NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, March 17, 2010

EMBE LILILOCHUMWA NA LILILOACHWA LIKAIVIA MTINI

 • Embe lililochumwa na lile lililoachwa likaivia mtini mpaka likadondoka lenyewe yanaweza kuwa na ladha tofauti
(Nilikuwa nafikiria jambo fulani la muhimu ndipo nikamkumbuka 
mjomba wangu mmoja aliyekuwa na miembe mingi sana...)

6 comments:

 1. CHUKULIA EMBE KAMA MAISHA. Ama kitu chochote maishani.
  Kuna tofauti kubwa kwa kitu chochote ambach kimekuwa tayari kwa njia ya asili na kile kilicholazimishwa kuwa tayari.
  Iwe ni embe, ndoa, uzazi, uchumba, biashara na mengine mengi
  Tunalotakiwa ni kusaidia njia ya asili kutuwezesha kupata tupatavyo kiasili, lakini tatizo letu sisi ni kuwa tunalazimisha kupata vitu vifananavyo na vya asili kwa njia zisizo za asili tukijifanya eti "twaharakisha upatikanaji"
  Ukiwaza kwa undani, POST HII INA MAANA KUUUBWA SANA KATIKA MAISHA YETU

  ReplyDelete
 2. Jamani duh! umenifanya mate yadondoke maana embe imeiva vizuri hiyo! Umenikumbusha mwaka jana niliyala maembe mpkaka....!Asante kwa kunitamanisha.

  ReplyDelete
 3. Jamani ndo nini hii kudondoshana udenda kwenye kompyuta zetu kwa picha hizi nzuri hivi? mwe, mwe, mwe umenikumbusha enzi za kudamka alfajiri kuokota maembe zafarani, kha! Asane!

  ReplyDelete
 4. wenye kudondokwa na udelele mtajiju...lol

  Ukweli ni kuwa japo yote ni maembe kwa vitamini lakini ni tofauti kwa ladha...lol

  Nakubaliana na kaka wa Msee ya Changamoto!

  ReplyDelete
 5. jamani hilo embe mwe, nimelitamani we acha tu.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU