NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, April 30, 2010

FIKRA YA IJUMAA: TUTAFAKARI KAULI HII YA SOCRATES

Shairi ni kutoka hapa.
 • Socrates - mmojawapo wa vingunge wa falsafa ya Kigriki aliyelichachafya tabaka tawala la Athens ya kale kwa maswali yake yaliyojaa lojiki na mantiki kinzani chokonozi mpaka likaamua kumuua kwa kumnywesha sumu aliwahi kutoa kauli ifuatayo:
"Kitu pekee ninachokijua ni kwamba sijui kitu"
 •  Na ukifikiria vizuri unaweza kuhitimisha kwamba pengine Socrates alikuwa sahihi. Ati ni kitu gani ambacho unaweza kusimama na kusema kwa uhakika kabisa kwamba unakijua? Ati, unaweza kusimama na kusema kwa uhakika kwamba unajua kula? Kulala? Kuendesha gari? Kupumua? Kungonoka? Kufa? Unajua nini???
 • Ati, una uhakika kwamba unakijua hicho "unachojua" kwamba unakijua? 
 • Poleni kwa maswali mengi; na wikiendi njema!!!
********************
 • Ni mwisho wa muhula na ni wakati wa kusahihisha makaratasi ya wanafunzi. Nina wanafunzi wanane wa Ph.D ya isimu na hawa makala zao inabidi zisahihishwe kwa umakinifu wa kiwango cha juu. Ndiyo maana nilipotea kwa siku mbili tatu hivi. Sasa mambo yameanza kupoa kidogo na libeneke litaendelea kama kawaida. Tuwemo!!!

4 comments:

 1. Kaka Matondo ahsante sana kwa tafakuri ya leo. Kitu chochote kikishakuwa poetic, basi ni ulevi mkubwa kwangu. Napenda kusoma falsafa za Socrates.

  Nakutakia kazi njema pamwe wikendi njema.

  Pamoja daima.

  ReplyDelete
 2. "Ati ni kitu gani ambacho unaweza kusimama na kusema kwa uhakika kabisa kwamba unakijua? Ati, unaweza kusimama na kusema kwa uhakika kwamba unajua kula? Kulala? Kuendesha gari? Kupumua? Kungonoka? Kufa? Unajua nini???"

  Dah! Mi nadhani najua sana kufukuzia mademu. Demu mi I swear hanilizii buyu miye. This one I know and I can prove Socrates wrong!

  ReplyDelete
 3. Anony! Una uhakika?

  Miye sijui chochote kwa kuwa hata profession sina....lol

  ReplyDelete
 4. Prof, kwa matazamo wangu, nadhani SOCRATES anaturudisha kwenye ule msemo/methali ya kiswahili kwamba, "elimu ni bahari."

  Kwamba in the face of eternity and the boyond, what every man knows is miniscule.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU