NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Sunday, February 7, 2010

WANABLOGU - KAZI YENU SI BURE!!!

Japo kimsingi kazi ya kublogu ni kazi ya kujitolea, inafurahisha kuona kwamba kazi nzuri inayofanywa na wanablogu imeanza kutambuliwa. Kesho si ajabu tukaanza kuona magazeti yakitenga kurasa kwa ajili ya yaliyojiri bloguni. Hali kadhalika vipindi vya leo magazetini katika redio zetu. Naamini huu ni mwanzo mzuri. Hongereni wanablogu. Kazi yenu si bure ati! Maelezo hapa chini ni kutoka kwa Mwanakijiji.

*******************************
Wanalibeneke na vyeti vyao vya shukurani toka Serengeti ambao kwa mara ya kwanza wameonesha mfano wa kutambua umuhimu wa globu na kuwaenzi waendeshaji wake. Toka shoto ni Ankal wa Globu ya Jamii, John Bukuku wa Fullshangwe.blogspot, Geofrey Mwakibete wa Mohammeddewji.com, Muhidin Sufiani wa Sufianimafoto.blogspot.com na Michuzi Junior wa Jiachie. ( Picha: Michuziblog)

3 comments:

 1. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!February 8, 2010 at 8:26 AM

  na nyie ambao hamkupewa vyeti hao wamewawakilisha, I pressume!

  Hivo hongera ni kwa woooote isipokuwa tu wale wanaotoa maoni :-(

  ReplyDelete
 2. Ng'wanambiti - hatuwezi kuwasahau watoa maoni na hasa wale makini kama wewe. Kimsingi ninyi ndiyo mnatoa mwelekeo wa blogu hizi na kuchochea fikra za wanablogu.

  Utaanzisha blogu yako lini? Ninataka kujua mambo ya Kikurya kurya.....

  ReplyDelete
 3. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!February 8, 2010 at 6:03 PM

  Masangu, bado nafikiria hasa nini cha kuandika kwa kuwa unaweza ukaanzisha blog halafu inakosa mwelekeo.

  Halafu sijajua jina la blog kwa kuwa nikishajua jina itakuwa rahisi kwangu kujiweka katika mtiririko huo ....lol

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU