NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, April 9, 2010

FIKRA YA IJUMAA: BINADAMU NA MAPOCHOPOCHO YAKE

Picha kutoka: iheartguts.wordpress.com
****************

Ilani 
Fikra ya Ijumaa hii kidogo imepinda. Natanguliza samahani 
kwa ye yote atakayekereka!
 • Maonyesho haya yanaonyesha kile kinachoendelea ndani ya mwili wa binadamu kuanzia puani, masikioni, tumboni, katika utumbo mwembamba na mkubwa na sehemu mbalimbali zinazotoa uchafu mwilini. Kama jina lake linavyoonyesha kweli ilikuwa ni "gross"
 • Niliondoka hapo nikiwa na maajabu mapya kuhusu mnyama huyu machachari aitwaye binadamu.
 • Swali (pengine la kipuuzi) ambalo mtoa maelezo mkuu katika maonyesho yale aliligusia, na ambalo lilinifanya nifikirie bila kupata jibu ni hili: Binadamu ndiye kiumbe pekee anayepika vyakula vyake na kuviunga mpaka vikapopochoka kwelikweli. Cha ajabu ni kwamba, pamoja na uwezo huu wenye faida na hasara zake nyingi, bado binadamu ni mmoja kati ya wanyama wenye vinyesi vinavyonuka sana.  
 • Cha kushangaza zaidi ni kwamba inavyoonekana kunuka sana kwa kinyesi cha binadamu hakuna faida yo yote kama ilivyo kwa wanyama wengine kama fungo ambao inasemekana harufu hiyo huwa ni kama "GPS" yao inayowasaidia wasipotee katika safari zao.

 • Binadamu (a.k.a) Homo Sapiens hamalizi vituko ati! Na kwa jinsi unavyozidi kumtazama ndivyo anavyozidi "kukushangaza"

  5 comments:

  1. binadamu ni chizi mwenye kujivika kila aina ya sifa, busara nk. anajisifia siiifa kem kem wakati matokeo ya kazi zake ni sumu kwaki na kwa viumbe wengine!!!!!

   ila sasa, ishu ya kinyesi kunuka ni kwa sababu hiyo hiyo ya kuandaa aina nyingi za vyakula.
   ni ukweli mtupu kwamba harufu ya mtu anayekula nyama kinyesi chake ni kali kuliko asiyekula nyama. hii ni kwa sababu nyma huoza ikiwa tumboni, hata baada ya kuchinjwa, nyama huoza mapaka inaliwa. na inaoza zaidi na hivyo kinyesi cha mla nyama kinanuka zaidi na zaid

   kutana na kinyesi au ingia chooni alikotoka mtu aliyekula nyama ya kuchomwa, kuchemsha nakukaangwa harafu akala samaki na kunywo pombe za kutosha, wewe!! utajuuuta kuwa na choo cha ndani

   ila sasa binadamu katengeneza marashi mnaita air fresha kupunguza harufu

   ila sijui Matondo ulikuwa unafikiria nini katika kutuambia hili, je ulinusu kinyesi chako chooni au ulijipangusa harufu ikazidi kukufuata???
   ni swali tu la ijumaa hii

   ReplyDelete
  2. Kamala - sikufikiria cho chote. Ni hayo maonyesho ya Grossology ambayo yanazunguka dunia nzima. Unaingia kwenye utumbo mkubwa na kujionea jinsi mambo yanavyofanyika huko na unaweza kushangaa kwamba mapochopocho yale matamu sasa yamegeuka uchafu wenye harufu kali kuzidi ule wa simba anayekula nyama mbichi...

   ReplyDelete
  3. Sisi tunaokaa Uswahilini ndio tunafaudu. Msururu asubuhi kwenda msalani na harufu za kila aina. Uzuri ni kwamba vyoo vyetu vingi havina paa vinginevyo watu wangeweza kufaint

   ReplyDelete
  4. annony, nimewahi kuishi uswazi jijini Dar, najua unachokisema

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU