NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, March 8, 2010

SIKUJUA KAMA KUNA "RADIO IKULU MBINGUNI" MPAKA NILIPOKUTANA NA HII TAARIFA YA HABARI

 • Kama mkereketwa wa masuala ya lugha, nimevutiwa na Kiswahili kilichotumika katika taarifa hii ya habari. Huyu jamaa ni mtangazaji mzuri sana na lugha ya Kiswahili anaimudu vyema!

4 comments:

 1. Nimeipenda sana hii taarifa ya habari kutoka mbinguni,nimekuwa nairudia kuisikiliza zaidi ya mara 4,na bado nahamu ya kuendelea kuisikiliza,asante sana kaka kwa kutuwekea hapa na sisi watembeleaji wa kibaraza hiki tumefaidika nayo.Safi kabisa.

  ReplyDelete
 2. Ninakubaliana na wewe shabaan Ndege anakimudu na kukizungumza vizuri sana kiswahili. Nakumbuka nilikuwa mpenzi mkubwa wa kipindi cha Regina Mwalekwa Redio one stereo siku za jumamosi. Sina uhakika kama kipindi bado kinaendelea.. Shukrani kwa kutuhabarisha na kutuburudisha

  ReplyDelete
 3. Dada - asante kwamba umeipenda hii taarifa ya habari. Hata mimi ilinivutia sana ndiyo maana nikaiweka hapa.

  Godwin - naona ulikuwa umepotea kidogo kwani sijayaona maoni yako fikirishi katika kibaraza cho chote kwa muda kidogo. Wewe ni mmojawapo wa watu ambao naamini kwamba muda si mrefu utaanzisha blogu makini yenye kuchambua mambo ya muhimu kwa undani. Hata sasa maoni yako unayoyatoa katika vibaraza mbalimbali huwa ni maoni makini yenye kufikirisha sana. Usichoke!

  Kuna maoni yako uliyatoa kule kwa Bwaya kuhusu uhusiano wa lugha na uwezo wetu wa kufikiri. Naandika makala fupi kuhusu maoni hayo na nikimaliza tu nitaiweka hapa tuendelee kujadili zaidi. Kazi njema!

  ReplyDelete
 4. Ni kweli kabisa kwa muda kidogo sikushiriki katika mijala endelevu kwenye vibaraza vingi. Lakini ukweli ni kwamba kila siku lazima nipitie/nisome si chini ya blog 15 za Watanzania.

  Kupitia vibaraza vyenu nimejifunza/ninajifunza mambo mengi sana.

  Ninashukuru kwa kunipa moyo, kweli wewe ni mwalimu.

  Nimegundua ninafurahia zaidi kusoma habari zilizoandikwa na watu kuliko mimi kuandika. Ndio maana mpaka sasa sina blog ingawaje niliwahi kujaribu kuanzisha blog kama miaka mitatu iliyopita

  Mimi ni mmoja katika watu wanaoamini ili vibaraza viendelee vinahitaji washikadau mbali mbali kama WAANDISHI(wamiliki wa blog) WASOMAJI, WACHANGIAJI au wanaofanya viwili au vyote vitatu. Mimi binafsi ninajiona kwenye kundi la WASOMAJI NA WACHANGIAJI.

  Ninasubiri kwa hamu kubwa kujifunza kutoka kwenye hiyo makala(uhusiano wa lugha na kufikiri). Kuna muda ninahisi kuna uhusiano ingawaje si wa moja kwa moja. Na kuna muda sioni kabisa uhusiano. Nimeshindwa kujiridhisha.
  NIKUTAKIE KAZI NJEMA!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU