NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, April 23, 2010

FIKRA YA IJUMAA: LEO TUTAFAKARI UBINADAMU WA BINADAMU (A.K.A "HOMO SAPIENS")

 • Ati, kama binadamu (a.k.a Homo Sapiens) ana ubinadamu, anajisikiaje anapowaibia binadamu wenzake waliomkabidhi madaraka na kujirundikia mamilioni ya dola huku akiwasikinisha na kuwaacha wakiishi katika hali kama hii? Je, hulka ya kibinadamu inamsuta anapowaona watoto wa wakulima wakiwa hivi wakati wa kwake wanabwia unga majuu?
 • Ubinadamu wa binadamu uko wapi anapowaibia watu wa taifa lake na kujijengea majumba ya kifahari kama hili la dola 35,000,000 la Teodoro Nguema Obiang kule pwani ya Malibu, California wakati wananchi wenzake wanaishi katika vibanda vya nyasi?
 • Mifano ya aina hii iko mingi lakini nadhani lengo kuu la Fikra ya Ijumaa hii limeeleweka. Ati, inawezekana ubinadamu wa binadamu umegota na sasa ameanza kusonga mbele kwa kurudi nyuma kama hii picha hapa chini inavyotuonyesha? Kwa ubinafsi huu wa kinyama, binadamu anaelekea wapi? 

 • Wikiendi njema!!!

8 comments:

 1. Binadamu tumejawa na ubinafsi,chuki zisizoweza hata kuelezeka.
  Wikiend njema.

  ReplyDelete
 2. kazi ipo, ni changamoto kubwa, hata kanisani wanataka sadaka kuubwa bila kujali kipato nk

  tunaipenda saana miili yetu kuliko roho

  ReplyDelete
 3. Umimi ni mkubwa mno katika binadamu, huwa nasikitika sana ninapoona watoto wanasimulia ya kwamba leo chakula hakikuwa kitamu shuleni, au mimi sitaki nguo hii, au kiatu hiki. Ukizingatia kuna wengine hawana hata chembe. Mwisho mwema wa juma nawe pia!!UPENDO DAIMA.

  ReplyDelete
 4. Binadamu hajui kwa nini yuko hapa

  Ujinga umemjaa kiasi cha kuamini kuwa yuko kwa ajili ya 'eat,.....drink......merry' na hapo ndo shida inapoanzia :-(

  ReplyDelete
 5. Prof. Hili suala linasikitisha sana kwa kweli. Halafu, kwa nini hili tatizo ni sugu in Sub-Saharan Africa tu? Mbona kule kwa waaarabu (Tunisia, Morroco, na Algeria)haya mambo hakuna? Yaani hawa viongozi wetu wamesababisha kila unapoangalia, ni RUSHWA TU, tena inakuangalia bila aibu. Wao wanachofanya ni kujilimbikizia mali tu, hali wananchi wa kawaida wanaendelea kulala na njaa. Yaani hii ni aaibu kwelikweli. Tunaongozwa na watu wenye tama, na wenye kupenda matumbo yao na familia zao, badala ya kujali maendeleo ya wananchi wao.
  Yaani kila unapoangalia; miundombinu mibovu, wakulima wanakopwa mazao yao, Afya ya jamii balaa, elimu ndio inazidi kudidimia, life expectancy,usitake hata kujua, unemployment? Mtume, ndio hata usiseme, kuna baadhi ya sehemu imefikia mpaka asilia 40. Ukienda kuangalia public fund, zote zinaishia kwenye mabenki ya kigeni, huku wananchi wanaendelea kutaabia.
  Hebu tuchukulie mfano wa huyu FURAUNI Sani Abacha kutoka kule Nigeria. Inasadikika kwamba huyu bwana aliwaibia Wanaigeria POUND BILLION 4, just imagine! Hizi pesa zote za nini? Pesa ambazo familia yake iliamua kurudisha, tena kwa kwa hiari, wakati wa General Abasanjo ni 2.1 billion Dollars. Jamani! Huyu bwana alikuwa ameajiriwa na wananchi wa Nigeria, mshaahara na marupurupu yake vyote vinajulikana, sasa haya mapesa yote kayatoa wapi katika kipindi cha miaka sita tu? (1993- 1996)
  Laiti kama hali ya wananchi wake ingekuwa ni nzuri, labda tungeweza kufumba macho kidogo, lakini watu wa Southern Nigeria hawatufautiani na Watanzania wa mikoa kama Kigoma, Mtwara, na Lindi katika mika ya nyuma, japokuwa asilimia kubwa ya Mafuta inatoka kwao.
  Hapo nyumbani ni hali kadhalika. Viongozi wanazidi kulimbikizia mali, hali wananchi wa kawaida wanaendelea kuumia. Kwa kweli hii hali ni ya kutisha. Kwa mtazamo wangu, ni bora kuiga nchi kama CHINA jinsi inavyopambamna na rushwa. Ukitiwa hatiani tu kwa kula rushwa, adhabu yake ni CAPITAL PUNISHMENT (wao wanapenda sana risasi ya usogoni)
  Wapo watakaosema kwamba this is too much! Well, tuangalie maisha ya mwananchi wa kawaida ambaye anaishi kwa less than a dollar a day ndio tutajua hali halisi iliyo. Rushwa inagusa maisha ya kila siku ya mwananch wa nchini: madawa hospitalini, walimu na madawati mashuleni, barabara na ajali za kila siku, mahakama zenye kupindisha sheria, na ulaji wa kodi za wavuja jasho. (by the way, wengine tunashukuru Mungu, kwani tulisoma wakati wa UPE Original)
  Tukiendelea kulifuga hili GONJWA, basi tujuwe kwamba kifo ndicho kitakachotuumbua.
  Prof. thank you for your efforts to shine yet another light on this troubling issue.

  *Waliotutawala wanakamsemo kasemao:
  ”Those who forget the lessons of history are doomed to repeat them.”

  Karumanzira.

  ReplyDelete
 6. Kamala - kwani watu wa kanisani wenyewe wakale wapi? Ni nani anayelipa bili za umeme, majengo, nyumba, gari na suti za mchungaji? Ni fungu la kumi la Mungu....

  Edna, Yasinta na Ng'wanambiti - ubinafsi na chuki ni jambo la kawaida na nadhani ndiyo asili yetu binadamu (kuna nadharia nyingi sana zinazojaribu kuelezea jambo hili). Tatizo ni pale vitu hivi vinapopindukia kimo kiasi cha kuufurusha kabisa ubinadamu. Lengo na kusudi kuu la maisha linapogeuka na kuwa kunywa, kula na kungonoka basi ubinadamu unakosa nafasi katika maisha ya binadamu.

  Karumanzira - Mpaka leo serikali ya Nigeria bado inajaribu kukusanya pesa ambazo Marehemu Abacha alificha kila mahali ulimwenguni. Kweli mtu unaiba paundi bilioni 4 za nini? Halafu unakufa unaziacha. Na hapa bado hujamtaja baba yao mafisadi wote wa Afrika Mobutu Sese Seko Nkuku Ngbendu wa Za Banga. Huyu inasemekana ni wa tatu duniani kote katika karne iliyopita akitanguliwa na Mohammed Suharto wa Indonesia na Ferdinand Marcos wa Ufilipino. Kwa Afrika ndiye anashika nambari wani:
  (http://www.guardian.co.uk/world/2004/mar/26/indonesia.philippines).

  Ufisadi ni kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya nchi za Kiafrika kusini mwa jangwa la sahara; na mpaka wananchi wake watakapoamka ndipo pengine mambo yataweza kubadilika.

  Ndiyo maana niliwahi kumgombesha mbunge wangu Mzee wa vijisenti hapa:

  http://matondo.blogspot.com/2009/12/shida-ya-maji-ya-kunywa-vijijini-tatizo.html

  ReplyDelete
 7. Prof. kwa kweli ni hali ya kusikitisha sana. Nadhani wewe na Prof. Mbele, ambao mpo mashuleni mna kazi kubwa sana kuitetea Africa, maanake kila mfano wa umaskini, kutokuendelea, viongozi wabovu, na rushwa inatolewa kwa Afrika.

  Ningependa kukupa pongezi pamoja na bloggers wote kwa kazi mnayoifanya, kwa sababu nyie ndio the CIVIL SOCIETY ya nchi yetu. Endeleeni kupiga kelele, labda ipo siku mambo yatabadilika.

  Tukumbuke kwamba, wakati wa kugombania UHURU, ni watu wachache huko vijijini waliokuwa wanajuwa kinachoendelea. Ni wale wachache tu ambao waliokuwa mijini, haswa sehemu kama Bagamoyo, Tanga, Karagwe, Ujiji, na D'salaam, na ambao walikuwa na mwamko na moyo wa kudai uhuru mpaka tukafanyikiwa, leo hii karibia miaka 50 baadaye, na tunaendelea kula matunda hayo.
  Kwa hiyo, SHIME MABLOGGERS kwa kazi mnayoifanya.


  KARUMANZIRA.

  ReplyDelete
 8. Karumanzira - Asante kwa wito wako. Ni kazi yetu sote kulipigania bara letu na hasa nchi yetu nzuri ya Tanzania. Tulifanikiwa kuwa na kiongozi ambaye, mbali na matatizo yake yote, aliipenda nchi yake na bado anaheshimika sana duniani. Mimi nadhani mahali pa kuanzia ni katika mfumo wa elimu kwani elimu ndiyo hasa muhimili wa mambo yote. Ikifika mahali wananchi wakaelewa kinachoendelea na kuwa tayari kuikaba koo serikali inapoboronga basi tutakuwa tumepiga hatua kubwa. Siku itafika ambapo wananchi watapewa pea za kanga na marundo ya mabati na wanapoingia katika kibanda cha kupigia kura wakachagua mtu wanayeamini kwamba atawaletea maendeleo. Hali hii ikifika hata hao watoa kanga na mabati wataacha kwani watajua kwamba gemu limebadilika. Tusife moyo na asante sana kwa maoni yako ya kisomi changamshi.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU