NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, April 1, 2010

YULE MWANAFUNZI MLEMAVU KUTOKA GHANA ALIYEPIGWA RISASI NA POLISI WA CHUO APATA NAFUU, AZUNGUMZA


Photo by Rob C. Witzel / Staff photographer
 • Yule mwanafunzi mlemavu kutoka Ghana aliyepigwa risasi na polisi wa chuo hatimaye amepata nafuu na kuzungumza juu ya kisa kilichosababisha mzozo wake na polisi na hatimaye kuishia kutandikwa risasi ya usoni.
 • Tangu kupigwa risasi kwake, alikuwa analindwa na polisi kwa masaa ishirini na nne na pamoja na kwamba ni mlemavu wa miguu na anatembea kwa kutumia magongo, bado polisi walimfunga minyororo miguuni wakati alipohitaji kwenda chooni baada ya kupata nafuu.
 • Leo alikuwa anatarajiwa kutolewa hospitalini na kupelekwa moja kwa moja katika zahanati ya gereza lakini familia yake imeweza kulipa dola 10,000 na kufanikiwa kumwekea dhamana.
 • Matibabu yake tangu apigwe risasi yanakadiriwa kugharimu dola 290,000 na Idara ya polisi inabidi ilipe kwa sababu kwa muda wote aliokuwa amelazwa alikuwa chini ya uangalizi wake. Ni kwa sababu ya kuogopa gharama ndiyo maana leo alitaka kuhamishiwa katika zahanati ya gereza.
 • Anadai kwamba siku aliyopigwa risasi hakuwa na matatizo yo yote na aliwaomba polisi waondoke. Hata walipovunja mlango wa chumba chake, hawakumwambia kunyosha mikono juu au kama alikuwa chini ya ulinzi kama ilivyo kawaida.
 • Habari kamili inapatikana hapa.

1 comment:

 1. Hapa ndio kwaanza KUMEKUCHA.
  Sijui WALIWAZA NINI kufanya maamuzi ya hivi? Lakini na askari nao "huchemka" na kugharimu walipa kodi mamilioni ya pesa.
  Nasubiri kujua muendelezo wa habari hii "tamu"

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU