NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, April 2, 2010

FIKRA YA IJUMAA: IPI NI RAHA KUU MAISHANI???

 • Tunasaka pesa usiku na mchana mpaka tunadai eti muda hautoshi!
 • Tunajirundikia "vijisenti" kwa kadri inavyowezekana, potelea mbali hata kama ni kwa njia za haramu!
 • Tuna........
 • Halafu siku ya siku inapofika, tunaacha vitu vyote tulivyohangaikia katika maisha yetu, tunavishwa "masulupwete" yetu na kutupwa gizani...
 • Upo mkondo wa mawazo unaodai kwamba pengine lengo letu kuu mojawapo hapa duniani ni kusaka raha..
 • Kama hivi ndivyo, ati ni raha gani ikupayo raha sana hapa duniani hadi ukaridhika na kusema kwamba sasa hata ukiondoka utakuwa umefaidi?
Ijumaa na Pasaka njema kwa waaminio. 

6 comments:

 1. Raha ni kuokoka na kumtegemea Yesu. That is it, hakuna kingine

  ReplyDelete
 2. binadamu anatafuta raha, furaha na amani. lakini kadri aitafutavyo ndivyo asononekavyo! sasa anabakia analia.

  tunaishi jana (majuto) na kesho (hofu)

  ila furaha na aamani ya kweli vimo ndani mwetu na sio nje yetu kama tudhanivyo

  kukua kiroho husaidia sana pia

  ReplyDelete
 3. Pesa, anasa na takataka nyingine haziwezi kumpa mwanaadamu furaha kamwe...

  Hebu jaribu kuwasaidia wale wenye shida na ndipo utakapoipata furaha ya milele...

  ReplyDelete
 4. Hebu tuacheni kubabaishana hapa. Kwangu mimi raha ni pale ninapopata janajike lenye matako makubwa na kwenda kulimeng'enyua usiku kucha. Hakuna raha inayozidi hii hapa duniani. Jaribuni muone.

  Hata ukiokoka bado utahitaji kuwameng'enyua wanakwaya au walokole wenzako humo humo kanisani. Acheni unafiki!

  ReplyDelete
 5. Final anony. mkorofi wewe. Nani alikwambia walokole wanameng'enyuana wao kwa wao. Anyway, comes to think about it. One of the satisfying moments in my life ni pale ninapokatwa whole night na real man asiyezubaa kitandani. Nothing compares to real orgasm ya mwanamke - and I think that this is very relieving and yes raha 100%

  ReplyDelete
 6. Anony (April 4, 2010 4:28 PM ) na Koku: Duh!

  Inawezekana ni kweli msemayo kama ndicho unachoamini kuwa ndilo kusudio la wewe kuja hapa duniani. La sivo utakuta ni majuto matupu kwa hicho unachokisema kuwa ni raha!

  Raha/furaha ya kweli imo ndani mwetu kama Omwami Kamala anavosema. Hata ukiwa na mipesa kama hujaigundua hiyo raha/furaha ilioko ndani mwako ni kazi bure.

  Ndiyo sababu unakuta mtu anatafuta mipesa halafu inamtesa: Nyumba ina mgeti mkuuubwaaaa na fensi ya umeme! Halafu Milango na madirisha yana grill. Kuna mlinzi na mbwa Mkali! Chumba cha kulala kuna grill! Chini ya mto anaolalia kuna Bastola!... :-(

  Kama mipesa ilaleta raha/furaha mbona yote hayo? Aaaagh! N hicho ni kipengele kimoja tu bado hatujazungumzia cha mabibi na mabwana wenye kuwapa maraha (?)

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU