NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, April 8, 2010

UTAFITI: KUJITOLEA KUSAIDIA WENGINE KUNA FAIDA NYINGI ZA KIAFYA

 • Katika Fikra ya Ijumaa iliyopita niliuliza swali lisemalo "Ipi ni raha kuu maishani?" Baadhi ya maoni yaliyotolewa ni haya kutoka kwa mwanaharakati na mchambuzi Dada Koero Mkundi. Yeye alisema hivi:
**************** 
Koero Mkundi said...
"Pesa, anasa na takataka nyingine haziwezi kumpa mwanaadamu furaha kamwe... Hebu jaribu kuwasaidia wale wenye shida na ndipo utakapoipata furaha ya milele..." 
****************
 • Dada Koero yuko sahihi. Watafiti sasa wamethibitisha kwamba kujitolea kusaidia wengine kuna faida nyingi za kiafya. Watu wanaoshughulika na mambo ya utambuzi (akina Kamala) wanasema kwamba pengine hili ndilo lengo na kusudi kuu la maisha yetu hapa duniani. 

 • Watu wanaojitolea pia huishi maisha marefu zaidi kuliko wenzao wasiojitolea.
 • Katika utafiti huu washiriki walijitolea kufanya shughuli za kawaida tu  kwa watu wasiowafahamu mf. kusafirisha wagonjwa, kuwasaidia wazee na wasiojiweza kazi za nyumbani, kulea watoto na shughuli nyinginezo. 
Mzee Matonya akiwa kazini
 • Japo kusaidiana ulikuwa ni utamaduni wetu wa tangu zama na zama, mikondo ya maisha ya kisasa tayari imeanza kutujengea misingi ya kibinafsi na sasa ni wazi  kwamba mambo si kama zamani. Pengine huu ni wakati mzuri wa kuuendeleza utamaduni wetu mzuri wa kusaidiana. 

 • Tendo moja lililofanywa kwa upendo wa kweli linaweza kuwa na nguvu kubwa ya kubadilisha mtazamo na maisha ya mtu hasa ambaye hatumfahamu. Mbali na kuwafaidisha wale tunaojaribu kuwasaidia kwa kujitolea kwetu, inafurahisha kama nini kuona kwamba kwa kufanya hivyo nasi tunafaidika kiafya ya kimwili, kijamii na kisaikolojia.
Kijana Msamaria Mwema kule India
 • Habari zaidi kuhusu utafiti huu zinapatikana hapa. Unaweza pia kutazama mikakati ya Wamarekani katika suala la kujitolea hapa.

  5 comments:

  1. mimi ni mwanafunzi wa utambuzi. nilichojifunza sasa ni kuanza kusherehekea sikukuu. sherehe zenyewe itakuwa ni kwenda mahosptalini kwani ulinifundisha kitu cha nguvu

   ila yaweza kuwa kweli japo mimi sipendi kuishi muda mreefu sana

   ReplyDelete
  2. Bwana Masangu niliwasiliana nawe baada ya kunipa barua meme yako ukanishiti. Nakutaarifu kuwa nimekifika sitakusumbua tena. Yote maisha. Lililoandikwa litatimia hata watu wakushiti vipi.
   Nahene lulu.
   Nkwazi Mhango.

   ReplyDelete
  3. Bhebhe Nkwazi Mhango, uli na makoye gambiti....lol

   Yaweza kuwa kweli...kusaidia kuna maana tu pale kutakapofanywa bila nia ya kujionesha ama kutaka misifa :-(

   ReplyDelete
  4. Usikonde kaka. Kuvunjika kwa kulego si mwisho wa uhunzi. Tutaunda tu kaka. Good enough wote tuko anga za juu tukiwinda.
   Nkwazi

   ReplyDelete
  5. Ng'wanangwa Nkwazi;
   Mbona nilikuandikia e-mail ndefu kuhusu ile ishu yetu? Nitaitafuta hiyo e-mail nii-forward tena kwako. Tuwasiliane pembeni kwani kupigana vijembe na kulalamikiana hadharani namna hii kama vile kuna kitu tunadaiana kwa wanaume wazima wala si vyema. Tuko pamoja ndugu yangu.

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU