NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, February 10, 2010

FENICHA ZA SERIKALI ZINAPOGHARIMU SH. BILIONI 4.5....

Wakati watoto wake bado wanasomea chini..........................
 • SERIKALI imetumia sh bilioni 4.5 kwa ajili ya ununuzi wa samani za ofisini na majumbani tangu mwaka 2005 hadi 2008.
 • Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa alisema hayo jana bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM), aliyetaka kujua kiasi cha fedha kilichotumika kuagiza samani za ofisi na za majumbani kwa matumizi ya serikali kuanzia mwaka 2005-2008.
 • Alitaka kujua pia kipindi ambacho serikali itaacha kuagiza samani kutoka nje ya nchi na badala yake kutumia viwanda kama SIDO, JKT, magereza na nyinginezo.
 • Akijibu swali hilo, Dk. Kawambwa alisema serikali haiagizi samani hizo moja kwa moja kutoka nje ya nchi bali kinachofanyika ni kwamba baada ya kupata mahitaji na kutangaza zabuni kwa kutumia sheria ya manunuzi mwaka 2004 (21).
 • Aliongeza kuwa kinachofanyika ni makampuni mbalimbali ya kuuza samani hapa nchini huomba na hatimaye huteuliwa na wizara kupeleka samani kwa ajili ya matumizi ya serikali.
 • Hata hivyo waziri huyo alisema ili kuweza kulinda wafanyabiashara wa ndani wa samani, serikali itaendelea kutoa elimu kwa watumishi wa umma kuhusu kupenda kutumia samani zinazotengenezwa hapa nchini.
 • Alisema serikali pia itaendelea kutoa maelekezo kwa wizara na idara za serikali kuhusu kutumia viwango vinavyotolewa na Wizara ya Miundombinu wakati wa ununuzi wa samani.
 • Alisema hatua hizo zitasaidia taasisi kama JKT, SIDO, Magereza na nyingine kuweza kuingia katika ushindani kwa kufuata sheria ya manunuzi ya kuuza samani zake kwa serikali endapo zimekidhi viwango.

2 comments:

 1. "...serikali itaendelea kutoa elimu kwa watumishi wa umma kuhusu kupenda kutumia samani zinazotengenezwa hapa nchini"

  Yaani watumishi wa umma kutumia furniture that is made in Tanzania ni mpaka WAELIMISHWE... Mbona wengine hatuhitaji KUELIMISHWA kuhusu jambo hili? Ina maana fenicha zote zinazokuwa made hapa Bongo hazifai... Yaani hii SIRIKALI yetu hii. Sasa wao wanamwaga more than US dolas 4 million kununua mameza ya thamani wakati watoto wetu hawana madawati na wanakaa chini. Very sad, very sad indeed!!!

  ReplyDelete
 2. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!February 11, 2010 at 9:49 AM

  Anony: nashukuru kwa hasira zako.

  Naomba nikushauri kuzitunza mpaka siku ya kwenda katika kile ki-box cha kura :-(

  Naomba pia nikujulishe kuwa watumishi wa umma na wananchi wanaelimishwa kwa kuwa hatununui fanicha za Tanzania na hazina soko kwa kuwa 'hazina ubora' unaotakiwa :-(

  matokeo yake ni kuwa show-rooms za fanicha toka nje zimejaa na kila mtu awe mtumishi wa serikali ama wananchi wameshobokea kununua za kutoka nje-dubai ama china. Swali ni nani anahakikisha ubora?

  lakini hizo za kutoka china zinatokana na nini? misitu yetu hiyo. Ukisoma hapo chini utaona jinsi tunavoibiwa kwa bei ya chee, halafu wanaziongezea thamani na kuzirudisha tena kwa kuwa pengine inaonekana hatupendi vya kwetu. http://www.tnrf.org/files/E-Mama-Misitu_Info-pack_TRAFFIC_report_summary.pdf

  Na hata hizo zinazoletwa si za kwalite ile inayotakiwa kwa kuwa za daraja ya 1 na la 2 hupelekwa kwenye masoko ya marekani na ulaya :-(

  kama serikali haiwashawishi wananchi wake kutengeneza bidhaa zenye ubora kwa kuwa za dubai zipo. viwanda na mashirika ya umaa tushauza yote kwa bei ya bwerere :-(

  hatuna viwanda weye wategemea nini?

  MADAWATI, SHULE nk si kipaumbele kwa sasa kwa kuwa hatuna sera....iliyopo ni ya KASI MUPYA, NGUVU MUPYA NA ARI MUPYA ilihali huo UPYA hatujui ni wa NINI na utatekelezwa vipi :-( (at least hivo ndovo ninavoona)

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU