NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, March 2, 2010

WAKATOLIKI WANAPOKUTANA KUSOGOA - UCHESHI

  • Wakatoliki - wanaume wanne na mwanamke mmoja - walikuwa wanakunywa kahawa kwenye mkahawa jioni moja. Mwanaume wa kwanza akaanza kuwaambia marafiki zake “Mwanangu ni padri, kila anapokwenda kila mtu humwita "Father"
  • Yule mwanaume wa pili akadakia kwa sauti ya juu kidogo “Mwanangu ni Askofu. Kila anapokwenda kila mtu humwita “Your Grace
  • Mwanaume wa tatu akasema kwa madaha “Mwanangu yeye ni Kadinali. Anapofika kwenye halaiki kila mtu humwita “Your Eminence”
  • Yule mwanaume wa nne akazungusha macho kisha akasema. “Mwanangu ni papa. Kila anapokwenda kila mtu humwita “Your Holiness”
  • Mwanamke pekee katika kundi lile aliendelea kunywa kahawa yake kimya kimya bila kujali majigambo ya wale wakatoliki wenzake wa kiume. Kuona hivyo, wale wanaume wakamuomba awaambie cho chote kuhusu mtoto wake. Kwa sauti yenye mamlaka, kujiamini na majivuno kidogo akasema “Binti yangu ni mrefu, maji ya kunde, umbo la wastani namba nane, matiti makubwa, tumbo jembamba saizi 24 na mahips makubwa saizi 44. Anapofika kwenye halaiki kila mtu husema “Oh My God!
***********************

2 comments:

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU