NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, April 21, 2010

MBEGU WALETE WAO, KULIMA NILIME MIYE, TENA KWA SULULU!!!

 • Wanafunzi wa darasa la tatu eti tayari wanafundishwa uotaji wa mbegu (germination) – tena kwa vitendo. Basi Alhamisi iliyopita binti akaleta mbegu walizootesha shuleni huku akisisitiza kwamba wameambiwa mbegu hizo ni lazima zipandwe bustanini na waendelee kuzitunza mpaka zikue na kutoa matunda. Walileta mbegu za matikiti maji, bamia, matango na nyanya. 
  • Na kama nilivyotegemea, kazi ya kulima hiyo bustani iliniangukia miye. Basi niliwakumbusha kwamba miye nimekulia kijijini na mara moja niliingia mzigoni. Tatizo pekee ni kwamba huku hakuna majembe ya mkono kama niliyozoea nyumbani na juhudi zangu za kuyatafuta zilishagonga mwamba tangu zamani nilipofika hapa. Hata hivyo sululu ilifanya kazi vizuri tena bila matatizo.
  • Yaani waleta mbegu (kama wanavyoonekana hapa chini) hata hawawezi kutia mguu kwenye nyasi. 
  • Mboga hizi zikishakomaa, nitawakaribisheni tule pamoja! 

   16 comments:

   1. Ha ha ha! Kaka Matondo umenifurahisha sana kukuona hapo unalima na nawashukuru shangazi zangu kwa kuotesha hizo mbegu. Safi sana. Mwenzako nilikuja na jembe langu kwa hiyo hali ya hewa ikiwa ya kulima nitalima maana nina kabustani hapa huwa tunapanda vimboga mboga mbalimbali. Inafurahisha sana kuona wengu bado tunafurahia utamaduni wa nyumbani. Kweli vyumbani ni nyumbani. Mwaka utakaoenda nyumbani tena basi usisahau kununua JEMBE.

    ReplyDelete
   2. Yasinta - uliwezaje kusafiri na jembe kwenye ndege? Nadhani kuanzia mwaka huu nitakuwa nalima bustani ili hawa wanao nao wajifunze. Nikienda nyumbani nitajaribu kuja na jembe na hata wakilichukua watu wa "eapoti" hakuna neno. Asante kwa ushauri.

    ReplyDelete
   3. Matondo, ukimaliza kulima hiyo ingwe yako, jaribu kufungua mtundiko kuhusu ulipojibu "mama yangu/wangu", na kadhalika, au fungua e-mail yako ya chuoni. Kuna majambo mawili nahitaji msaada wa umahiri wa Kiswahili, tafadhali!

    ReplyDelete
   4. Kunradhini, "ingwe", ISOMEKE "ugwe".... na sentenso iendelee kama hivi:

    Matondo, ukimaliza kulima huo ugwe wako, jaribu..."

    ReplyDelete
   5. Anony - nimekupata. Nitakujibu kwa ufasaha wikiendi hii. Ni mwisho wa muhula, na kama unavyojua hapa mwanafunzi ni mfalme. Kwa hivyo tumebanana kweli kweli!

    Asante kwa maoni na maswali yako fikirishi!

    ReplyDelete
   6. Na nikirejea kwenye kichwa cha habari kinafikirisha sana.

    Kwamba "mbegu walete wao, kulima nilime miye, tena na sululu" Nadhani umesahau neno moja. Ungeongeza 'tena na sululu na MIWANI' manake naona umevaa miwani (au macho yangu mabovu?)


    Kwa kweli kazi unayo. Nasubiria kula hizo mboga.

    ReplyDelete
   7. Ng'wanambiti nawe. Miwani inakuzingua nini? Bila miwani ningeweza kujigida sululu miguuni...karibu sioni mbali naona, si maajabu haya

    ReplyDelete
   8. Ha ha ha Watu bwana umeniacha haoi kweli hapa raha kweli kublog. Kaka mimi nina nyego pia ni lazima niendeleze utamaduni wangu nije bila vifaa huku itakuwaje sasa.

    ReplyDelete
   9. Ukiona na kusikia hilo basi usishangae mwanao akilala ilhali amevaa miwani ILI AWAONE ANAOWAOTA....lol

    Kama huoni karibu basi unahitaji jembe la kisukuma yaani lenye mpini mrefu au uwende kwenye pori la karibu ukate mti utengeneze mpini mrefu wa kuanzia mita 5 na ushei :-(

    ReplyDelete
   10. We, Ng'wanambiti wewe. Niende porini nikakate mpini mrefu, nikikamatwa utakuja kuniwekea dhamana? Unafikiri hapa unakwenda kwenye mapori hovyo hovyo na kuanza kukata miti bila mpangilio? Ukikata mti ambao umo kwenye "endangered species" au ukaingia kwenye pori la mtu/serikali mbona kimbembe utakiona?

    Yasinta - kweli nikienda nyumbani safari hii nitajaribu kupenyeza jembe pale eapoti ya Mwalimu Nyerere tuone itakuwaje. Lakini isije ikawa skandali ya kuandikwa kwenye magazeti: MTANZANIA AKAMATWA NA JEMBE LA MKONO KATIKA NDEGE. Ukiniona katika CNN na jembe langu usije ukacheka. Kumbuka ni ushauri wako!

    ReplyDelete
   11. Usiwe na hofu nitakuja kukuokoa au tufanye hivi kwa nini usije sweden kuazima moja:-)

    ReplyDelete
   12. Matondo lini uliwapeleka shangazi zangu Shinyanga? namsifu sana Yasinta wanawe hawaogopi nyasi.

    ReplyDelete
   13. Da Mija - hawajawahi kwenda Shinyanga hawa. Wanakwenda kiangazi hiki....

    ReplyDelete
   14. matondo, bado nasubiri:

    Anony - nimekupata. Nitakujibu kwa ufasaha wikiendi hii. Ni mwisho wa muhula, na kama unavyojua hapa mwanafunzi ni mfalme. Kwa hivyo tumebanana kweli kweli!

    Asante kwa maoni na maswali yako fikirishi!

    April 22, 2010 1:53 AM

    ReplyDelete

   JIANDIKISHE HAPA

   Enter your email address:

   Delivered by FeedBurner

   VITAMBULISHO VYETU