NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Sunday, March 28, 2010

NENDENI MKASALI KWANZA, POMBE MTANUNUA MKITOKA MAKANISANI!

 • Hapa Florida (na naamini hata katika majimbo mengine) siku za Jumapili vilevi haviuzwi mpaka ifike saa saba mchana. 
 • Nilipoulizia niliambiwa kwamba lengo la sheria hii lilikuwa/ni kuwahimiza watu kwenda makanisani kuabudu nyakati za asubuhi badala ya kuanza kuhangaika na pombe. 
 • Hata hivyo mtu unaweza kujiuliza, kama mtu hataki kwenda kanisani siku za Jumapili na badala yake anataka kuanza kuzitwika asubuhi asubuhi, kuna ugumu gani wa kujinunulia kilevi akipendacho mapema?

6 comments:

 1. Ni kweli kabisa kumshukuru Mungu kwanza na ndipo hayo mapombe. Lakini kumshukuru Mungu ni sehemu yoyote ile sio lazima kanisani au?

  ReplyDelete
 2. Hahaa,sasa mtu si anaweza nunua jana yake, ili azinywe jpili wengine wakiwa kanisani? sidhani kama hiyo mbinu itasaidia kuwashawishi watu kwenda makanisani. Labda wangesema atakaye uziwa bia ni yule tu ambaye alikwenda kanisani...Sasa sijui atathibitishaje lol....

  ReplyDelete
 3. unaweza kuta zile ulizonunua jana yake ulizinywa jana hiyo hiyo hadi zikaisha.. sasa inabidi uamke asubuhi ukatafute za kuzimulia.. patamu hapo!

  ReplyDelete
 4. inabidi ziwe zinauzwa kanisani. kwani mvinyo si kilevi?? fikri kanisa likiuza pombe, litajaa na sadaka kibao

  wahaya wanasema hivi: akwima marwa, akulokola tamiilo

  ReplyDelete
 5. Nafikiri sheria hiyo ilitungwa na wasiokunywa pombe!

  ReplyDelete
 6. Da Yasinta: Pole sana kwa kuwa kuna watu wanakwenda kanisani wakati mawazo yao yako BAA!

  si afadhali waruhusiwe tu kugida?
  Nakumbuka wakati fulani wa krismas mzee wangu akiwa amepitia katika moja moto-moja baridi (SIMSHITAKI KWENU, ebo!) akaja katika misa ya usiku.

  Mimbarini pamoja padre nilikuwapo mie kama mtumikiaji (minstrant kama tuitavyo na mkanzu mweupeeee)!

  Basi Padre akisema Bwana awe NANYII! yeye kwa sauti kubwa AWE PIA NAMIIIII!

  Padre akiwambia INUENI MIOYO yeye Nimeshaiua glasi huko nilikotoka....lol

  Kimbembe ni pale wakati wa kusimama na kukaa...yeye alikuwa anafanya kinyume...lol

  Swali: na waislamu nao hulazimishwa hivo siku ya ijumaa ama hawako hapo kwenyu?....lol (nauliza nikijua kuna wengine wagidao hata visivoruhusiwa kama baadhi ya wasabato wanavokandamiza samaki ambao hawaruhusiwi)....lol

  HITIMISHO: hakuna mantiki yoyote kumhimiza mtu kwa kumlazimisha anywe kwa wakati ule watawala wapendao kwa kuwa anaweza kuwa amelewa kabla hata hajenda huko....lol

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU