NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, May 21, 2010

FIKRA YA IJUMAA: TUNASONGA MBELE AU TUNARUDI NYUMA? USHIRIKINA, VIBAKA NA HUKUMU YA PAPO KWA PAPO

 • Huyu kijana ambaye anasemekana ni kutokea Mwanza (haijulikani kama ni Msukuma msije mkaanza kunirushia vijembe/madongo) amepigwa na kuuawa na wananchi wenye hasira baada ya kudaiwa kuwa ameanguka wakati akiruka na ungo akiwa katika safari zake za kishirikina kule Mbezi Luis jijini Dar es salaam siku ya Jumanne (18/5/2010).
 • Nilipokuwa mwanafunzi wa sekondari miaka ile nilikuwa nafikiri kwamba imani hizi za kishirikina zitaanza kupungua baada ya watu wengi kujipatia elimu na "kuelimika". Leo hii tuna mashule ya sekondari mpaka vijijini, vyuo vikuu vinazaliwa kila siku, academy ndiyo usiseme lakini bado imani za kishirikina ndiyo zinazidi kujiimarisha katika jamii. Kuna nini? Kwa wataalamu wa Elimu Jamii (Sosholojia), tatizo hasa ni nini?
 • Inasemekana polisi nao iliwachukua zaidi ya masaa mawili kufika katika tukio hili na kumkuta huyu kijana tayari ameshauawa na wananchi wenye hasira.  

 • Tabia hii ya kuua mtu kwa tuhuma kama hizi au eti kwa vile tu amekwapua simu au saa nayo inatatanisha. Ni kweli maisha ya mtu yanalinganishwa na simu au saa? Wapo wanaounga mkono tabia hii ya kuua vibaka kwa vile eti vibaka wamezidi, lakini sidhani kama hili ndilo suluhisho sahihi na la kudumu. Inabidi tujaribu kutafuta hasa kiini cha tatizo ni nini. Vibaka hawa wanatoka wapi? Kwa nini vijana  wengi wanaamua kuwa vibaka au majambazi? Pengine ni kwa sababu ya mfumuko wa matabaka na ufa mkubwa unaozidi kupanuka kati ya wachache wanaokula na kusaza hadi kutupa makombo majalalani kwa upande mmoja na wale wengi wanaoshindia chips dume au kulala na njaa kwa upande mwingine. Tukijaribu kuchunguza na kutafuta hasa kiini cha tatizo, na kujibidisha kutafuta masuluhisho yenye mashiko, tutakuwa tunajiepusha na misukosuko zaidi huko mbele ya safari. Na wamiliki wa mfumo wasikae na kukenua meno wakidhani kwamba hukumu hizi za papo kwa papo kamwe hazitawagusa eti kwa vile tu wanamiliki vyombo vya dola. Historia ina mifano mingi inayoonyesha kwamba mambo kama haya yakiachiwa yanaweza kuleta mtafaruku mkubwa katika jamii. Wikiendi njema!
  • Kwa habari zaidi juu ya kisa hiki, tembelea blogu ya Amani Masue

  10 comments:

  1. Kaka Matondo hivi ilikuwaje kuwaje huyu Msukuma akasafiri kwa ungo kutoka Mwanza hadi Dasalamu?

   Ha ha haaaaa!

   Kaka, nimekulia mji wa Tunduma, wanaita boda la wajanja. Nikiwa mdogo, mwanafunzi wa shule ya msingi, nilianza kushuhudia wananchi kujichukulia sheria mkononi. Mji ule nadhani ndiyo ulioongoza kwa wezi na wachawi kuchomwa moto.

   Wakati ule nipo shule ya msingi lilikuwa ni jambo la kawaida kusikia mtu katiwa ndani ya gunia, petroli ikamwaga na kiberiti kikafanya kazi. Niliyashuhudia matukio hayo kwa macho yangu..

   Kilichowafanya wananchi kujiundia utaratibu huo, ni tabia ya maaskari kuwaachia huru watuhumiwa wengi. Wananchi wakapoteza imani nao.

   Tabia hiyo ilikoma Ben Mkapa alipoingia madarakani na kuanza kukemea tabia ya wananchi kujichukulia sheria mkononi.

   ReplyDelete
  2. Kaka Matondo hivi ilikuwaje kuwaje huyu Msukuma akasafiri kwa ungo kutoka Mwanza hadi Dasalamu?

   Ha ha haaaaa!

   Kaka, nimekulia mji wa Tunduma, wanaita boda la wajanja. Nikiwa mdogo, mwanafunzi wa shule ya msingi, nilianza kushuhudia wananchi kujichukulia sheria mkononi. Mji ule nadhani ndiyo ulioongoza kwa wezi na wachawi kuchomwa moto.

   Wakati ule nipo shule ya msingi lilikuwa ni jambo la kawaida kusikia mtu katiwa ndani ya gunia, petroli ikamwaga na kiberiti kikafanya kazi. Niliyashuhudia matukio hayo kwa macho yangu..

   Kilichowafanya wananchi kujiundia utaratibu huo, ni tabia ya maaskari kuwaachia huru watuhumiwa wengi. Wananchi wakapoteza imani nao.

   Tabia hiyo ilikoma Ben Mkapa alipoingia madarakani na kuanza kukemea tabia ya wananchi kujichukulia sheria mkononi.

   ReplyDelete
  3. Elimu tu labda ya utambuzi ili tujue kanuni mbali mbali, eti alisafiri kwa Ungo?? inawezekana sana, sasa yanammuua badala ahojiwe ili kama anautaalamu huo atuelezee labda tutumie usafiri wa gharama nafuu, yanamuu ikiwa na maana kuwa yanaamini na kuogopa sana mambo hayo

   unadhani kuna tofauti yoyote kati ya ushirikina na dini zetu hizi?? mbona mazingaombwe ni yale yale kwa lugha na mazingira tofauti kidogo??

   ReplyDelete
  4. This is totally nonsense. Watanzania, kwa sababu ya njaa na umaskini tunakubalu kurudi kwenye maisha ya karne ya 12 na 13 ya WITCH HUNT bila sababu yoyote.Huyu jamaa wamemuonea tu, wala hana kosa lolote. Hakuna cha uchawi wala nini, hapo ni umaskini tu. Badala ya kupambana na rushwa na viongozi wabovu, wanaanza kugeukiana wenyewe kwa wenyewe.
   Uchawi upo bungeni na kwenye baraza la mawaziri katika kutafuta vyeo na madaraka, na sio huko mitaani, ambako kila mtu ana njaa.

   ReplyDelete
  5. Laiti kama hukumu za vifo kama hizi zingeweza kutolewa kwa watuhumiwa wa rushwa na ufisadi mambo yanguwa mwake sana :-(

   Kamala: udhaifu huo hauko katika vibaka tu bali katika nyanja nyingine. Hujawahi kusikia watu kukamatwa wakituhumiwa kujihusisha na kutengeneza silaha zenye kutumia risasi ama kutengeneza mabomu ilhali hawajasoma kama wewe na mie?

   Nini hutokea? hufungwaQ Je haingefaa hao kuendelezwa na kupelekwa pale MZINGA morogoro wakatumika kubuni silaha mbalimbali bora na kupunguza kununua nje?

   Aaagh!

   ReplyDelete
  6. nadhani mabadiliko huwa hayana wakati ambapo husemwa kuwa ni mapema au imechelewa. Nadhani kw kiasi mambo haya yamapungua. watu wamejua njia sahihi.

   ReplyDelete
  7. "....... amepigwa na kuuawa na wananchi wenye hasira baada ya kudaiwa kuwa ameanguka wakati akiruka na ungo akiwa katika safari zake za kishirikina kule Mbezi Luis jijini Dar es salaam siku ya Jumanne (18/10/2010)."
   Naanza na TAREHE. Iko sawia hiyo? Ama wenzetu wa Dar wako mbele zaidi?
   Hahahaha
   Kuhusu ushirikina ....
   DUH!! Ntachangia baadae kidooogo

   ReplyDelete
  8. Mzee wa Changamoto - tarehe ilikuwa ni "typo" kidogo. Imesharekebishwa!!!

   ReplyDelete
  9. Ukiangalia historia ya Uchawi duniani, kuanzia the crazy witch hunt in Europe (http://www.squidoo.com/witchcrafthistory) au ile maarufu ya the Salem witch trial (http://www.eyewitnesstohistory.com/salem.htm) utaona kwamba kwa wakati ule ni wale wenye nguvu (POWER) ndio waliokuwa wanashutumu na kuwauwa wasiokuwa na nguvu. Kwa mfano, the European crazy Hunt ilikuwa ni Kanisa Katoliki dhidi ya wakina mama wakunga na watabibu (Inasemekana wanawake million tisa waliuwawa kutokana na shutuma za uchawi). Kwa upande wa Salem Witch Persecution, ilikuwa ni the Puritans dhidi ya watuhumiwa watatu, ambao moja wao alikuwa mtumwa mweusi (Tituba) kutoka Caribbbean, mwingine alikuwa na shutuma za ukahaba na wa mwisho alikuwa shutuma za ulevi. Lakini cha ajabu ni kwamba, kesi ilibidi ifutwe pale jina la mke wa meya wa jiji la Salem alipohusishwa na scandal hiyo. Hapa unaweza kuona jinsi gani madaraka yanavyoweza kubadilisha mchezo wote-laiti kama huyo mama angaekuwa mke wa hohehahe, na yeye angeuwa
   Tofauti kubwa iliyoko kati ya witch Hunt za huko Ulaya na Marekani na za kwetu kama nilivyosema hapo mwanzo ni kwamba, Ulaya ilikuwa ni wenye nguvu dhidi ya wanyonge. Tanzania, na Afrika kwa ujumla ni walala hoi kwa walala hoi, haswa wakinamama kule vijijini. Hiyo ndio SONGOMBINGO iliyopo. Watu wana njaa na wamechanganyikiwa na umaskini kiasi kwamba hawajuwi ni nani adui yao.
   Ushauri: Nadhani ni muhimu kwa wanablog wote kwa ujumla kulivalia njuga hili suala ili kuwaelimisha wananchi na kuwakaripia wale wenye kuunga mkono jambo hili la kibaradhuli, kwa sababu, watu wanaohusika na haya mambo hawatoki mwezini, bali ni wenzetu na tunaishi nao pamoja. Hili suala ni zito sana nchini mwetu. Kwa mujibu wa website itwaayo www.infidels.com , kati ya 1991- 2001, watu zaidi 20,000 walishutumiwa kwa uchawi na kuuwawa na wananchi wenzao nchini Tanzania. Elfu Ishirini!! Sina njia ya kuthibitisha hizo takwimu, lakini hata kama ni mtu moja, hii hali hatuwezi kuiacha iendelee.

   Kwa kumalizi tu ningependa kuquote kauli ya Rais wa zamani wa Tanzania, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, katika hutuba yake kwa wanakijiji huko Shinyanga mnamo 1987, ambapo alisema:

   You are killing innocent women, some of them your own mothers, grandmothers or old people
   who have all along taken good care of you: how come they suddenly become witches? Do (you)
   pay them back by killing them? (Mesaki 1994: 58).

   ReplyDelete
  10. naona Annony katoa darsa hapo...
   kaka mbona kimya!?

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU