NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, April 7, 2010

WANASAYANSI: NGONO INA FAIDA NYINGI ZA KIAFYA

 • Kwa wanyama wengi, lengo kuu la ngono inaonekana ni kuendeleza uwepo wa wanyama hao kutoka kizazi kimoja hadi kingine na kuhakikisha kwamba hawatoweki. Ni kwa sababu hii wanyama wengi wana vipindi maalumu (wakati mwingine ni mara moja tu kwa mwaka) vya kufanya ngono, vipindi ambapo mnyama jike ana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata mimba.
 • Binadamu yeye, kama ilivyo kawaida yake ya kupindisha mambo; na pengine kutokana na maumbile yake kama mnyama dhaifu sana, ngono kwake hailengi tu katika kuhakikisha mwendelezo wa vizazi. Kwa mnyama huyu machachari, ngono imegeuka kuwa starehe na biashara inayomwingizia mabilioni ya dola kila mwaka. Mpaka kuna mkondo wa mawazo unaodai kwamba pengine raha za kingono ndiyo lengo hasa la maisha. Mkondo huu wa mawazo unajulikana kama Eunoterpsia
 Binadamu amejitungia hadi vitabu....

Wanasayansi sasa wanasema kwamba ngono (salama) ina faida nyingi za kiafya. Faida hizi ni pamoja na 
 1. Kupunguza msongo wa mawazo
 2. Kuongeza uwezo wa kinga asili ya mwili
 3. Kupunguza uzito
 4. Kuboresha afya ya moyo
 5. Kuongeza kujiamini
 6. Kupunguza maumivu
 7. Kupunguza uwezekano wa kupata kansa ya "prostate"
 8. Kuimarisha misuli ya "sakafu" ya nyonga
 9. Kukufanya ulale "fofofo"
 10. Kuimarisha upendo na "mshikamano" wa kimapenzi kati ya wenzi.
 11. Kuongeza uwezo wa kunusa.
 12. Kupunguza uwezekano wa kupata homa za mara kwa mara
 Ngono pia imemletea binadamu matatizo...

Unaweza kusoma hapa na hapa kuhusu faida hizi. Zitazame pia hekaheka za binadamu wa kiume hapa kuhusu ngono.

10 comments:

 1. Kuna samaki maarufu kwa jila la Pombooo,au kwa kiingereza anaitwa Dolfin, na yeye nasikia yuko kwam binadamu katika kulifaidi tunda, hasubiri msinu akipata ashikitu anapanda na insemekana anatongoza na pia ana wivu kama alivyo binadamu.

  Ila kaka huo utafiti wako nadani utachochea maambukizi yua Ukimwi, maan wanaume wanavyopenda kujamiiana, akisoma Kamala hapa itakuwa kaazi kweli kweli....I hope hatasoma maandishi haya....LOL

  ReplyDelete
 2. Koero: Duh!

  Ila sidhani kama ni wanaume wote wanaopenda kula tunda ovyo ovyo inategemea na unavomuona weye...lol

  ReplyDelete
 3. Koero; Inasemekana kwamba pomboo ni mmojawapo wa wanyama wenye akili sana. Nilikuwa sijui kama naye ana "ujanja" kama wa binadamu kuhusu suala hili.

  Kamala akikushukia na shoka lake la utambuzi mimi simo...

  Ng'wanambiti - ni kweli si wote, japo inawezekana kuwa ni asilimia ndogo. Tatizo kwa wanaume ni vishawishi. Mojawapo ni hii tabia ya kupita kwenye kontena kila siku na kuanza kugida na kula nyama choma mpaka usiku wa manane....

  Yasinta - Ndiyo. Hii kweli ni habari!

  ReplyDelete
 4. No wonder sina "faida nyingi za kiafya"
  Sisemi zaidi

  ReplyDelete
 5. Mzee wa Changamoto - nimeiona falsafa yako ng'amuzi hapa. Nami sisemi zaidi.

  ReplyDelete
 6. Watafiti kwa visa! Lakini inawezekana ikawa kweli. Bubelwa kumbe una vituko hivi?

  ReplyDelete
 7. Kaaazi kwelikweli!!
  Hapa nimeanzisha bonge la discussion kuhusu faida za ngono(baada ya kupitia blog yako). Kila mtu anatoa ma experience yake, very interesting! Tena mi nimegundua kumbe nakosa faida nyingi sana mana trend yangu ya shughuli hii ni very poor, sometimes as once or twice a year. Sasa naona itabidi nibadilike mana kumbe faida ni nyingi hivi......Siku njema!

  Mdau kutoka Mbeya

  ReplyDelete
 8. Tendo la ndoa unaweza ukalichukulia kama mchezo fulani, Hivyo kuna michezo tofauti na huu ambayo inaweza kuwa na faida hizi na pengine zaidi, Hivyo tusiseme faida hizi zinatokana na kufanya ngono. Tuwe makini, we have the substitute!

  ReplyDelete
 9. thank you for this pretty advise,keep it up....lakini kuna zingine zaidi ya hizo..

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU