NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, April 14, 2010

TUSISAHAU KIJIJINI TULIKOTOKA, TUSIWASAHAU WALIOTUPIGA TAFU HADI TUKAFIKA HAPA TULIPO!

Picha ni kutoka kwa Mjengwa
 • Jana nilikuwa naongea na kijana wangu mmoja kutoka kule Unyantuzu Bariadi. Alinisimulia kisa cha jamaa mmoja katika kijiji cha jirani aliyekuwa ameletwa nyumbani kijijini kwao kuzikwa (Mungu Amlaze mahali pema peponi!). 
 • Aliniambia kwamba ilikuwa aibu tupu na watu waliomleta nyumbani kwao katika safari yake ya mwisho kutoka Mbeya hawakuamini kama kweli hapo ndipo palikuwa nyumbani kwao kwa baba na mama yake. 
 • Walishangaa kuona kwamba mamake mzazi alikuwa anaishi katika kibanda kidogo cha nyasi na kwamba umasikini ulikuwa umetamalaki pale nyumbani wakati jamaa huyu alikuwa anaishi maisha ya kifahari sana kule Mbeya. Kumbe akawa amepasahau nyumbani kwao kijijini alipozaliwa na kukulia, nyumbani kwa mama yake mzazi!
 • Ati, mbona tusahau vijijini tulikotoka? Mbona tuwasahau watu waliotulea na kutusaidia mpaka tukafika hapa tulipo? Wengine hata kijijini tulikozaliwa hatuendi tena, mpaka turudishwe tukiwa katika masanduku. Kwa nini?
 • Kama kuna kitu kikubwa ambacho nimejifunza kutoka kwa Mzee wa Changamoto ni kutoa shukrani kwa watu waliotupiga tafu kwa namna yo yote ile mpaka tukafika hapa tulipo. Naamini kwamba hili ni jambo la muhimu sana katika maisha yetu hapa duniani. Unaweza pia kumsoma Mzee wa Uungwana kuhusu mada hii.
 • Hebu tumsikilize Jimmy Gait hapa akitusihi kurudi kijijini na kuwakumbuka ndugu zetu tuliowatelekeza huko!

2 comments:

 1. Je ni ulimbukeni unaotusumbua ama kujisahau?

  Kuna baadhi yetu tunasema hatuwezi kufanya kazi nyumbani ati tutasumbuliwa na ndugu :-(

  Lakini pia Kaka Matondo: MILA za KIJINGA!!!!!

  Kuna baadhi ya mila kama Waluo na wengineo wanaoamini kuwa kujenga nyumba nzuri nyumbani watauawa kwa uchawi! Ni ujinga kama ukiwa umesoma kuamini vitu vya kishamba kama hivi na ndo sababu unaweza kukuta mambo ya kijinga kama nilokumbana nayo leo asubuhi (http://mataranyirato.blogspot.com/2010/04/karne-ya-21-na-uchawi.html)

  ReplyDelete
 2. Mwl.Prof Matondo elimu ni kubwa kiasi cha kutosha.Tujaribu kuwapeleka watoto wakajifunze tulivyoishi ikiwa ni pamoja na kuchota maji,kukata kuni,kuchunga ng'ombe, na kuwasaidia ndugu sio 'usumbufu' ndo baraka zenyewe. tuendeleze kwetu kama wafanyavyo wachagga ingawa wanazidisha(Cohesivity)

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU