NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, March 17, 2010

HII IMEKAA VIZURI: POLISI AKATAA RUSHWA YA DOLA 3,000. ATUZWA TSH. 4,000,000!!!

  • Askari namba E. 7235 PC John Anthony Mwesongo wa kituo cha polisi cha Polisi Kiwanja cha ndege cha Mwalimu Julius Nyerere ambaye ni mtunza vielelezo wa kituo hicho, akionyesha hundi ya T. Sh. 4,000,000 motisha baada ya kukataa rushwa ya dola za kimarekani 3,000 na watu waliokamatwa na madawa ya kulevya waliomtaka abadilishe vielelezo hivyo. 
  • Hundi hiyo alikabidhiwa na Inpekta Jenerali wa Polisi (IGP), Saidi Mwema Jana  (13/3/2010) katika ukumbi wa maofisa wa polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam. (Picha Na Hassan Mndeme- Jeshi la Polisi) 
  • Hongera PC John Anthony Mwesongo. Wewe ni mfano wa kuigwa! Picha na maelezo ni kutoka kwa Mzee wa Mshitu.

1 comment:

  1. Ninalowaomba hawa wahusika wa jeshi wamuhamishe kisha wasiseme anahamia wapi. Maana kama ulivyoandika kuwa waliotaka kumpa pesa ni WAUZA MADAWA ambao wana mtandao (network)
    Namtakia maisha ya salama na yenye utii.

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU