NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, February 16, 2010

SAA ZA WANASIASA ZINAPOTUMIWA KAMA FENI - UCHESHI

Jamaa mmoja alikuwa ananyosha miguu msituni jioni moja wakati wa joto kali. Mara akatokeza katika nyumba moja nzuri iliyokuwa inamilikiwa na ajuza mmoja. Nyumba hiyo ilikuwa na mkusanyiko mkubwa wa saa za ukutani.

"Saa zote hizi ni za nini?" Aliuliza yule jamaa
"Kila mtu hapa duniani ana saa yake" Alijibu yule ajuza kifalsafa na kuendelea "Kila mara unaposema uwongo, saa yako inasogea mbele kwa sekunde moja"

Yule jamaa aliona saa moja ambayo ilikuwa haisogei kabisa.
"Hii saa ni ya nani" Aliuliza kwa shauku
"Hii ni ya Mama Thereza. Haijasogea tangu iletwe hapa miaka mia moja iliyopita" Alijibu yule ajuza.
"Saa za wanasiasa ziko wapi?" Jamaa akauliza.
"Hizo huwezi kuziona hapa"Alijibu yule ajuza halafu akaendelea
"Huwa tunawagawia watu wasio na umeme wakati huu wa joto ili wakazitumie kama feni majumbani mwao"

Yule jamaa alitikisa kichwa chake na kuondoka kimya kimya bila kusema neno!

5 comments:

 1. Kamala nawe Bwana. Gonga hiyo link usome habari juu ya mtawa huyu wa Calcutta - India . Nadhani Wakatoliki wako mbioni kumpa "utakatifu" na wanasubiri muujiza wa pili utokee (unahitaji angalau miujiza miwili itakanayo nawe kuukwaa utakatifu. Muulize Kitururu atakwambia).

  ...Safari ya Mwalimu Nyerere kuelekea "utakatifu" imefikia wapi? Miujiza haijatokea tu kule Butiama?

  ReplyDelete
 2. Matondo umenichekesha sana...leo naona nimekutana na blog ya pili ikiniburudisha vema na kunipa habari..

  nafikiri za wanasiasa wa Tanzania haziruhusiwi hata kutumiwa majumbani maana zina kasi ya ajabu nahisi zinatumika kusukuma mitambo mikubwa ya umwagiliaji...

  tutafika tu

  ReplyDelete
 3. This comment has been removed by the author.

  ReplyDelete
 4. Nanukuu..'Kamala nawe bwana'. Mwisho wa kunukuu. Kaka Matondo huwezi amini na mimi nilipoisoma comment ya Kamala kitu cha kwanza nikasema.., Kamala bwana!! Halafu niliposoma komenti yako nimecheka na nimeshinda nacheka maana niliisoma asubuhi. Kwa kweli Kamala ananikumbusha sana enzi za ujana wangu nilikuwa na misimamo hata yeye ana afadhali. Lakini watu wanasema utu uzima dawa, Siku hizi najiuliza zaidi kwa nini kitu hiki kiko hivi kuliko kukipinga moja kwa moja. Kamala jamani!!!! Sipati picha siku akikutana ana kwa ana na NABII NYAHBINGI

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU