NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, March 20, 2010

JAPO KILIO NI TIBA, TAFADHALI USILIE MBINGUNI....


Kama ungeangua kilio mbinguni, kila mtu angeangua 
kicheko akidhani kwamba ulikuwa unatania tu.

4 comments:

 1. Kadiri ya mapokeo ya kidini MBINGUNI ni furaha mtindo mmoja...lol

  Hivo hakuna hata awezaye kufikiria kuangua kilio kwa kuwa wenye kulia wako Jehanamuuuu!

  Pengine ujumbe huu unaweza kuupeleka kunako kumbi za Arusi...lol

  Hivi ni kwa nini wazazi wa bibi arusi hulia? Ni jambo la furaha tu huko lakini kwa nini kilio?

  Hivi ni nini bibi arusi hutoa mchozi siku ya arusi? Ni kwa sababu ana furaha ya kuolewa au ya kuwaacha wazaziwe? Kama ni kuwaacha wazaziwe kwa nini asivue hiyo shela na kurejea nyumbani/

  Ninajaribu tu kulalama kipumbavu kwa kuwa huwa sipati picha....lol

  ReplyDelete
 2. We nawe - ulishawahi pia kujiuliza why wanawake hulia wakati wa ligwaride. Tena Kurya women ndo usiseme. Sometimes ndo wako on top commanding the troops. Mbona tu wasinyanyuke and that will be the end of the cries? Why???

  ReplyDelete
 3. matondo wewe mara ya mwisho ulilia lini na nini kilichokuliza?

  ReplyDelete
 4. Ng'wanambiti - Kila kitu kipya kinabeba gunia la sintojua na wasiwasi sana. Na mazoea yana tabu. Kwa hivyo bi Harusi akifikiria kwenda kuanza maisha mapya (ambayo yamejaa sintojua) na kuacha maisha aliyoyazoea (ambayo hayana sintojua) basi anakuwa na wasiwasi. Na wakati mwingine anaweza kuwa analia kwa furaha. Pengine majibu kutoka kwa akina Yasinta na Mwanamke wa shoka yatatupa mwanga zaidi.

  We anony. nawe. Una lako jambo. Hujasikia kwamba wakati mwingine wanaume ndiyo hulia? Mbona hao nao hawanyanyuki na kwenda zao?

  Kamala: Jana nilikuwa naangalia kipindi kinachoitwa "World's Dumbest Partiers) na kulikuwa na arusi moja ya Kirusi. Upande wa bi harusi ulihisi kwamba upande wa bwana harusi (ambao ni matajiri sana) ulikuwa unaonyesha dharau. Basi ngumi zikafumuka kati ya pande hizi mbili. Yaani ilikuwa ni vurugu mechi ya vuta nkuvute kwa masumbwi ya kweli kweli na huku akina mama wakitumia viatu na kila silaha waliyoweza kuipata. Yaani zilipigwa mpaka baba wa bwn. harusi akafleti. Hali ilipotulia, wenye kuvuja damu wakajisafisha na yule aliyekuwa amefletishwa akafufuka, basi familia zote mbili ziliingia jengoni na harusi ikafungwa bila wasiwasi. Tena wakakumbatiana kwa upendo na kutakiana mema.

  Jinsi mwendesha kipindi kile alivyokuwa akisimulia tukio hili na jinsi ngumi zenyewe zilivyokuwa zikiungurumishwa nilijikuta nikicheka sana na mwishowe nikaishia kulia. Sijui ni kwa nini niliishia kulia lakini baadaye nilijisikia furaha, nikakoga na kwenda maktabani.

  Kilio ni "Catharsis" na wakati mwingine kunasafisha nafsi. Ndiyo maana si busara kumkataza mtu mwenye huzuni kulia. Isitoshe kwenye kulia ndimo pia mna kucheka (and vice versa). Ndiyo maana nahisi kuna watu ambao pengine mbingu inaweza ikawaboa kwa vile tunaambiwa huko hakuna kulia!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU