NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, March 3, 2010

HISABATI SIYO MCHEZO ATI!

 • Unakokotoa weeeee, halafu......????

7 comments:

 1. Mimi nakiri hisabati zilinipiga mweleka kabisa. Mpaka kesho huwa nazikimbia

  ReplyDelete
 2. Halafu unapata ZERO...lol

  Ni changamoto kwa kweli!

  Juzi nimeona katika TV prof mmoja wa Hisabati hapo UDsm analalamika sana juu ya wanafunzi kutofaulu/kutopenda somo hilo, nkashangaa!

  Kwa kuwa hata kulalamika kwake ni sawa na huo mkokotoo hapo juu...lol

  ReplyDelete
 3. hahahhaaa,mimi sisemi...maana zilinipitia kushoto.

  ReplyDelete
 4. nilipenda sana hesabu, lakini walimu walikuwa wanakuja na kiboko na hivyo kuogopa kiboko.

  ila hisabati infanana na philosophy na siasa kwa upande mwingine. unatafuta vijisababu tu mpaka unkubalika.

  mke wangu ni mtaalamu wa hii kitu

  ReplyDelete
 5. Nilipofika darasa la sita mwalim wa Hesabu alininyanyasa sana kwenye hesabu!Nikaenda sekondari tulipofanya mtihani wa form two tukalazimishwa kusoma additional maths na baade tukalazimika kusoma pcm. matokeo nikajikuta nikisoma degree ya hisabati na fisikia. nikaishi kama mtumwa wa masomo hayo mpaka leo!!Nimelazimika kuingia kwenye applied maths kama kujiliwaza na makali ya hisabati!!Maisha ya kulazimishwa na mfumo kutokana na kujiweza kidogo hisabati ingawa haikuwa hobbie yangu!!

  ReplyDelete
 6. Kumbe tuko wengi ambao Hisabati ama zilitupiga chenga ama hatukuzipenda kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo ukali wa walimu na kutofundishwa vizuri. Ndiyo maana mwaka huu niliamua kujitolea kufundisha hesabu darasa la tatu katika shule moja ya umma hapa Marekani kila siku za Ijumaa na Alhamisi. Lengo langu hasa lilikuwa ni kujifunza jinsi watoto wa wenzetu hawa wanavyofundishwa somo hili muhimu. Nimejifunza mambo mengi sana ambayo nategemea kuyajumuisha katika kijitabu changu kimoja ninachokazana kukimalizia. Darasa lina watoto 19 na kati yao ni wawili tu ambao wameshaniambia mara nyingi kwamba wao na hesabu si marafiki. Waliobaki wanasema wanazipenda sana kwa sababu ni raha kujifunza, zinaburudisha na zinawasaidia kuelewa mambo mengi ikiwemo kuhesabu pesa zao wanazojiwekea akiba (watoto hapa wana tabia ya kudunduliza "chenji" kwenye makopo yaitwayo "piggy bank").

  Ng'wanambiti - huyo Profesa mwambie kwamba somo hili likifundishwa vizuri na wanafunzi wakaelewa umuhimu wake basi pengine hali itabadilika. Kuna matatizo mengi sana katika ufundishwaji wake na mimi kusema kweli sikuelewa ni kwa nini tulikuwa tunalazimishwa kukokotoa namba na alama ambazo hazieleweki. Tazama hapa: http://matondo.blogspot.com/2009/12/wanafunzi-sikilizeni-msidharau-somo-la.html

  Edna na Upepo Mwanana: Ni kweli ziliwapiga chenga au pengine hamkuzipenda kutokana na sababu zingine tu?

  Kamala - hapo mbona patamu? Mama Bingwa wa Hisabati na wewe kingunge wa falsafa na utambuzi. Watoto watakuwaje? Mi nasubiri!

  JPNtisi - Si haki kusoma kitu ambacho hukipendi. Ndiyo maana watu kama miye sikuogopa kuitwa 'ngwini' au 'kilaza' kwa kuamua kusoma HGK badala ya PCM/PCB/...Kusoma na kufanya kitu ukipendacho hapa duniani ni muhimu zaidi kuliko kufuata mkumbo. Natumaini kwamba umeshajishabihisha vizuri na taaluma yako hiyo - japo ni kwa shingo upande!

  ReplyDelete
 7. unapigwa bonge la X! then 0/10 then anakupa na dongo la mwisho linasema SEE ME! weweeeeeee....yh sometimes I don't miss primary school :-|

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU