NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, March 22, 2010

SWALI LA KIZUSHI: "KITCHEN PARTY" NI NINI HASA? INA UMUHIMU GANI KATIKA ARUSI NA NDOA KWA UJUMLA?

Picha ni kutoka Blogu ya Zeze
 • Pengine nianze kwa kusema kwamba pengine mimi ni "mshamba" au "Old school" na inawezekana kidogo "nimefulia". Baada ya kukaa Marekani kwa miaka karibu 10 sasa nimejikuta Kiswahili changu kinaanza kudorora na mambo mengi yamekuwa yanabadilika kwa haraka kiasi kwamba si rahisi kwenda nayo sambamba. Hata neno kufulia lenyewe ilibidi niulize lina maana gani.  
 • Hivi karibuni nimekuwa nikisoma mara kwa mara kuhusu "kitchen party" na kusema kweli nimekuwa sifahamu hasa undani wake ni nini. Kitchen party ambayo imenivutia sana mpaka imebidi niulize swali hili ni hii iliyowasilishwa katika Blogu ya Shamim "Zeze" Mwasha. Ati, kitchen party ni nini hasa? Ina nafasi na umuhimu gani katika mchakato mzima wa harusi na ndoa? Tangu hapo kuuliza si ujinga ati! Asanteni.

4 comments:

 1. I don't think I can answer the question here kwasababu sijaolewa bado...yaani mpaka kufanyiwa hiyo kitchen party. Zile nilizohudhuria, sana inakuwa mama na mashoga zake wanamuandalia mtoto sherehe hiyo...so I think ni "kumfunda" mwari pale atakapoingia kwenye maisha ya ndoa na kujitegemea (including how to treat a man in terms of "ahem...lol", usafi, upishi na kadhalika)...si unajua hautokuwa na mama na baba tena so it's all up to you...hicho ndio ninachokielewa mimi ni the whole point ya kitchen party. Ambaye ameshawahi kufanyiwa ndio description yake itakuwa bora zaidi kuliko mimi.

  Pamoja na hayo sielewi pale mwanamke ameachika halafu "somehow" anaolewa kwa mara nyingine, eti wanamfanyia kitchen party...mi nilidhani anajua namna ya kum-treat mwanaume tayari au ndio "revising"? I absolutely don't get it!

  Na naona siku hizi kitchen party zimekuwa a little bit decent maana zamani ilikuwa mmmh!...also naona kama imekuwa "lazima"...yaani unakuwa "pressurized" kufanya coz kila mtu anakukodolea macho. Alongside Send-Off na Reception yenyewe...by the time you are done...you are BROKE! lol

  ReplyDelete
 2. Ina maana kitchen party na send off are different? And then the wedding? Wow. And all of them are extravagant like the one referred to here? And after one year they divorce? Who pays for all the expenses?

  ReplyDelete
 3. They all means NOTHING.
  Sikuwa chochote kati ya alivyotaja Ndg Njage na bado mimi na mke wangu twapendana kuliko maelezo.
  Havina lolote la kusaidia katika ndoa. Ni kuwekeza ukitaraji kudaiwa. Kwanza wengi wafundao maharusi kwenye kitchen parties wameachika

  ReplyDelete
 4. Kitchen party hii:

  http://8020fashions.blogspot.com/2010/03/mishi-bs-kitchen-party.html

  ...ndiyo ilinishtua mpaka nikauliza hili swali. Ina maana hapo bado send off party na halafu harusi yenyewe? Kazi kwelikweli. Ndoa ya aina hii pengine ingetegemewa idumu milele, lakini kama ulivyogusia Mzee wa Changamoto, mambo kama haya hayana uhusiano wo wote na mapenzi na mara nyingi ni kujionyesha tu. Unahongereshwa eti kitchen party yako "imefunika".

  Candy1 - hilo la mwanamke aliyeachika kufanyiwa kitchen party tena nalo neno. Wanawake mnayajua haya mambo tusije tukawaingilia. Wakati wako ukifika usisite kutujuvya!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU