisikitisha sana haswa la viongozi kutojali rai wao kwa kuwatengenezea njia nzuri za usafiri wa anga na nchi kavu na baharini ili nao raia wajisikie fresh katika kuendelea na shughuli zao za kimaisha!
  sasa mimi natoa wito kwa rais kikwete:
  PLIZ RAIS KIKWETE KAMA UNATAKA ILI TUKUCHAGUE TENA MWEZI WA KUMI ILI UTUONGOZE KWA KIPINDI CHA PILI ,TUNAKUOMBA UWAAGIZE WALE WOTE WAHUSIKA KATIKA SHIRIKA LA NDEGE,WAACHE TABIA YA KURUHUSU NDEGE MBOVU KUPAA ANGANI ZIKIWA NA RAI WAPENDWA,ILI ISIJE KULETE KILIO KWA TAIFA."UKIFANYA HIVYO NDUGU MUHESHIMIWA WATANZANIA WOTE TUTAKUPA KURA ZETU.
  SINA LA ZAIDI.
  WENU MWENYE KAJINA KADOGO "TZCHALIA"

  ReplyDelete
 5. Mie naona hasa hizi ndege tunazopelekwa nazo huko kwetu Africa ndio mbovu kabisa!!!! Yaani sio vitu vya kuamini kwa kweli ila somehow tunafika...naogopa kusafiri na ndege (japo tunajikaza kisabuni lol) lakini mmh!!!...

  Sasa si bora hizo ndege kubwa, huo mfano uliutoa wa Air Tanzania...ingekuwa mimi ningezimia kabisa...na hizi ndege za kwetu imani nazo hata sina...ila at the end of the day tunataka kufika mahali na ninavyojionea mie, kwa mapenzi yake Mungu tunafika maana hivi vyombo...si gari wala treni ni salama, not at all!

  PS: Hahahaha, nimeclick ile post tena ya yule rubani aliyetua ndege. I keep on replaying the video and never get tired of it! hehehehehe

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU