NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, April 8, 2010

VYOO VYA KULIPIA KWENYE NDEGE VINAKUJA............

 • Kutokana na hali ngumu ya kiuchumi, mashirika mengi ya ndege yamekuwa yakifanya kila njia ili kujipatia pesa za ziada. Hii ikiwa ni pamoja na kuuza vyakula na vinywaji, kutoza ushuru wa mizigo; na matumizi ya mito na blanketi.
 • Jana shirika moja la ndege la hapa Marekani liitwalo Spirit Airlines limetangaza kwamba litaanza kutoza dola 20 - 45 kwa kila mzigo ambao msafiri ataingia nao kwenye ndege - iwe ni laptop au mikoba ya mikononi (kwa akina dada). Bila shaka mashirika mengine yatafuata muda si mrefu ujao.
 • Sasa shirika la ndege la Ryanair limetangaza kwamba litaanza kutoza paundi moja au Euro moja kwa ajili ya matumizi ya vyoo katika ndege zake kwa safari fupi fupi.  
 • Baada ya mlolongo huu, nini kitafuata? Mambo yakiendelea hivi kuna hatari ya baadhi yetu kupiga mguu, au kusafiri pamoja na makontena....

2 comments:

 1. Hivi nyie mnajua OKSIJENI NDANI YA NDEGE NI AGHALI SANA?
  Sasa nadhani tutaanza kuwalipisha na hiyo ili msafiri mkiwa hai.
  Hahahahaaaaaaaaaaaaaaa.

  Sijajua kifuatacho ni nini sasa

  ReplyDelete
 2. Mzee wa Changamoto - ni kweli sitashangaa kama tutaanza kulipia Oksijeni pia....Hawa jamaa inaonekana wako "creative" sana na sitashangaa kama wakiibuka na kitu kingine cha kushangaza zaidi kuliko hili la vyoo...

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU