NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, April 16, 2010

FIKRA YA IJUMAA: TUEPUKE CATAGELOPHOBIA

   
 • Kwangu mimi blogu imegeuka kuwa ni shule elimishi ajabu na elimu niliyoipata katika mwaka mmoja niliodumu katika kublogu haifundishwi katika chuo cho chote hapa duniani.  
 • Mbali na mambo mengine, nimejifunza kuwa na uvumilivu, subira na nidhamu kila mara ninaporushiwa madongo. Hili si jambo rahisi kwetu kama binadamu. Nimegundua kwamba katika kila dongo, tukiangalia na kufikiria vizuri kuna jambo jema ambalo tunaweza kujifunza. Kwa hivyo tuache kulalamika na kukurupuka kila mara tunapoambiwa kwamba tumefulia, tumeishiwa na madongo mengineyo. Haya ni mambo ya kawaida tu na tuyatazame kama chachu na uthibitisho kwamba angalau kuna watu ambao wanajali kiasi cha kupoteza muda waokiturushia madongo. Bila shaka katika kila u-hasi mna chembechmbe za u-chanya pia. Ni lazima tujitahidi kuziona pande zote mbili.
   • Pia ni lazima tuheshimu mawazo na hoja kinzani. Tunapopingwa kwa hoja tusikarisike na kuanza kulalamika. Hakuna faida yo yote na kusema kweli hatupaswi kutegemea maoni sambamba na yetu. Tujibidishe kuzijibu hoja (hata zile za ma-anony) kila inapowezekana ingawa najua kwamba mara nyingi huwa hakuna muda wa kutosha. 
   • Asanteni sana wanablogu wenzangu kwa hoja zenu nzito nzito pamoja na ma-anony wote mliowahi kunirushia madongo ya kila aina (Fundi Mangungo upo?). Yenu ni elimu ya kweli ambayo imeinukia kuwa ya muhimu sana katika maisha yangu. Tusongeni mbele. 

   • ANGALIZO: Catagelophobia ni hofu ya kurushiwa madongo.

   4 comments:

   1. kaka Matondo:

    1. Huwezi kupendwa na wote na wala huwezi kuchukiwa na wote

    2. Huwezi kueleweka na wote unaowaelimisha

    Kumbuka:

    1. Watoao vitisho ama madongo ndo wamefulia

    2. Waliofilisika kifikra hawana jipya na ndo sababu wanatumia kila mbinu kuhakikisha kuwa ujumbe unaowakilisha sauti za wanyonge usiweze kufika kunakotakiwa.

    3. kwamba wanaona kuwa umefulia, huna jipya manake ujembe umefika. Na hivo umetimiza wajibu wako kama mwananchi makini.


    Nawaasa pia kama ulivosema kuwa wanaBlog wasiogope madongo kwa kuwa katika KUDONGOLESHWA (samahani mtaalamu wa Isimu kama nimekosea kiswahili unachokithamini sana ...lol) unakua kifikra, kiroho na kimwili kwa maana ya kujua tatizo kwa undani zaidi.

    Tuko pamoja

    ReplyDelete
   2. Mwl.Prof Matondo 'usipodongoleshwa' huwezi kujitathmini vema.Kudongolewa kuchukuliwe katika uchanya wake ili kuleta mabadiliko na kunyanyua ari ya kukubali kukosolewa na sio kuchukia na kuzira kufikiri na kujenga chuki kwa aliyekukosoa bali kumuombea kwa Mungu atende alichokisema.

    ReplyDelete
   3. Madongo ni moja ya changamoto hususani kwa sisi wanablog. MADONGO yana pande mbili HASI na CHANYA nikiwa na maana ya kujenga na kubomoa.Haina haja ya kuwachukia ila tuchukulie yale wayasemayo ni kama changamoto kwetu...Siku zote maadui huwa ni wengi kuliko wale wakutakiao mema.

    ReplyDelete
   4. nawapenda walusha madongo pia, ndo maana nawapa uhuru wa kusema / kurusha madongo yao

    ReplyDelete

   JIANDIKISHE HAPA

   Enter your email address:

   Delivered by FeedBurner

   VITAMBULISHO VYETU