NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, May 14, 2010

BAJETI YA MFANYAKAZI INAPOJUMUISHA NYUMBA NDOGO NA MICHANGO YA ARUSI, SEND OFF NA KOMUNIO...

 • Japo bado kuna usafiri, huduma za matibabu, chakula na mahitaji mengineyo, mahitaji mengine pia si ya lazima (mf. nyumba ndogo, michango ya harusi, michango ya send-off, michango ya komonio...)
 • Japo katuni hii imefumbata ucheshi na dhihaka, inaashiria ugumu wa maisha unaomkabili mfanyakazi wa kawaida wa Tanzania kwa ufasaha. Halafu tunategemea kweli huyu apewe rushwa akatae?

6 comments:

 1. Kaka Matondo kwa mchanganuo huo hata hizo 315,000/= za mbayuwayu wala hazitoshi hata kidogo. Inabidi kima cha chini kiwe walau milioni na nusu.
  Ha ha haaaaaaa!

  ReplyDelete
 2. Dah!! Lugha ni kitu kitaamu sana. Lakini pia... DUH!!!
  Nawaza nikitamka hiyo "komunyo" uhayani watanielewaje?
  We Kaka si umekaa Bk na waijua lugha? Labda kaka Kamala atasaidia kutafsiri.
  Kumradhi kwa kutoka ne yada.
  Ombi: Iandikwe "komunio" labda ita-sound vema (kwa sisi nshomile"
  Hahahaaaaaaaa

  ReplyDelete
 3. Mzee wa Changamoto - hata kwa Wasukuma komunyo si neno zuri sana (-nyo ni tupu ya mbele ya mwanamke) lakini nadhani ndivyo linavyopaswa kutamkwa katika Kiswahili. Kwa heshima yenu Nshomile basi nimeibadilisha na kuiandika kama komunio. Hili hata hivyo si suluhisho la maana kwani ukitamka komunio kwa haraka, si ajabu ikatoka kama komunyo hiyo hiyo tunayojaribu kuikimbia.

  Lugha ndivyo zilivyo na huu ni uthibitisho mmojawapo unaotuambia kwamba lugha ni sauti za nasibu.

  Vipi kuhusu Biblia inapotuambia kwamba Waisraeli walikuwa wanakula "MANA" walipokuwa wanasafiri kule jangwani? Tuwaambie nao wabadilishe kwani nijuavyo mana pia si neno zuri katika Kihaya. Lugha!!!

  ReplyDelete
 4. Ujumbe utawadia tu jamani, maisha haya!!!

  ReplyDelete
 5. "inaashiria ugumu wa maisha unaomkabili mfanyakazi wa kawaida wa Tanzania kwa ufasaha"

  Hiyo inamaanisha kuwa tunaishi kwa ujanjaujanja kwani utawezakuta mtu analipwa 80alfu kisha unapata kadi za mialiko za 150alfu kwa mwezi na zote unachanga, watoto wanakwenda choo, unavaa, unakuwa na pesa za ugimbi na kzalika :-(

  Akili mukichwa....lol

  As for hiyo mineno: duh! Wakati nilipokwenda ujitani na kutamka kuwa nahitaji KINYERO (nikimaanisha mboga/kitoweo) ilikuwa nzugwe kwani kila mtu aliziba macho kwa mikono... :-(

  Na ukisema MANA kwa mjita...mmmh, ni kama kwa nshomirhe!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU