NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, March 17, 2010

UTAJIRI WETU UNAPOGEUKA LAANA. KUNA NINI NORTH MARA GOLD MINE???

 • Japo nilikuwa nimeshawahi kusoma juu ya athari za kimazingira zilizosababishwa na mgodi wa dhahabu wa North Mara, picha hizi kubwa zimenisikitisha sana (bofya mojamoja utazame vizuri)
 • Ni kweli tu masikini kiasi cha kukubali kufanyiwa hivi, eti tu wawekezaji hawa wasiojali wachimbe dhahabu nasi tufaidike? Pengine sielewi kiini hasa cha sakata hili lakini kwa vyo vyote vile, hali hii inatia huzuni na kusikitisha sana. Halafu ukitazama mapendekezo ya serikali kuhusu suala hili (tazama chini ya post hii), mtu unatikisa kichwa na hata kupata kizunguzungu.


Edit: Ripoti ya Wizara ya Nishati na Madini iliyotolewa Juni 4, 2009 inaishia hivi:
*************************
Recommendations:

- Local village residents around the mine should be educated on the environmental impacts caused by vandalism and theft of liners...

- There should be timely reporting of various incidents by the mine to the licencing authority.

- It is proposed that liners be covered with compacted thick materials as deterrent to vandalism and theft.

- Mine management should work on ways to ensure that such environmental incidents do not occur in the future.
***************************
Picha zote ni kutoka hapa; na mapendekezo ya ripoti ya serikali yapo hapa. Unaweza pia kusoma hapa kuhusu suala hili. 

2 comments:

 1. OMG! Inatisha na kusikitisha sana,jamani hawa watu wanahitaji walipwe fidia,hivi kweli wana mtu anawasikiliza kilio chao? pesaza mgodi wao hawafaidiki nazo,wanaofaidika nazo wengine,wao wanaambulia vilema na kupoteza maisha eeeh mungu! kwanini wengine wateseke kiasi hiki?kula yao tabu,mavazi tabu,malazi tabu na maradhi juu? ama kweli dunia ina mengi.

  ReplyDelete
 2. Kaka Matondo, yaani we acha tu. Hali inatisha. Ukikutana na hawa watu wewe mwenyewe utasema labda hatuna serikali.

  Habari hizi ziliandikwa kitambo na wengine na kutokana na tafiti mbalimbali utashangaa kwa nini serikale haichukui hatua!

  http://www.business-humanrights.org/Search/SearchResults?SearchableText=north+mara&x=0&y=0

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU