NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, April 20, 2010

WAMAREKANI NA UMAKINIFU WA KUTUNZA KUMBUKUMBU: RAIS GEORGE WASHINGTON BADO ANADAIWA VITABU NA MAKTABA KUU YA NEW YORK!!!

 • Wamarekani ni watu wanaotunza kumbukumbu sana na karibu kila kitu unachofanya kinaweza kutafutwa na kufukuliwa kutoka katika makabrasha ya kumbukumbu zao. Ndiyo maana watu wenye azima ya kugombea kazi za kuchaguliwa (ukiwemo uraisi) huanza kujiandaa asubuhi na mapema wakijaribu kukwepa kila jambo ambalo litakuja kuwaumbua huko mbele ya safari na kuzizima ndoto zao. 
 • Mkutubi wa maktaba kuu ya jijini New York ametangaza kwamba raisi wa kwanza wa nchi hiyo (George Washington) bado anadaiwa vitabu viwili ambavyo aliazima katika maktaba hiyo zaidi ya miaka 220 iliyopita. Vitabu hivyo - Law of Nations na Debates of the Britain's House of Commons vilitakiwa kurudishwa tarehe 2/11/1789. 
 • Mkutubi mkuu wa maktaba hiyo amesema kwamba japo hawamdai raisi huyo malimbikizo ya faini zinazotokana na kutorudishwa kwa vitabu hivi (dola 300,000) ingekuwa vizuri sana kama vitabu hivyo vingetafutwa na kurudishwa katika maktaba hiyo.
 • Tayari kelele zimeanza kupigwa kwamba pengine kiongozi huyo anayeheshimika sana hakuwa mmakinifu kama inavyosadikiwa; vinginevyo asingesahau kuvirudisha vitabu hivi. 
 • Sisi tunatunza kumbukumbu za viongozi na mashujaa wetu? Kumbukumbu hizi ziko wazi kwa kila Mtanzania? Unaweza kuisoma taarifa hii hapa.

2 comments:

 1. Nimeipenda sana hiyo ya Wamarekani. Hapa kwetu sidhani kama hata kumbukumbu za maktaba miaka 22 tu nyuma zipo hai.
  Na hapa kwetu nadhani mtu akishakuwa kiongozi, kikombe kinafunikwa.

  ReplyDelete
 2. kama maneno yao yamesahaulika unadhani kumbukumbu zinatunzwa?

  Na hata kama zipo nani anajali? Nenda kaombe kanda ya hotuba ya Mwl. Nyerere uone jinsi utakavyo-'zanzamilwa' kama mpira wa kona... :-(

  Si wakumbuka mlivoelezwa kuwa muondoe hotuba za Mwl ktk blogu zenyu wakati wa kumbukumbu yake? Hiyo tu inaonesha jinsi tulivo wabinafsi ktk kila sekta... :-(

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU