NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, March 19, 2010

FIKRA YA IJUMAA: MASWALI YASIYO NA MAANA YO YOTE

 1. Ati, kama mtu angekuita kwa jina lisilo lako, ungeitika?
 2. Leo unafikiri kwamba unachofikiri ndicho unachofikiri?
 3. Unafikiri kwamba unachokifikiri kwa sasa ndicho unachopaswa kukifikiri?
  Fikiri!!!
  Wikiendi njema.

  7 comments:

  1. Swali tamu haswaa!

   wengi huitika majina yasokuwa yetu na kufikiri kusikokuwa kwetu :-(

   Tunafikiri vile tulivofunzwa na wazazi, ndugu, jamii na marafiki! Tunaitwa na kuyaishi majina tulochaguliwa katika maisha yetu.

   ni changamoto kwa kweli.

   ReplyDelete
  2. Ukiniita hata kwa mluzi sigeuki achana mbali na kuniita jina lisilo langu.
   Pia haya majina ya kukodi mh!!

   ReplyDelete
  3. Siitiki kwa jina lisilo langu,kuhusu kufikiri sina hakika kama ninacho kifikiria sasa ndicho nitafikiria baada ya lisaa limoja.

   ReplyDelete
  4. sisi huwa hatufikiriii maranyingi kwani tunagonganisha fikra za wengine na kuzaa utofauti tunaouita fikra zetu.

   ndio maana matondo ni mkristo/anadini utadhani ni yake.

   natumia majina ya wazazi walionipajchika lakini la ukristo nimelitema

   nikiona kwamba ninachofikiri sicho nilichopaswa kufikiri then nafanya meditation kidogo

   ReplyDelete
  5. 1. Hapana sitoitika, kwasababu sio langu na sio "identity" yangu. Lakini hata hivyo, I think kwa binadamu huwezi kuitikia jina ambao sio lako.

   2. Hehehehe....sijui!

   3. Ninachofikiria sasa ni kujibu haya maswali matatu ambayo mawili kati yake sidhani kama napaswa kufikiria ninavyofikiria....

   .....mmh (thinking...)

   ReplyDelete
  6. 1) Sitaitika maana sitajua kama anaongea na mimi.
   2) Hapana kwa sababu ninayetaka kumfikiria wewe umeniambia nisimfikirie (Baba Ariana)
   3) Hapana.

   ReplyDelete
  7. Asanteni. Hili swala la kufikiri nililifikiria baada ya kumtazama Dr. Wayne Dyer akilizungumzia kwa undani. Alikuwa anasema kwamba nguvu ya fikra inaweza kubadili kila kitu na kutupatia kila kitu tunachokihitaji katika maisha yetu. Tatizo letu ni kwamba wengi wetu hatujui kufikiri na mara nyingi tunafikiri vitu ambavyo hatupaswi kufikiri ambavyo ni shaghalabaghala tu bila mpangilio.

   Kama alivyosema Kamala, ku-meditate ni njia mojawapo muhimu iliyothibitishwa kwamba inaweza kuyarudisha mawazo na kumakinikia lengo lako la siku hiyo ili hatimaye kuweza kufikia lengo la jumla. Dr. Wayne Dyer ni mmojawapo wa walimu niwapendao sana kutazama programu zao kwani mambo anayoyazungumzia huwa hayaegemei katika miujiza (ambayo huna guarantee ya kutokewa nayo) bali ni mambo ambayo unaweza kufanya mwenyewe tu na ukaleta mabadiliko unayoyataka katika maisha yako. Mojawapo analolisisitiza mara kwa mara ni ku-meditate! Kitabu kimojawapo ni hiki: http://www.hayhouse.com/details.php?ref=89&id=3187

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU