NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, April 20, 2010

VIINIMACHO VYA UCHAGUZI MKUU VIMESHAANZA RASMI: “WAPIGANAJI WA KWELI” WATOA TAMKO!!!

Lisome kwanza tamko la "wapiganaji wa kweli" 
linalozunguka sana mtandaoni HAPA (pdf).
 • Mtu unaweza kujiuliza, hawa “wapiganaji wa kweli” walikuwa wapi? Ni lazima wasubiri mpaka uchaguzi ufike ndipo upiganaji wao uchemke namna hii? Tutajuaje kama siyo watu ambao wana wasiwasi wa kupoteza ulaji wao katika uchaguzi wa mwaka huu na sasa wanatapatapa? Kama wana ujasiri wa kutaja majina ya “maadui” ndani ya ile nyumba kongwe, mbona wasiwe na ujasiri wa kujitaja majina yao? Bila kutaja majina yao (ukijumlisha na e-mail ya yahoo), watu makini wanaweza kutilia shaka lengo hasa la tamko lao hili, pamoja na uzito wake.
 • Pamoja na maswali haya chokozi, mambo wanayoyaibua hawa “wapiganaji wa kweli” ni mazito na yanastahili kutazamwa, kujadiliwa na kutathiminiwa kwa jicho pevu. Naamini kwamba "wamiliki" wa nyumba (kongwe) wanajua kwamba nyumba idumuyo ni ile irekebishwayo na kufanyiwa matengenezo kila inapolazimu kufanya hivyo. Swali la msingi linaloweza kuulizwa hapa ni hili: ni nani atakayeyatekeleza madai haya gonga-kichwa ya hawa wapiganaji? Nauliza hivi kwa sababu mambo wanayoyazungumzia siyo mapya na chama kimojawapo cha upinzani kimekuwa kikipiga kelele hizi hizi kwa muda mrefu sasa. Je, ni kweli tutaona mabadiliko?
 • Uchaguzi ndio huo umeshaanza na bila shaka tutaona mengi. Na muda si mrefu mvua ya kanga, vitenge, chumvi, sukari, baisikeli, mabati, pikipiki na mabulungutu ya pesa itaanza kuwanyeshea wapiga kura. Neema iliyoje!
 • Mungu Aendelee kuibariki Tanzania ili, kama kawaida yetu, tuvuke uchaguzi huu kwa amani na salama. 

  2 comments:

  1. Sasa hawa wapiganaji ambao hata majina wanaficha, wanapigania nini?

   Ni hivi: Kama una uhakika na unachosema na kwa hakika ukiamini kuwa unachokisema kinastahili kupewa uzito, na bado wewe huyo huyo unaficha jina, tukueleweje?

   Mimi naona huu ni mtiririko ule ule wa utamaduni wetu wa unafiki.

   ReplyDelete
  2. Hapa hakuna jipya. Hawa ni wachovu wa CCJ tu wanatapatapa. Watu wenyewe waoga fyata mkia. Utapambanaje wakati ukiwa na woga huu wa kitoto? CCM ni nambari wani na kwa mtindo huu itabakia madarakani MILELE, no matter what!!! Wapiganaji wa kweli my foot. Kafieni mbali huko walafi nyie na hiyo email yenu ya yahoo.....

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU