NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, February 13, 2010

PROFESA AUA WATATU NA KUJERUHI WENGINE WATATU

 • Yalipotokea kule Columbine, wahusika walikuwa ni wanafunzi. Hata kule Virginia Tech na kwingineko, wahusika walikuwa ni wanafunzi. Matukio ya matumizi ya bunduki mashuleni na vyuoni hapa Marekani bado yanaendeelea na sasa yameanza kuhusisha hata maprofesa.
 • Jana Ijumaa majira ya saa 10 jioni Profesa wa Elimu ya viumbe (Biology) - mwanamke aliyepata shahada yake ya uzamifu kutoka katika chuo kikuu mashuhuri cha Harvard - aliwatwanga risasi na kuwaua maprofesa wenzake watatu akiwemo mkuu wake wa idara. Pia aliwajeruhi watu wengine watatu - maprofesa wawili na karani.

 • Inasemekana kwamba tukio hilo lilitokea wakati waalimu hao wakiwa katika mkutano wa idara ambapo profesa anayeshukiwa aliambiwa kwamba maombi yake ya kupatiwa "tenure" yalikuwa yamekataliwa.
 • Kwa habari kamili soma hapa.

2 comments:

 1. Duh! Pole sana! Hii inaonesha kuwa chuo hicho ndo pekee anachoweza kufundisha :-(

  Ama alikuwa na sababu nyingine?

  Mbona hapa kwetu profesa ananyimwa kazi ya kufundisha kwa sababu za kisiasa na bado maisha yanaendelea tu?

  Aaagh!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU