NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, April 17, 2010

"STUDIO ROOMS" ZINAPOPANGISHWA KWA DOLA 1,200 KWA MWEZI

 • Chuo Kikuu cha California cha jijini Los Angeles (UCLA) kimezungukwa na Hollywood, Beverly Hills, Bel-Air na Westwood, na bei ya vyumba vya kupanga ni ghali kweli kweli. Nilipokuwa nasoma huko, bei ya chumba kimoja cha studio kingeweza kukugharimu dola zaidi ya 1,200. Ndiyo maana wanafunzi wengi tulikuwa tunakimbilia mbali kidogo  na UCLA kama vile Santa Monica na kwingineko.
 • Kumbe hali ni ile ile hata Dar es salaam. Ni Watanzania wa aina gani wanaomudu kupangisha hivi vyumba?  Kwa nini vyumba hivi ni ghali namna hii? Ni mahali vilipo, ni ughali wa viwanja au? Wachumi mnajua?
*******************

Bathrooms : 1
Bedrooms : 1
Location:
Regent Estate, Dar-es-Salaam
Living Area (Sqm):
Plot Size (Sqm):
Asking Price: USD 1,200

Tangazo hili ni kutoka Dally Estate.

  6 comments:

  1. Hao wa Dar wamezidisha sana.
   Kigali napo pia nyumba ni ghali. zipo kati ya 1,000 - 2,000 full furnished

   ReplyDelete
  2. Bwana Chib - tunazungumzia nyumba au chumba? Studio ni chumba ambacho hakina sebule - kitanda, jiko na kila kitu viko pamoja na bado ni $ 1,200 kwa mwezi. Hata katika baadhi ya maeneo niliyoyataja kule Los Angeles studio kwa $1,200 bado ni ghali kidogo.

   Oh, Kigali. Kuna rafiki yangu huko ambaye haishi kunichokoza na kuniomba nimtembelee siku moja ili "kujionea maajabu yake muumba!"

   ReplyDelete
  3. Prof. That’s what James Chanson called “The Property Values Bubble.” Huyu mjomba ndie aliyetabiri kuanguka kwa ENRON, remember? Hizi bei za nyumba na vyumba Tanzania kwa kweli inatia kichefuchefu kabisa, yaani utadhani ni yale aliyokuwa anayasema Mzee Ruksa (Alhaji Mwinyi) kuhusu Taifa Stars ya zamani, kwamba ilikuwa kama kichwa cha mwendawazimu.
   Watu wanapata mepesa ya kuiba, lakini hawana vision wala Ideas za biashara, kwa hiyo sehemu rahisi ya kuinvest mapesa yao ni kwenye real estate, na ambayo bei zake hazireflect the Market reality. Bwana mkubwa, na washauri wake wa kiuchumi sijui kama wanaliona hilo, kwamba hayo mahekalu, ni asilimia moja au mbili tu ya Watanzania ndio wenye uwezo wa kuyanunua. Karibia asilimia 80 ya wananchi wanpokea chini ya dola moja kwa siku, sasa sijui ni nani atakuja kuishi kwenye hizo nyumba.
   Sijui thamani ya Real Estate Tanzania kwa upande wa GDP yetu, lakini inaonekana kwamba ni sehemu kubwa sana ya mapesa ambayo yameinvestiwa huko. Tatizo nililonalo mimi ni kwamba, je ikitokea mtikisiko mdogo kama ule uliotokea DUBAI, au yanayoteokea GREECE, na Baba yao U.S.A tutakuwa mgeni wa nani? Dubai bado wana tumafuta kidogo, Greece wamo ndani European Union, Marekani wapo fit, sasa sisi tutafanyaje?
   Haa haa haa! Nadhani muheshimiwa Raisi atahamia ughaibuni ili kuwashawishi wadhungu waje kuokoa jahazi. Najua wengine watasema, hiyo haitatokea Tanzania, lakini yanatokea hapahapa, na tunayaona.
   Yalitokea kule kwa 5- Tigers Asia, tumeyaona Dubai na Greece- Nchi ambazo tayari zilikuwa zimeisha piga hatua. Sasa kwetu sisi, ambako ndio tunaanza dede sijui itakuwaje. Haya jamani, tutashikana mashati, ohhh.
   I hope hao wakubwa tuliowapa dhamana ya nchi yetu wanapay attention. Hauwezi kuwa na Free Market Economy bila kuheshimu SUPPLY AND DEMAND. Kwangu mimi, nadhani common sense ni REGULATIONS, REGULATIONS, REGULATIONS. Haiwezekani nyumba Kinondoni iishinde bei nyumba ambayo ipo Los Angeles, Torornto au Scotlanda, that's insane.
   Hakuna nchi hata moja dunia ambayo ilipiga hatua ya maendeleo kwa kukimbilia kijenga majumba, bila ya kuwa na miundombinu na maendeleo kwenye sector nyingine za uchumi.


   KARUMANZIRA.

   ReplyDelete
  4. Well said Karumanzira, Well said. Indeed.

   ReplyDelete
  5. Mheshimiwa Karumanzira;
   Nashawishika kuamini kwamba wewe ni Mchumi - tena aliyebobea. Asante kwa maoni yako makini. Kwa tulioishi miji ghali kama Los Angeles kidogo inashangaza kuona kwamba kumbe ughali tuliokuwa tunaulalamikia hata hauoni ndani kwa ule wa kwetu. Kwa mtu mbumbumbu wa mambo ya uchumi kama mimi inashangaza kidogo ninapoona kwamba chumba studio kilichopo Kinondoni kinazidi chenzake kilichopo Hollywood kwa ughali!

   ReplyDelete
  6. Mimi kichefuchefu kilinipata tangu mwaka juzi nilipoona eti nyumba bongo inauzwa dola million 3. Sasa mimi swali langu ambalo ningependa nijibiwe na yeyote mwenye jibu ni Akina nani hao wanaokaa kwenye hizi studios?? Inashangaza sana..

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU