NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, March 23, 2010

UTAFITI: UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME UNAWEZA KUWA NI DALILI ZA MAGONJWA YA MOYO

 • Kama unahitaji Mkuyati au Supu ya Pweza kabla ya ligwaride, basi ni vyema ukachunguze afya ya moyo wako. 
 • Utafiti mpya uliochapishwa katika jarida la Circulation: Journal of the American Heart Association la mwezi huu unaonyesha kwamba wanaume wanaousumbuliwa na matatizo ya ukosefu wa nguvu za kiume (uzimbezimbe) wana uwezekano mkubwa zaidi ya mara mbili wa kuugua magonjwa ya moyo kuliko wenzao wasio na tatizo hilo.  
 • Utafiti mwingine uliofanywa na madaktari wa hospitali maarufu ya Mayo Clinic unaonyesha kwamba wanaume wenye matatizo ya nguvu za kiume wana uwezekano wa kuugua magonjwa ya moyo kwa asilimia 80 zaidi kuliko wenzao wasio na tatizo hilo. 
 • Japo tatizo la upungufu wa nguvu za kiume linaweza kusababishwa na sababu za kisaikolojia, wataalamu wanashauri kwamba ni vizuri watu wenye tatizo hili wachunguze afya ya mioyo yao badala tu ya kukata njia za mkato kama kula Viagra, mkuyati au Supu ya Pweza.   
 • Kwa habari zaidi juu ya utafiti huu soma hapa na hapa.

2 comments:

 1. sijui nguvu za kiume zinaishaje na zinapunguaje, inahitaji kulinganisha hii. sijui spidi ya manii au usimamaji wa lidude!

  ReplyDelete
 2. Kama wanavyosema wenyewe ...jongoo likishindwa kupanda mtungi...utajua tu. Huna sababu ya kulinganisha!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU