NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, February 2, 2010

PADRI WA KIKATOLIKI AKAMATWA KWA WIZI!!!

 • Steven Poole, padri wa Kanisa Katoliki mwenye umri wa miaka 41 amekamatwa kwa kuiba siagi pamoja na kitambaa cha kufunikia makochi katika duka kubwa la Wal-Mart kule Illinois nchini Marekani. Padri huyo alishindwa kulipia kopo la siagi lenye thamani ya dola 3.22 na kitambaa cha kufunikia makochi chenye thamani ya dola 60.00 katika kituo cha kulipia ambacho hakisimamiwi na karani au keshia. Padri huyo alitenda kosa hilo tarehe 25/1/2010.
 • Baada ya kufanikiwa kuiba vitu hivyo, padri huyo alirudi tena katika duka hilo kubwa, akachukua godoro moja spesheli kisha akabadilisha lebo ya bei. Thamani ya godoro hilo maalum ilikuwa ni dola 145 lakini padri huyo alibadilisha bei hiyo na kumfanya alipe dola 31 tu.
 • Mtumishi huyu wa Mungu pia alikutwa na vifaa vya kompyuta ya mkononi ambavyo polisi wanadai kwamba ni vya wizi. Kutokana na kasheshe hili, polisi wamemfungulia mashtaka mawili ya wizi na yuko nje kwa dhamana. Kwa habari zaidi kuhusu kisa hiki soma hapa.
***********************************
 • Kwangu mimi visa kama hivi ni vya muhimu kwani vinasaidia katika juhudi zetu za kuweza kumfahamu hasa binadamu ni kiumbe wa aina gani. Hii ikiwa ni pamoja na unafiki, u-Homo Sapiens pamoja na utakatifu bandia ambao hakawii kujivika!

5 comments:

 1. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!February 2, 2010 at 5:22 PM

  padiri mimi jamani-eti nami nigefanya hivo kwa kuiba matobholwa na michembe mali ya parokia :-)

  ReplyDelete
 2. We Ng'wanambiti wewe. Jaribu kuiba michembe na matobolwa ya parokia uone. Utakula mvua 30!!!

  ReplyDelete
 3. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!February 3, 2010 at 9:19 AM

  Dkt, hudhani kuwa alikuwa anabip kuona kama kuna systems za kuzuia wizi? :-(

  ReplyDelete
 4. "siku za mwisho watenda dhambi (wezi, wadokoji na wabadilisha bei) watalia na kusaga meno"
  wasema mapadri

  hili ndo tatizo la kusomea upadre /utakatifu wakati unazaliwa, huoni kitururu? kausomea wapi?

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU