NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, April 15, 2010

HIZI NDIZO ZAWADI NILIZOLETEWA.......

 • Wikiendi iliyopita binti yangu (darasa la tatu) alikwenda Kennedy Space Center kwa ziara ya kimasomo. Baada ya hapo alijiunga na mamake huko na akapitiliza kwenda Disneyland Orlando kujiburudisha pamoja na wenzake. Basi aliporejea nilimuuliza kama kulikuwa na zawadi aliyokuwa ameniletea. 
 • Nilishangaa sana alipotoa kimfuko na kunikabidhi. Nilipofungua nilikuta hizo zawadi tatu - Space Shuttle, Boeing 747 na Hummer. Nilipomuuliza ni kwa nini aliamua kuniletea zawadi hizi na si vikombe au kitabu alisema kwamba ameshanisikia mara nyingi nikiongelea juu ya Space Shuttle, madege makubwa makubwa pamoja na Hummer. 
 • Nilikuwa najua kwamba watoto husikiliza sana maongezi ya wakubwa kwa lengo la kujifunza na kuimarisha uwezo wao wa lugha. Kumbe wanajibidisha hata kujua "hobbie" za wazazi wao na mambo yanayowavutia. Wazazi, tuweni waangalifu kwani tunasikilizwa sana na maneno yetu na aina ya lugha tunayotumia vinayo athari kwa hawa malaika wa Mungu tuliowaleta hapa duniani na kujivika jukumu la kuwalea mpaka watakapoweza kujikimu wenyewe.
 • Basi tuliongea mambo mengi na tumepanga kwamba tutakwenda Kennedy Space Center kushuhudia safari ya mwisho ya Space Shuttle itakaporushwa kwenda katika Kituo cha Anga cha Kimataifa baadaye mwaka huu. Rais Obama ameunga mkono kustaafishwa kwa Space Shuttle mwishoni mwa mwaka huu na amesema kwamba serikali ya Marekani haitatoa pesa kufadhili mradi mpya wa NASA unaojulikana kama Constellation.

2 comments:

 1. Watu wengi huchukulia ya kuwa watoto hawajui chochote. Kimsing mtoto katika umri wa miaka 3 anasikiliza na kuelewa vitu vingi kuliko watu wanavyofikiria.
  Maneno mnayo ongea nyumbani anaweza kwenda kumsimulia mtu nje mpaka mkashangaa.

  ReplyDelete
 2. Somo hili ni la muhimu sana. Achilia mbali mazungumzo ya kawaida, ni muhimu sana wazazi mnapogombana mhamishie ugomvi wenu mbali kabisa na watoto kwa hii huwaathiri sana kisaikolojia...

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU