NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, March 16, 2010

JAMII AMBAYO BADO INASHABIKIA MAMBO HAYA INA MUSHKELI!

 • Nina wasiwasi sana na jamii ambayo katika karne hii na wakati huu tulionao bado inafagilia mambo ya kupiga ramli na kusoma alama za vidole kama njia ya mkato ya kufikia malengo yake.
 • Upigaji wa ramli, usomaji wa nyota za watu na alama za vidole vinapochukuliwa kama njia mojawapo muhimu ya kutatulia matatizo ya jamii na kuijengea matumaini ya wakati ujao (mf. bahati, utajiri, mafanikio katika ndoa, kilimo, michezo n.k), jamii hiyo kwa hakika ina lake jambo.
 • Pengine hatupaswi kushangaa ndugu zetu maalbino wanapochinjwa kikatili eti kwa sababu viungo vyao vinafungamanishwa na ngekewa ya utajiri, au watoto wachanga wanapokatwa mikono kwa sababu tu eti viganja vyao vina alama zenye bahati.
 • Ni wazi kwamba jamii ya aina hii ina matatizo na ni wajibu wetu sote kuitafutia dawa. Uongozi bora na elimu makini ndiyo mkakati mama katika kujaribu kuikomboa jamii ya aina hii.

4 comments:

 1. Ndo maana wewe nakwambia ni Professor wa kiswahili (tena feki)! Sasa nisome hivi...Hiyo elimu ya nyota (unajimu), kama hujui ni elimu ya science ya nyota inasomewa na kuna hadi ma professor wa elimu hiyo (Astrology), and hence so called Astrologers. Elimu hii ni ndugu na elimu ya astronomy, na kwa maana hiyo wana share baadhi ya methods! Ni elimu kama elimu nyengine, kama kilivyo kiswahili chako!

  ReplyDelete
 2. Ni yule rafiki yangu fundi mangungo nini asiyependa walimu wa lugha? Karibu tulonge!

  Ninajua kwamba kuna unajimu na Wanaastronomia mashuhuri kama Johannes Kepler, Nicolaus Copernicus na Galileo Galilei walikuwa pia wataalamu wa nyota. Hata "watabiri" maarufu kama Nostradamus walitegemea nyota (tazama hapa: http://matondo.blogspot.com/2009/10/mwaka-2012-ndiyo-mwisho-wa-dunia.html)

  Tunajua pia kwamba elimu yo yote ile - hata iwe nzuri namna gani - ikitumiwa vibaya inaweza kuleta madhara katika jamii. Na hili ndilo lengo langu kuu katika andiko hii.

  Wakati elimu hii ya nyota imesaidia kuleta mabadiliko kwingineko, mimi nadhani kwamba inatumiwa vibaya katika jamii yetu. Jamii yetu bado inaamini katika imani za kishirikina na haya mambo ya kupiga ramli ama kwa mganga wa kienyeji au kwa mtaalamu wa nyota yametajwa sana kuwa yanachangia katika matukio ya kushangaza tunayoyashuhudia kama vile mauaji ya maalbino na mengineyo. Elimu hii na imani zetu za kishirikina zinapogongana zinaweza kuleta madhara.

  Napenda pia niseme kwamba sina ugomvi na Mzee wa Mwembechai na nadhani anaweza kutoa mchango mkubwa katika kuielimisha jamii kuhusu elimu hii kwa kuwa bayana na kuonya kuhusu madhara yake ikitumiwa vibaya na watabiri wenye tamaa ya kujitajirisha haraka haraka.

  Kuhusu kuwa profesa feki wa Kiswahili hapo sina la kusema mkuu. Eti nasi wanaisimu (linguists) huwa tunajiona kuwa tumesomea taaluma muhimu sana kwa binadamu kama taaluma zingine, kumbe tunakosea. Tunapaswa kuona aibu na kukaa kando kwani elimu tuliyosomea haina hadhi na haituwezeshi hata kutumia haki yetu ya kikatiba na kibinadamu - haki ya kutoa maoni yetu - bila kubezwa!

  http://matondo.blogspot.com/2010/02/fikra-ya-ijumaa-ati-msomi-ni-nani.html

  ReplyDelete
 3. Mwanisongole (Houston TX)March 16, 2010 at 11:29 PM

  Hebu tuacheni kubabaishana. Astrology ni academic ya shetani/darkness na hata siku moja cannot be compared with pure science kama Astronomy. Nadhani kila Astronomer anajua kuhusu alignment za nyota (this is a fraction of what they do) ingawa lengo lake siyo kudanganya watu. Lakini kila astrologer siyo lazima ajue anything about Astronomy, which is pure science.

  Hawa palm readers kama huyu mzee wana tofauti gani na waganga wa kienyeji? Isn't this the same guy who said sijui mtu akimoppose Kikwete kwenye election ya mwaka huu basi atakufa? Come on people. This issue doesn't even merit our discussion and fighting. I also don't understand why there are tv programs to propound this crap. What is the purpose of these programs? Kufundisha kupiga ramli or what?

  ReplyDelete
 4. ni muhimu katika ulimwengu wa kukua kiroho. ila ni changamoto kweli inabidi kuelimisha watu wetu wajitambue

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU