NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, May 1, 2010

MJADALA JUU YA MUNGU, DINI, WOKOVU NA MOTO WA MILELE: MAONI BINAFSI YA MTU ASIYEAMINI KWAMBA KUNA MUNGU

 • Leo niliuona ujumbe huu umebandikwa nyuma ya gari kubwa (SUV) karibu na maktaba nilikokuwa nimekwenda kurudisha vitabu. Katika upande wa dereva alikuwa amekaa mwanamke wa makamo huku akisikiliza muziki kwa chini chini.
 • Japo mimi si mwongeaji sana kiasi kwamba watu wengi husema nina aibu na kwamba eti niko "anti-social", niliamua kuongea kidogo na mwanamke yule na kutaka kujua hasa kisa cha ujumbe ule kwenye gari lake.
 • Kiufupi alisema kwamba yeye haamini kwamba kuna Mungu na hataki  sala na maombi kuendeshwa mashuleni au sehemu yo yote isiyohusika mbali na makanisani na sehemu zingine za ibada. Alijitambulisha kwa makeke kwamba yeye ni "proud atheist" na anaamini kwamba dini ni mbinu tu za kumtawala na kumnyonya binadamu na kumzuia asikue na kufikia malengo yake. Aliendelea kusisitiza kwamba dini ni kwa watu "wasiofikiri" (Bofya hapa).
 • Ningekuwa mlokole pengine ningemwashia moto wa sala, mapambio na kusema  katika roho, lakini nilizungumza naye kidogo juu ya sababu zangu za kuamini kwamba kuna Mungu. Nilimuuliza kama anaamini kwamba eti vitu vyote tunavyoviona na tusivyoviona vilitokea kwa bahati tu kama wanasayansi wanavyotuambia. Jibu lake kidogo lilinishangaza. Alisema kwamba anaamini kuna nguvu fulani ambayo pengine iliendesha na inaendelea kuendesha mambo yote, lakini nguvu hiyo si Mungu na wala haina athari zo zote katika maisha yetu. Tunatakiwa kuishi tukiwa huru bila kutishwa wala kukumbushwa kila siku kwamba tutakufa na kwamba eti tutakwenda katika moto wa milele wakati hao wanaotuambia hivyo nao hawajui na wala hawawezi kuthibitisha kile wakisemacho. Dini, aliendelea kusisitiza, ni njia mojawapo tu ya binadamu ili kuwatawala binadamu wenzake na kuwanyonya kupitia zaka, sadaka na njia nyinginezo. Alitoa mfano wa mambo mengi yaliyowahi kutendwa na kanisa Katoliki. Alitaja pia wasiwasi wake juu ya dini ya Kiisilamu na mambo yanayofanyika sasa kupitia makundi kama Al Qaeda na mengineyo.
 • Mwishowe alinipa kadi yake na kuniambia kwamba kama nilikuwa nataka kuendelea na mjadala ule basi nimtafute. Nilimwomba ruhusa ya kupiga picha huu ujumbe nyuma ya gari lake na kisha nikaagana naye. Kuna mwenye maoni yo yote kuhusu mjadala huu juu ya Mungu, dini, wokovu na moto wa milele?

8 comments:

 1. Kaka Matondo, hii mada ni tete kidogo tu na kutokana na yale yanayoendelea naomba niachie kwanza tuone mwisho wake. Nasema hivo kwa kuwa kama mkatoliki tena alopitia masomo ya falsafa na tauhidi (theolojia) kidogo naweza ambiwa kuwa nimekuwa kama huyo mama.

  Lakini niseme moja tu kwa Mungu YUPO kweli na anatenda kila kitu kama tukimtafuta ktk kweli na ROHO. Natofautiana na huyo bi mkubwa kuhusu nadhania zake ambazo kwa kiwango cha ufikiri wake anadhani yuko sawa.

  Ambacho hatukijui ni kuwa MUNGU yu NDANI mwetu na KAMWE hawezi kutafutwa nje yetu.

  Naacha nsije nkaambiwa kuwa nahubiri theolojia ya UKOMBOZI nkawa excommunicated ...lol

  ReplyDelete
 2. anaweza akawa sahihi kwa mtizamo wake wa kuwep na NGUVU, tatizo hajua kuwa yeye ni sehemu ya hiyo nguvu.

  ila kweli kama unafikiria, wakati mwingine unaweza kerwa na wahubiri wetu wasiojua wakihubiricho au wanaopoteza watu makusudi

  ReplyDelete
 3. Mwalimu, mimi ninafikiri kuna mambo mawili yamechanganywa katika maongezi yako na huyo mama na hoja nzima kwa jumla: dini na mungu. Inaelekea huyo mama haamini katika dini lakini anatambua kuwa kuna muumba. Kumbukeni hata kabla ya sisi waafrika kuletewa ukristu na uislamu, wahenga wetu walikuwa na imani za kiroho na kila lugha ina jina la muumba - na ni jina hilo hilo ambalo wasambazaji wa imani za ukristu walitumia kufundishia dini zao wakati wakiita imani za asili kuwa ni ushenzi. Ninamuunga mkono huyo mama. dini ni itikadi za kiroho kama vyama vya siasa vilivyo itikadi za kisiasa, na kwamba kuna muumba. kwa mfano katika jamii ya wazungumzaji wa lugha ya kihaya aliitwa katonda.
  bwenge

  ReplyDelete
 4. Kuwepo au kutokuwapa kwa Mungu hutegemea na athari za mhusika toka kwa wazazi wake. Kimsingi si wanaoamini Mungu au wasioamini wanaweza kukupa maelezo ya kina kuhusiana na uwepo wa Mungu-HAONEKANI. Kwa upande wa dini, ni kweli ni nyenzo zilibuniwa na watu wachache kuwaibia wengi. Maana ukiangalia zinavyosisitiza watu waaamini siyo waelewe, utajua nimaanishacho. Kuamini maana yake ni kuwa hakika na jambo usilojua kana kwamba unalijua. Jiulize. JE nalijua? Silijui ingawa najipa uhakika. There is where the kamba gets you guys. Kama dini yasingekuwa magenge ya wezi waliojivisha utukufu sawa na wanasiasa, zisingekuwa na vita-maana zote zinalenga kumkomboa na si kumuibia mwanadamu. Dini zote zina asili moja-upagani wa kuabudia mawe, vinyago na masanamu ingawa zinaka na kujificha kwenye utaua.
  Kwa walioko Tanzania wanakumbuka ufisadi unaotendwa na matapeli kama Kakobe, Rwakatale, Gamanywa na matepeli wengine walijivisha majoho. Hii inaweza kukuonyesha ni jinsi gani dini zilivyo magenge ya uhalifu. Al-Qaeda, Al-Shabab na magenge mengine ya ugaidi yanajificha nyuma ya uislam na waislamu vipofu wanayaunga mkono. Huu ni ushahidi mwingine wa upofu utokanao na kuamini. Waislamu wanawatuhumu wakiristo kuabudia sanamu wakati wao wakifanya hivyo kwenye jiwe jeusi liitwalo Al-kaaba wanalosema lilitoka kwenye hekalu alilojenga Ibrahim. Ukiwauliza kwanini jiwe moja na si hekalu watakupa majibu ya ajabu ajabu. Ukiwauliza kisa cha kupiga mnara mawe wakisema ni shetani, jibu nalo shaka tupu! Waulize walokole mtu anawezaje kuokoka na akaendelea kuishi? No logical answer as well. Waulize wakristo waliupata wapi ukristo wakati Yesu alicha wanafunzi. No sensible answer. Waulize waislamu walipata wapi Korani wakati Mohammad hakuiacha. The same yadda yadda story! Mradi sanaa na kila mtu kuvutia ulaji wake kupitia neno la Mungu na Mungu.
  Kimsingi kila kitu kiko wazi kama utaamua kutumia akili vizuri as opposed to imani.

  ReplyDelete
 5. Try to put good graphics to you pages please coz this color does not reflect good

  ReplyDelete
 6. Anony. What color are you talking about? If it is the picture above, I just saw that bumper sticker on a car and I took a picture of it by using my phone. There is nothing I can do about the color as I am not an expert on graphics or anything of that nature.

  Thanks for visiting my blog!

  ReplyDelete
 7. Wewe ni mfanyabiashara, mwanasiasa, muziki,
  mwanafunzi na anataka
  kuwa tajiri, wenye nguvu, na maarufu katika Uzima
  inahitaji nguvu
  ili kufikia ndoto zao. Unaweza kufikia yao
  ndoto na
  mwanachama wa Mwangaza. na hiyo yote yako
  ndoto na
  tamaa ya moyo ambayo inaweza kufikia kikamilifu kama wewe
  kweli unataka
  kuwa mwanachama majina makuu ya
  Mwangaza basi
  wanaweza kuwasiliana na (illumenatirichtemple@gmail.com)
  Nchi ................. ............................. Nchi.
  au
  piga simu miss sarah juu na unaweza pia kuongeza juu ya whatsapp +2348104857337 asante

  ReplyDelete
 8. Wewe ni mfanyabiashara, mwanasiasa, muziki,
  mwanafunzi na anataka
  kuwa tajiri, wenye nguvu, na maarufu katika Uzima
  inahitaji nguvu
  ili kufikia ndoto zao. Unaweza kufikia yao
  ndoto na
  mwanachama wa Mwangaza. na hiyo yote yako
  ndoto na
  tamaa ya moyo ambayo inaweza kufikia kikamilifu kama wewe
  kweli unataka
  kuwa mwanachama majina makuu ya
  Mwangaza basi
  wanaweza kuwasiliana na (illumenatirichtemple@gmail.com)
  Nchi ................. ............................. Nchi.
  au
  piga simu miss sarah juu na unaweza pia kuongeza juu ya whatsapp +2348104857337 asante

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU