NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Sunday, March 7, 2010

FIKRA YA IJUMAA: KARIBU KILA MTU ANATAKA KWENDA PEPONI; LAKINI PEPO IPI?

 • Kifo. Ndiyo kifo. Kipo, kilikuwepo na kitakuwepo. Pengine siku moja kitakoma...
 • Kifo, kimemsumbua binadamu tangu enzi na enzi na kimeyakunguwaza na kuyashinda matumaini yake ya kuishi milele.
 • Ati, kipi ni bora? Kufa na kusahaulika (na pengine kukumbukwa - kwa mema au mabaya) au kuishi milele, hata kama ni milele isiyo timilifu?
 • Wapo wanaoamini kwamba dini "ziligunduliwa" ili kuendelea kupalilia matumaini ya binadamu ya kuishi milele. Ndiyo maana kila dini inatoa matumaini fulani ya umilele peponi ama kwingineko.
 • Wikiendi iliyopita nilikuwa namsikiliza mchekeshaji mmoja akijaribu kuhoji hii dhana ya kuishi milele peponi. Kimsingi alikuwa analinganisha pepo zinazoahidiwa na dini mbalimbali.
 • Alisema kwamba pepo pekee inayomsisimua ni ile inayoahidiwa katika Uisilamu. Inasemekana kwamba katika pepo hiyo, ukitekeleza majukumu yako vizuri hapa duniani, kuna uwezekano wa kuishi na mabikra tena wasiomaliza ubikra hata baada ya kuwabikiri milele na milele. Mchekeshaji huyu alisema kwamba hii ndiyo pepo hasa atakayopigana kufa na kupona mpaka aingie!
 • Aliendelea kusema kwamba pepo inayoahidiwa katika Ukristo kidogo inaboa. Inasemekana katika pepo hiyo kuna kuimba, kupiga vinubi na kumsifu Mungu usiku na mchana milele na milele. Alisema kwamba hana uhakika kama anataka kuishi maisha yake ya umilele namna hii.
 • Pepo zingine zote, hazivutii na zingine zinatisha. Aliitaja ile ya "incernation" ambako kuna uwezekano wa kuzaliwa tena na tena katika maumbo mbalimbali - na wakati mwingine ukiwa kama mnyama. Alisema kwamba hataki pepo hii ya kubahatisha.
 • Hitimisho lake: Pepo pekee inayovutia na ambayo inapaswa kupiganiwa ni ile inayoambatana na kufaidi mabikra wasiomaliza ubikra!
 • Ambacho alikisahau mchekeshaji huyu ni kile kinachoahidiwa kwa wale ambao hawatakwenda katika pepo hizi. Katika Ukristo kuna moto wa milele. Kwenye Uisilamu sijui makafiri wanasubiriwa na adhabu gani. Mimi nadhani ni bora kuishi kwa kuimba, kupiga vinanda na kumsifu Mungu usiku na mchana milele na milele kuliko kuitumia milele yote katika Ziwa la moto ambako inasemekana kuna kuungua bila kuteketea. Oh, mateso yaliyoje!
 • Makanisa mengine kama Mashahidi wa Jehova wanaamini kwamba moto wa milele ni mafundisho ya Kipagani yaliyoingizwa kinyemela katika Ukristo na kwamba Mungu mwenye upendo usiopimika kamwe hawezi kuwachoma binadamu aliowaumba mwenyewe milele na milele. Kifo ndiyo Jehanamu yako!
 • Kwa wengine pepo na Jehanamu ziko hapa hapa duniani!!!

Swali la kizushi: Ati, nawe wategemea kwenda peponi? Ipi?

*****************************
Natamani kama ningekuwa na uwezo wa kuiandika fikra hii katika mtindo wa Mtakatifu Kitururu. Hoja ingenoga ajabu lakini wapi. Nimejaribu nimeshindwa. Hata hivyo natumaini kwamba hoja imeeleweka; na kwamba sijamkwaza mtu!
******************************

5 comments:

 1. kifo, pepo nk. tatizo la imani ni kuonge hata vitu vya ajabu. kama aliyeeelezea juu ya pepo ya mabikra, angeishi na kufikia umri wa kuona ngono haina maana, angebadilisha sifa za pepo hiyo na labd akuwa pahala pa wazee

  pepo na kuzimu zote tunazo hapa duniani na maisha yetu yamegeuzwa kuwa ya kuzimu zaidi japo kuna watu wanaoishi peponi wakiwa duniani. peo inaanzia hapa hapa.

  swala la incarnationa niliwahi kuliongelea na lipo isipokuwa kwa wanaoishi peponi wakiwa duniani. ANGALIZO; pepo niziongelezo ni tofauti na za dini hizo mbili.

  ReplyDelete
 2. Mimi nakiri sipendi Mabikira kwa sababu nyingi ,...

  ..... moja wapo ikiwa ni kuwa kwao bila uhakika kwamba shughuli ni shughuli au wanajaribu na faida kwao kikauli yaweza kufupishwa TU kwa sentensi `` Jamani INAUMA lakini endelea tu mie nakupenda!´´:-(

  ...kwa hiyo MBINGU ya KIISLAMU inaweza kunitesa nikifikiria inabidi nifundishe au tu nielezee sana NINIKITEKENYWE hasa wakati hamu inahitaji vitendo.:-(

  Lakini CHAKUJIULIZA tukiwafikiria hao MABIKIRA ambao nikiwa bomba la JAMAA watashughulikia uwaji wangu MBINGUNI ,- hivi hao mabikira MBINGUNI YAO waipendayo ni kushea?

  Ya KIKRISTO kwa kweli inaboa kwa karibu kivyovyote nilivyoisikia kwakuwa ingawa nimeimba sana katika kwaya za KILUTHERI na MAKANISA MENGINE ila bado baada ya kwaya kulikuwa na ustaarabu mwingine wa kuchochea mishemishe ya siku ambayo ilikuwa ina BALANCE kuimba na michepuo mingine ya sayansi ya siku.:-(


  Hiyo ya kufa na kugeuka sisimizi chakula cha MJUSI mie AKA BABU WEE, kwa maana nikija kuzoea kuwa SIMBA litakuwa bonge la tatizo kuonyesha maringo kisa nimezaliwa upya na kuwa SWALA katika vichaka vilevile.:-(

  Halafu kuchomwa MILELE nakositaki.:-(

  SHUGHULI NINAYO !:-(

  ReplyDelete
 3. Kinachotusumbua sisi b'damu ni hii kitu inayoitwa akili. Unafikiri ng'ombe wanajua kwamba one day watakufa? Na kama hawajui basi everything is fine na hakuna haya mambo ya kutishana kuchomana moto na kuzaliwa upya in a form of ants.

  Intelligence is a curse to human beings!!!

  ReplyDelete
 4. Hii blogu ina mambo ya ajabu

  ReplyDelete
 5. Kamala: Hebu uje utuelimishe vizuri kuhusu "incarnation." Waifu wangu anafanya kazi na jamaa mmoja kutoka Asia ambaye anaamini kabisa kwamba aliwahi kuishi hapa duniani zamani ingawa hakumbuki aliishi katika umbo gani. Pia anadai kwamba anaweza kukisia atarudi katika umbo gani hapo baadaye!

  Mtakatifu: Vipi ikiwa hawa mabikra wa peponi wanafahamu kila kitu na hawahitaji kufundishwa? Utaifagilia pepo yao? Umenichekesha kuhusu uimbaji wako katika kwaya za Kilutheri na jinsi chanya na hasi zilivyogongana huko...

  Anony wa kwanza: Siamini kama akili ni laana kwa binadamu. Akili hiyo imeweza kumwokoa binadamu kutoka katika mikatale ya kimazingira na kumpa uwezo wa kuwatawala wanyama wengine ingawa bado anauawa na bakteria na virusi ambavyo hata hawezi kuviona! Tatizo ni kwamba kuna wakati ameitumia vibaya akili hiyo...

  Anony wa pili: Sijawahi kufikiria kama blogu hii ina mambo ya ajabu. Waweza kutoa ufafanuzi kidogo?

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU