NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, March 16, 2010

POLISI ATUHUMIWA KUTAZAMA VIDEO ZA NGONO KWENYE SIMU YAKE AKIWA KAZINI. AJIUZURU

  • Polisi mmoja katika mji ninaoishi amejiuzuru kazi wakati akiendelea kuchunguzwa kwa kosa la ku-download na kutazama video za ngono katika simu yake aina ya ipod touch (kama hiyo juu) wakati akiwa kazini.
  • Katika kipindi fulani polisi huyo aitwaye Laurence Gilbert alimwomba polisi mwenzake wa kike ajumuike naye katika kutazama video hizo chafu. Badala yake polisi huyo wa kike alikwenda kutoa taarifa kwa bosi wao akidai kuwa alikuwa amenyanyaswa kijinsia.  Habari kamili inapatikana hapa.
  • Sehemu nyingi za kazi zimeshapiga marufuku mambo kama haya na zinafuatilia shughuli zote zinazofanywa na wafanyakazi wao mtandaoni hasa wakati wakiwa kazini. Makampuni mengi pia yanafuatilia mazungumzo ya wafanyakazi wake katika tovuti za kijamii kama facebook na myspace. Mzee wa Changamoto alishawahi kuonya kuhusu jambo hili. Na Mura kutoka kijijini Mataranyirato pia alishawahi kugusia kuhusu wanaume laptop.
  • Tuwe waangalifu!

2 comments:

  1. Kaka Matondo, uchunguzi huo ukifanywa hapa Bongo utawagharimu wengi sana kazi zao. Niseme asilimia kubwa ya wafanyao kazi katika ofisi zenye mawasiliano ia intaneti watabambwa.

    ReplyDelete
  2. Hawa nao wamezidi. Simu ingekuwa ya ofisini ndiyo ingekuwa noma. Simu si kanunua mwenyewe sasa noma ya nini? Huyo polisi wa kike naye fala tu.

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU