NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, May 10, 2010

DUNIA INGEKUWAJE BILA MWANAMKE? HAPPY MOTHER'S DAY KWA MAMA NA AKINA MAMA POPOTE MLIPO

Ni mama na mimi nilipokuwa mwaka wa pili Mlimani. 
Hapa ni kijijini Bariadi. NAKUMBUKA!!! 
******
 • Mzee Matondo aliuacha mwili mapema sana na kuniacha nikiwa na miezi mitatu tu. Ni mwanamke machachari shujaa aitwaye Eunice Long'hwe Mugema Dindai ndiye alijifunga kibwebwe na kuhakikisha kwamba ninakua, kusoma na kunifanya niwe kama nilivyo leo.
 • Kutokana na mahusiano haya ya pekee na mama, pengine ndiyo sababu ninayo heshima na upendo wa ajabu kwa akina mama. Kwangu mimi mwanamke ni shujaa na nguzo kuu ya familia na jamii kwa ujumla. Bila mwanamke sijui kama familia nyingi na jamii vingeweza kusimama tisti. Sijui bila mwanamke ulimwengu huu ungekuwaje.
 • Japo Mother's day ilinikuta nikiwa safarini jana, napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru mama na akina mama wote. Asanteni kwa kujidamka asubuhi na mapema kwenda kutafuta maji. Asanteni kwa kusafiri maili nyingi kwenda kutafuta kuni. Asanteni kwa kulea watoto wenu katika mazingira magumu. Asanteni kwa kila kitu.
 • Hebu tuungane na Emmy Kosgei, mwimbaji mahiri wa Injili kutoka Kenya anayeimba katika lugha ya Kikalenjin   katika kuwabariki na kuwasherehekea mama zetu wapendwa kwa yote waliyotutendea na wanayoendelea kututendea. Tuwakumbuke, tuwaenzi, tuwaheshimu na kuwatunza hasa wakati huu wa uzee wao wanapotuhitaji sana. Tusikakawane mijini tukiponda raha kumbe mama zetu wazazi waliotuleta hapa duniani wanateseka vijijiniAti, ni nani kama mama?

Huyu hapa Emmy Kosgei akiuliza Nani Kama Mama?
 • Unaweza pia kusoma hapa na kuwasikiliza Boys II Men katika wimbo wao wa A Song to Mama.

4 comments:

 1. hakuna kabisa kama mama na kaka matondo huu wimbo yaani we acha tu!! nachukua pia nafasi hii kumpa hongera mama yangu Alana Ngonyani pia akina baba wote kwa kutuhusudu sisi akina mama.

  ReplyDelete
 2. Baada ya kudma ile posti ya kaka Mubelwa na kuona maoni yako, ndipo nilipotimka mbio kuja kusoma hii hapa kwani sidhani kama niliwahi kuisoma.
  Mungu ambariki sana Mama Masangu na hongera kwake kwa yote aliyopitia katika kutimiza na kuzidi (meet and exceed) katika jukumu alilotarajiwa kulifanya, kwani wapo akina maama wengi ambao hupelea katika malezi ya watoto wao kwa sababu mbalimbali na hivyo kuwa chanzo cha watoto wasio adabika.
  Hongera sana kwako kaka Matondo kwa ushirikiano wako katika ulezi wa watoto kwani kila nionapo posti zenye kuelezea unavyoijali familia yako, ninatamani wanaume na akina baba wote wangejitwika kisawasawa jukumu lao la ulezi na uangalizi wa familia ili kumwezesha Mama kuweza kutimiza jukumu lake vyema zaidi.
  Hongera sana!
  @Yasinta, hongera kwa ulezi mwema wa wanao na familia yako. Akubariki Mwenyezi kwa unayoyafanya.

  ReplyDelete
 3. Hongera sana matondo kwa kumkumbuka mama. Najaribu kufikiria kama si yeye sidhani leo hii ungekuwa ukinguruma hapo States tena kama mwalimu aliyewahi kupata tuzo ya mwalimu bora wa mwaka, japo sikumbuki ulikuwa na mwaka gani lakini akilini kwangu kuna kumbukumbuku kama hii, kuwa ulishipata tuzo ya mwalimu bora wa mwaka.

  ReplyDelete
 4. Da Subi - Asante. Wewe ni mfano mzuri wa upendo wa akina mama. Siamini kama mwanaume angeweza kazi ya kusaidia kila mwanablogu mwenye tatizo la kiufundi anayeomba msaada kwako. Asante tena kwa maneno yako mazuri.

  Bwana Malkiory - Asante pia kwa maneno yako mazuri. Ukweli ni kwamba hakuna kama mama. Mimi nilelewa na mama pekee na ndiyo maana ninao uhusiano wa karibu sana na mama ambaye kusema kweli kwa sasa ni mzee sana.

  Posti unayoiongelea ni hii:

  http://matondo.blogspot.com/2009/10/nakumbuka-siku-niliyotunukiwa-zawadi.html

  Zawadi kubwa niliyopata kutoka kwa mama pengine ni yale mafunzo ya kuwa mtu mwema na kusaidia wengine hapa duniani. Mengine yote ni madogo tu.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU