NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, March 10, 2010

TABIA YA KUKOJOA HOVYO YAMPONZA MWANAMICHEZO HUYU

 • Tabia inayokera ya kukojoakojoa hadharani hovyo (ambayo niliwahi kuigusia hapa), katika nchi nyingi za wenzetu ni marufuku na inaweza kukutia matatani. Hiki ndicho kilichotokea tarehe 24/1/2010 wakati mchezaji wa kutegemewa wa timu ya mpira wa kikapu ya Chuo Kikuu cha Villanova aitwaye Corey Stokes alipopewa tiketi (ya faini) baada ya kufumwa na polisi akikojoa hadharani katika sehemu ya kuegeshea magari nje ya baa moja.
 • Mchezaji huyo alibambwa akilimwaga kojo muda wa saa tisa usiku katikati ya magari mawili huku akiwa amezungukwa na wachezaji wenzake. Tukio hili liliripotiwa katika vyombo vya habari, kuandikwa magazetini na mitandao mbalimbali.
 • Kocha wa timu ya Villanova baadaye aliamua kumsamehe mchezaji huyo baada ya kuomba msamaha na kuahidi kwamba hatarudia tena kukojoa hadharani. Isome habari juu ya kikojozi huyu hapa na hapa.
 • Tuwe makini na kuziacha tabia korofi kama hizi tunapotembelea hizi nchi za wenzetu kwani jambo "dogo" kama hili linaweza kukugharimu kitita cha dola, kukulaza selo na hata kuwekwa katika rekodi yako ya kudumu.

3 comments:

 1. Tabia hiyo inaudhi sana, kwetu ndio imekomaa haswa kwa wanaume, utakuta mchana kweupee mtu anachafua mazingira bila aibu.
  Yote kwa yote, hiyo picha yenye onyo kwa kiswahili, he he hee

  ReplyDelete
 2. Keroooooooooooooo!!!!!! Bongo nako kuwe na adhabu! hivi hivi watu wataendelea tu

  ReplyDelete
 3. Candy1: Huku bongo (Mji wa Moshi) ukitema mate tu ama kuangusha karatasi ya vocha ilotumika UNALO BIBI. Utalipishwa faini ya sh 20,000/= mpaka 50,000/= ukamsimulie mumeo ama mkeo! lol

  Tatizo ni pale ambapo tunaona hatua hizi nzuri zinatekelezwa kwa namna ya virakaviraka. Utaona kwa Tz nzima ni Moshi tu! Miji mingine iko wapi?

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU